BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Saturday, June 30, 2012

FANUEL BENJAMIN NAE AMEJOIN BLOG YA KIJANJA!!! SOMEWHERE BLOG!!!

Anaitwa Fanue anapatikana facebook pia katika page ya unlimited swaggazz.....hapa sisemi mengi ukitaka kumjua zaidi mtafute facebook kwa jina lake hilo!! Aisee Fanuel karibu sana Somewhere blog!!!!


NAKAAYA ALIA KUPORWA BWANA



 Nakaaya akiwa na Peter.
Nakaaya Sumari.

MWANAMUZIKI Nakaaya Sumari, juzikati alimwaga machozi huku akidai kuibiwa bwana’ke na mwanamke mwenzake aliyemtaja kwa jina la Beatrice, Ijumaa linakupa mchapo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Nakaaya amekuwa hana raha baada ya kuzidiwa ujanja na Beatrice ambaye inadaiwa ni mzazi mwenza wa mwanaume huyo anayetajwa kwa jina la Peter.
“Yaani Nakaaya hana raha kabisa baada ya kuchukuliwa bwana wake. Lakini sisi uhusiano wake na Peter hatukuwa tunaujua na inaonekana walikuwa wakitoka kwa siri sana,” alisema sosi huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake .
Ijumaa lilipozinasa habari hizi lilimwendea hewani msanii huyo ambaye alipopatikana alitoa ushirikiano kwa paparazi wetu akisema:
“Ni kweli kumetokea msuguano kati yangu na Peter ambaye nilikuwa nampenda sana na tukadumu kwa miaka miwili, lakini niligundua amempa mimba mwanamke mwingine,” alisema Nakaaya na kuongeza:
“Mimi sitaki shari naye kwa kuwa tabia yake haijanifurahisha, nina mambo mengi ya kufanya kama Peter bado anamzimia basi waendelee ila Beatrice asiwe ananisumbua maana nimechoka na mapenzi ya kushea bwana, bora nizame kwenye game la muziki kama mwanzo,” alisema Nakaaya.
Kwa upande wa Peter, alipoulizwa kuhusu madai hayo, alikiri na kusema kuwa ameamua kuendeleza uhusiano wake na Beatrice ambaye yuko naye kwa zaidi ya miaka mitano baada ya kuona Nakaaya haelekei.
“Nilikuwa nampenda sana Nakaaya lakini nimeshindwa baada ya kusikia ana bwana mwingine wa Kizungu, nisingeweza kuendelea naye bora niendelee kudili na kazi zangu na maisha mengine, mapenzi ya ki-supastaa yamenishinda,” alisema Peter.

RIPOTI KAMILI





Dk Ulimboka akiendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha mifupa (MOI) kwenye chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).


NYUMA ya kipigo alichopewa kiongozi wa madaktari ambao wako kwenye mgomo nchi nzima, Dk. Steven Ulimboka kuna siri nzito, Ijumaa lina ripoti kamili.
Gazeti hili lilinyetishiwa mkanda mzima na mtu aliyekuwa na Dk. Ulimboka (jina tunalo ambaye naye ni daktari) usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
MUVI LA MATESO LAANZA
Jamaa huyo alidai kuwa, wakiwa viwanjani hapo wakipooza koo, walifika watu watano waliojitambulisha kuwa ni askari wakiwa na silaha ambapo walidai kuwa walimfuata Dk. Ulimboka na kumwambia anatakiwa Kituo cha Polisi Kati (Central).
Ilidaiwa kuwa Dk. Ulimboka alishurutishwa kupanda kwenye gari leusi ambalo halikuwa na namba za usajili na kuondoka eneo hilo huku akiacha gumzo kuwa Central anapelekwa kwa ishu gani.
Ikadaiwa kuwa baada ya Dk. Ulimboka kuchukuliwa, marafiki zake walitoka spidi kuelekea Central kujua kulikoni na pia kumwekea dhamana.
Jamaa huyo alidai kuwa marafiki zake walipofika Central hawakumkuta na wala hakukuwa na dalili za Dk. Ulimboka kufikishwa mahali hapo.
Aliendelea kudai kuwa walianza kufanya mawasiliano usiku huo ili kujua rafiki yao alipelekwa wapi lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda.
SIMU HAIPATIKANI
Alidai wakiwa Central, askari mmoja aliwataka kutulia hadi asubuhi wangepata taarifa kamili kwani kwa wakati huo hata simu yake ilikuwa haipatikani.
Jamaa huyo alidai kuwa saa 12:00 asubuhi alipokea simu kutoka kwa msamaria mwema aliyekuwa maeneo ya Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar akamwambia kuna mtu amemkuta akiwa taabani ambaye alimtajia namba kwa shida ili aipige na kutoa taarifa ya hali yake.
“Alisema alimtajia namba tu na hakumsesha tena,” alisema rafiki huyo wa Dk. Ulimboka.
Alidai kuwa baada ya kujulishwa habari hiyo alitaka aende mwenyewe lakini alipoomba ushauri watu walimsihi asiende peke yake.
Jamaa huyo alisema alitafuta watu akaenda nao na walipofika huko walimkuta Dk. Ulimboka aliyechukuliwa akiwa mzima hajitambui na hakuwa na uwezo wa kuzungumza.
Alisema kuwa baada ya kumuona mwenzao alivyochakazwa, wakamchukua na kumpeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Bunju ambapo yule msamaria mwema alitoa maelezo jinsi alivyomkuta.
Rafiki huyo wa Dk. Ulimboka alidai kuwa, katika maelezo ya yule msamaria mwema alisema kuwa alishtuka alipomkuta akiwa porini na hali mbaya huku akiwa amefungwa kitambaa cheusi usoni na kutapakaa madonda mabichi mwili mzima.
Baada ya kuchukuliwa maelezo walipatiwa PF-3 ambapo walifanya jitihada za kumkimbiza katika Hospitali ya Muhimbili kwa kutumia ambulance ya AAR, alipofikishwa tu madaktari wenzake walianza kumpa matibabu ya hali ya juu ili kunusuru uhai wake huku mgomo wao ukiendelea.
MTU ALA KIPIGO
Wakati anafikishwa Muhimbili tayari wanaharakati mbalimbali walishajitokeza ili kumpokea lakini mara baada ya kufikisha mtu mmoja aliyesadikiwa kuwa ‘njagu’ aliingia chooni na akasikika akizungumza na simu.
Ilidaiwa kuwa katika mazungumzo yake alisikika akisema kumbe jamaa hajafa, jambo lililoibua hisia kwamba alijua kilichoendelea.
Ilisemekana kuwa watu waliomsikia wakamchomoa na kumpa kipigo cha mbwa mwizi hadi Radio Call inayotumiwa na polisi ikamchomoka kwenye suruali kabla ya askari waliokuwa doria kumwokoa na kuondoka naye.
KOVA ATHIBITISHA
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alithibitisha kutokea kwa tukio hilo linalodaiwa kuwa la utekaji na kuongeza kuwa uchunguzi unafanyika na sheria itachukua mkondo wake dhidi ya wahusika.
Wananchi waishauri serikali
Wakiongea na Ijumaa mara baada ya tukio hilo kutokea, baadhi ya wananchi wameitaka serikali kuhakikisha uchunguzi wa kina na wa haraka unafanyika na ripoti yake kuwekwa hadharani ili kuondoa utata uliotawala.
Imeandaliwa na Haruni Sanchawa, Issa Mnally na Makongoro Oging.

Dk. Ulimboka: Nakumbuka kila kitu




NI juu ya kilichompata alipotekwa na watu wasiojulikana, muda mfupi baada ya kuokotwa akiwa taabani, mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka amefunguka kuwa alinusa kifo.
Akisimulia tukio hilo, Dk. Ulimboka alisema kuwa alipigiwa simu na mtu aliyejitambulusha kwake kuwa anaitwa Hemed, aliyemwambia kuwa anahitaji kuongea naye, ndipo walipopanga kuonana kwenye Viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar.
Dk. Ulimboka aliyekuwa akizungumza kwa tabu, alisimulia kuwa wakati akiongea na mtu huyo anayekiri kuwa alikuwa wakifahamiana naye kabla, alikuwa na wasiwasi kwani kila mara mtu huyo alikuwa akipokea simu na kuwasiliana na watu wengine ambao hawakuwapo eneo hilo.
Dk. Ulimboka alisema kuwa baada ya muda alishangaa kuona wanaongezeka watu wengine watano wakiwa na silaha, kisha wakamwambia kuwa anahitajika kituo cha polisi na kumvuta na kumuangusha barabarani kabla ya kumuingiza katika gari lenye rangi nyeusi na kuondoka naye.
Dk. Ulimboka alisema kuwa, wakiwa njiani walimpiga na kumfikisha katika Msitu wa Pande na kuendelea kumpiga mpaka alipopoteza fahamu.
Ilielezwa kuwa jamaa hao walimwacha na kuondoka wakiwa na uhakika kuwa amekufa kumbe alikuwa amepoteza fahamu tu hadi alipookotwa asubuhi.

Uchuro vifo vya mastaa




KATIKA hali ya kuendeleza uchuro unaofanywa na mastaa mbalimbali, msanii wa sinema za Kibongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ (pichani) hivi karibuni ametoa mwongozo wa mazishi yake yatakavyokuwa pindi akifariki dunia, Risasi Jumamosi linakubainishia.
RANGI YA JENEZA
Jack amesema kuwa anapenda jeneza lake lipambwe kwa rangi ya fedha (silver) kwani anaipenda sana rangi hiyo.
“Japokuwa wakati huo sitakuwa nikijua kinachoendelea, naomba ndugu, jamaa na marafiki zangu wazingatie jambo hilo,” alisema.
NGUO ZA WAOMBOLEZAJI
Pia, staa huyo amepanga nguo vitakazovaliwa na waombolezaji watakaofika katika msiba wake ziwe za rangi ya pinki na nyeupe.
“Nawaomba ndugu na marafiki zangu wa karibu siku hiyo washone nguo zenye rangi nyeupe na pinki. Rangi nyeupe inawakilisha amani, japokuwa nitakuwa nimekufa, nitapenda kila mmoja abaki na amani kwani kila nafsi itaonja mauti.”
KWA NINI PINKI?
Jack amesema kuwa anaipenda rangi ya pinki na siku hiyo itakuwa inawakilisha upendo kwani yeye ni mtu wa upendo kwa kila mtu.
“Pamoja na kwamba sitakuwa najua kinachoendelea ulimwenguni lakini suala la upendo kwa kila mmoja ni la muhimu. Hivyo, nitapenda ndugu zangu waishi kwa upendo kwani hiyo ni amri kuu ya Mungu ambayo aliagiza tupendane.”
JIDE
Hata kabla ya mwaka haujakatika, msanii wa Bongo fleva, Judith Wambura ‘Jide’ naye aliweka wazi jinsi anavyotaka watu wavae siku ya mazishi yake.
Mbali na hivyo, Jide alitoa hadi mfano wa jeneza analotaka azikwe nalo.
JACK PATRICK NAYE
Naye mwanamitindo, Jacqueline Patrick hakubaki nyuma, alichukua fursa kueleza jinsi atakavyopenda azikwe baada ya kukata roho.

Uwoya, Flora...




MASTAA wawili wanaokimbiza kwenye sinema za Kibongo, Irene Uwoya na Flora Mvungi hivi karibuni wamevunjiana heshima kisa kikiwa ni msanii wa Bongo fleva, Hamis Ramadhani Baba ‘H. Baba’ Risasi Jumamosi linakujuza.
Akizungumza na gazeti hili, Flora ambaye anatoka na H. Baba hivi sasa, alionesha kukasirishwa na kitendo cha Uwoya kumtolea kashfa mwanaume wake huyo mara kwa mara kwenye vyombo vya habari kwa kusema kuwa hayajui mapenzi.
HUYU HAPA UWOYA
Katika mahojiano aliyofanya na jarida moja la burudani hivi karibu, Uwoya bila ya kuumauma maneno, alishusha tuhuma nzito kwa H. Baba ambaye alikuwa mwandani wake wa zamani na kumchana kwamba ni ‘mbumbumbu’ anapofika kwenye kiwanja cha sita kwa sita ndiyo sababu penzi lao likavunjika.
FLORA ANATIRIRIKA
“Anadai H. Baba hajui mapenzi wakati miye ndiyo nimefika, ananiridhisha vya kutosha! Yeye ndiyo hajui mapenzi ndiyo maana hakai na wanaume kila siku anamzungumzia H. Baba. Atakuwa bado anamtaka angekuwa muwazi, asingekuwa anamzungumzia kila siku.
“Kuna raha anazozikumbuka ndiyo maana anaongea sana. Wanaume wote aliotoka nao mbona hawazungumzii? Aseme anachotaka asizunguke,” alisema kwa hasira.
Frola anadai kuwa Uwoya roho inamuuma kwa kuwaona wawili hao wanavyopendana, kama vile haitoshi Frola alisema kuwa Uwoya hawezi kuishi na mwanaume ndiyo maana hata ndoa yake imemshinda.
“Si aliolewa na anayedhani anajua mapenzi, mbona kashindwa kudumu naye?” alihoji Frola.
NI KWA NINI H. BABA?
Kumbukumbu ya miaka kadhaa iliyopita inaonesha, Uwoya aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na H. Baba wakamwagana, hivyo imedaiwa kuwa hafurahi kumuona Flora akifaidi mapenzi motomoto ya H. Baba.
KUMBE NI VITA YA MUDA MREFU
Mbali na Uwoya ‘kumvua’ vibaya H. Baba kwenye jarida hilo kwamba hajui mapenzi, chanzo makini kimeeleza kuwa mara kwa mara Uwoya amekuwa akimtupia vijembe vya dharau Flora kwamba amejiweka kwa mtu ambaye hajui mapenzi.
“Siyo mara moja wala mara mbili, Uwoya anawadharau sana H. Baba na Flora hata hivi majuzi amewachana redioni,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini.

‘MAMA KANITIA AIBU




Wema Isaac Sepetu na mama yake, Mariam Sepetu hawapo vizuri tangu yale mahojiano aliyoyafanya mzazi wake huyo runingani wiki mbili zilizopita akiwachana marafiki wa staa huyo mkubwa wa picha za Kibongo, Risasi Jumamosi linafunguka.
ALIJISIKIAJE?
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum juzi Alhamisi ndani ya Ofisi za Global Publishers, Wema alisema kuwa hawezi kusahau siku mama yake alipofanya ‘intavyu’ kwani aliposikia anaaza kutiririka ilibidi aipigie magoti runinga akiiomba inyamaze akidhani inamsikia.
TUJIUNGE NA WEMA AKITIRIRIKA!
“Kwanza sikuwepo wakati mama anafanya intavyu ‘so’ sikutarajia kama angezungumza vitu vya namna ile.
“Ni kweli mama yangu kama mzazi alikuwa na kila sababu ya kunizungumzia, alikuwa na uchungu na mwanaye sawa! Lakini ‘mai mom’ alipitiliza.”
ALITAKIWA KUHARIRIWA?
“Nadhani kuna vitu vilitakiwa kuondolewa kwa sababu mara baada ya kuzungumza, hali ilikuwa mbaya sana kuanzia kwenye mitandao ya kijamii na hata dada yangu alinipigia simu nikamweleza nilivyojisikia vibaya.”
KANITIA AIBU!
“Nilijua mama kanitia aibu lakini nikajikaza kwa sababu utakumbuka ndo’ kwanza nilikuwa kwenye maandalizi ya uzinduzi wa filamu yangu ya Super Star.
“Nilikaa kimya, nilijifanya kama hakuna kitu chochote kilichotokea lakini si unajua lazima moyo utakuuma tu hata kama ukijifanya kusahau.
“Baada ya kuona nipo kimya ‘aithinki’ siku iliyofuata alinitumia meseji mbaya na ninazo lakini hadi leo sikumjibu.”
TUNAWEZA KUSEMA ALIKUDHALILISHA?
“Yaah…ukweli ‘situwesheni’ haikuwa nzuri. Meneja wangu Martin (Kadinda) alimpigia mama na kumsisitiza mwaliko niliokuwa nimempa wa kuhudhuria kwenye uzinduzi wa filamu yangu lakini amini usiamini mama yangu hakuhudhuria. Kwa upande wa baba naye hakufika lakini alinipa sababu za msingi kabisa nikamwelewa na pia alikuwa akifuatilia kila kitu kwa kuchati na dada yangu kwani alijua niko bize.”
VIPI KUPELEKWA KWA WAGANGA?
“Sijui mama alipata wapi hiyo kitu ‘coz’ sijawahi na wala sijui mambo ya waganga kama alivyozungumza yeye.”
NISAMEHENI SANA
“Kwa yeyote aliyeguswa na mama kwa namna yoyote, naomba anisamehe sana. Yaani magazeti ya Global naombeni muwe wa kwanza kunisamehe kwani yule ni mzazi wangu pamoja na yote, nampenda sana.”
NENO LA RISASI JUMAMOSI
Wema ameamua kutoa la moyoni mwake akiamini kuwa yeye ni staa kwa hiyo ni kioo cha jamii, hataki kuwepo na chuki kati yake na vyombo vya habari, kwa maana hiyo AMESAMEHEWA.

Friday, June 29, 2012

BODA BODA GO! GOOO!......
KUWA UYAONE………..CHECK ABIRIA ALIVOKAA HAPO….., hii sio editing wala cartoon ila nimekutana nayo leo maeneo ya ubungo mwisho! chezea boda boda wewe? BODA BODA GOOOOO!!!!......

Thursday, June 28, 2012

Italia kupambana na Uhispania katika fainali

Italia na Ujerumani
Ballotelli aliifungia Italia magoli mawili na kuifikisha nchi yake katika fainali ya Euro 2012
Mario Balotelli alifunga magoli mawili ya kupendeza mno na kuiwezesha timu yake ya Italia kuishangaza Ujerumani kwa kuifunga magoli 2-1 katika nusu fainali ya Euro 2012, na nafasi ya kucheza mechi ya fainali mjini Kiev dhidi ya Uhispania.
Mabao ya mshambulizi huyo wa klabu ya Manchester City ya England, aliingiza goli la kwanza wavuni kupitia kichwa, na pili kwa mkwaju wa kasi mno katika uwanja wa mjini Warsaw, na Italia kuwathibitishia Wajerumani katika kipindi cha kwanza kwamba ilikuwa na nia kamili ya kufika fainali.
Wajerumani, kufuatia mshituko, walianza kucheza kwa makini zaidi, lakini bao lao la penalti, ambalo lilipatikana katika dakika ya 92, kupitia Mesut Ozil, lilichelewa mno, na halikuweza kuwaokoa.
Italia kamwe hawajawahi kushindwa na Ujerumani katika mashindano makubwa, na wamefanikiwa sasa kucheza mechi nane dhidi ya Ujerumani pasipo kushindwa.
Hii sasa itakuwa mara ya tatu kwa Italia kuingia fainali za michuano hii ya mataifa ya Ulaya, na wataingia fainali kama timu inayodhaniwa kuwa dhaifu ikilinganishwa na mabingwa watetezi Uhispania.
Timu hii ya meneja Cesare Prandelli ilistahili ushindi, kwani sio tu waliweza kupambana na Ujerumani ambayo iliwashinda wapinzani wao kwa urahisi, bali pia walifunga mabao yao mapema katika kipindi cha kwanza.
Timu hiyo ya Azzurri ilikuwa na nafasi ya kujiongezea magoli, lakini ilicheza kwa tahadhari kwa kuhofia kwamba iwapo ingeliongoza mashambulizi zaidi dhidi ya Italia, kulikuwa na uwezekano wa ngome yao kuachwa ikiwa dhaifu, na Wajerumani kuwashambulia.

Bima ya afya kwa raia Marekani

Mahakama kuu ya Marekani imeruhusu kisheria moja wapo ya mapendekezo ya Rais Obama kuhusu kuufanyia mageuzi muswada wake wa afya ambao unakabiliwa na changamotokwa misingi ya kikatiba
Mahakama hio imekataa madai kwamba muswaada huo umevuka-mpaka kwa sababu ya kikwazi cha kuwataka wamarekani wote wanunue bima ya afya.
Mahakimu wanne kati ya mahakimu tisa wa mahakama ya juu walipinga pendekezo hilo.
Inaarifiwa kuwa mahakimu hao ni wahafidhina.
Muandishi wa BBC aliye mjini Washington amesema uamuzi huo wa mahakama kuu ni ushindi mkubwa sana kwa rais Obama.

Beckham hatashiriki Olimpiki


Aliyekuwa nahodha wa Uingereza, David Beckham, amekosa nafasi katika timu itakayowakilisha Uingereza wakati wa michezo ya olimpiki.
Beckham amesema hakuchaguliwa kuwa mmoja wa wachezaji katika timu hiyo inayojumuisha wachezaji kumi na wanane.
Amesema kuwa angependa kuiwakilisha Uingereza na amevunjika moyo kutoka na uamuzi huo.

Mwanariadha wa Kenya matatani

Ezekiel Kemboi
Polisi nchini Kenya wamemchukulia hatua mwanariadha mashuhuri Ezekiel Kemboi kwa madai ya kumdunga kisu mwanamke mmoja Jumatano usiku.
Kemboi anasifika kwa mbio za mita elfu tatu kuruka viunzi na maji. Mwanamke anayedai kufanyiwa kitendo hicho, Anne Njeri Otieno, anadai kuwa mwanariadha huyo alimshambulia wakati alipokataa kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye.
Kemboi, aliambia polisi kuwa wakati alipokuwa anamrejesgha nyumbani mwanamke huyo katika mji wa Eldoret, walishambuliwa na watu wlaiokuwa wamejihami na hivyo akajeruhiwa kwenye purukushani hilo.
Kemboi mwenyewe ni afisaa wa polisi na anajiandaa kwenda mjini London kwa michezo ya Olimpiki.
Hata hivyo Kemboi aliachiliwa kwa dhamana baada ya kulipa dola 595 za Kimarekani na kesi yake itasikilizwa tena mwezi Septemba baada ya michezo ya Olimpiki.
"Tayari niko katika kikosi cha wanariadha watakaowakilisha Kenya kwenye michezo ya Olimpiki. Ninaomba mahakama kunipa nafasi niweze kushiriki " alinukuliwa akisema Kemboi mbele ya mahakama.
Mwandishi wa BBC mjini Eldoret Wanyama Chebusiri anasema kuwa Kemboi alichukua muda wa saa saba katika kituo cha polisi alipokuwa anahojiwa.
Kituo hicho cha polisi pia kilijaa watu waliokuwa wanataka kumuona Kemboi alipofika kwa mashtaka.
Hapo awali, Bi Otieno, ambaye anaendelea kupata nafuu hospitalini, aliambia waandishi wa habari kwamba alikuwa kwenye mkahawa mmoja na Kemboi wakati alipokubali kumpeleka nyumbani usiku ulipoingia.
Mwaka 2004 Kemboi aliyeshinda dhahabu kwenye mbio za elfu tatu aliambia polisi kuwa alivamiwa na wezi alipokuwa nje ya gari lake na kumtaka awape pesa na kisha kumshambulia.
Alisema alichukua hatua hiyo ili kujilinda dhidi ya kuvamiwa na katika purukushani hiyo Bi Otieno akajeruhiwa.

SIRI YA PUMZI KATIKA KUENJOY MAPENZI

 
Sijui nianzie wapi! Topic tete...TUTAPONA TU MDOGO MDOGO


Kwanza, Kuna wanaume ambao Wanawake wao wanalalamika,jamaa wako fasta kuinua mashabiki..Dakika 10 nyingi watu Yangaaaa Yangaaaaa....Washafunga Mahesabu....Ndo kwanza mpenzi anapanda Kilima wewe huyoooo unatiririkaaaaa...Inaudhi na kukera sana,na sometimes,jamaa linajifanya linajuaaaaaaaaaa hadi huwezi hata kuliambia,maana ukiliambia ugomvi...ooh unaleta mambo ya ajabu utakuwa ushapata mtu mwingine...


Ah ah,kama unakosea utaambiwa tu...Jifunze tufaidi wote..Raha ya Mechi ya mpira wa miguu ni magoli,ila Raha ya Mechi hii huwa ni Raha kwa wote...Waingereza wanasema Pleasure for Both....Tiririka muda muafaka.


Upande wa Pili...Kuna Wanawake,Amini usiamini,wamezoeshwa aina flani ya Mapenzi ambayo hawatiririki ng'oo...Wameingia kwenye huu ulimwengu wakakutana na Wanaume flani ambao ni Selfish,hawajali mama katiririka au Lah,wenyewe wakimaliza ndo basi...Filimbi Pyeeeee!Kati!


Hili ni tatizo kubwa.Na likifika kwenye Ndoa ndo inakuwa balaa zaidi....Leo tujifunze Power of Breathing....Inhaling and Exhaling...


Mfumo wa Upumuaji husaidia pumzi kupita kwenye kila part ya Mwili....Pumzi ina-release tension kwenye maeneo yenye tension na kuhakikisha mtu yuko at ease...


This is the Secret behind breathing


Kwa wale wanaume wenye haraka haraka...wenye Kisebengo...Mnawaudhi sana Wanawake wenu na mtasaidiwa kwelikweli na jamaa wanaosimamia kucha..Tena usiombe akamatwe na wale wakongo wa Saluni ndo kabisaaaaa....Fally ipupa haoni ndani,Show ndefu Dar mpaka Kinshasa.


Tafuta muda,wewe na mpenzi...Sio mkionana unarukia tu kama Basi la Kawe limefika...hujui mchuchu ana stress au hana,we unakwea tu...Sio mnazi...Muandae awe tayari kwanza,ndo uendelee

Tumia dakika 5,kaa nae...Fanya mazoezi ya Breathing,,,In and Out mkiwa mmekaa pamoja,mnaangaliana..Inakuwa kama aina flani ya Mchezo but its very healthy.

Hata kama alikuwa na tension,atajisikia released maana Breathing inasaidia kuondoa tension kwenye Mwili.

Na mkianza ile shughuli kumbukeni kuwa na pose kwenye breathing,ili kuendelea kuwa na Oxygen  ya kutosha kwenye Mwili

Kwa wanawake ambao kwao Kilele wanakisoma kwenye Stori za Eric Shigongo please do this...

Before the match do it,hata 5 times hivi ili uwe at ease..na ukiingia kwenye mechi jitahidi kuwa unavuta pumzi ya kutosha and exhale kwa kutumia pua na sio mdomo.

Ruhusu hewa nyingi ndani na uiachie yote,fanya hivyo kama mara 3....

Kamwe usipige kipute huku una mawazo...Mara kazini hivi mara bosi vilee...CONCENTRATE.

Akili yako iwe kwenye Mechi.....Jitahidi kumuangalia jamaamachoni...eye contact helps katika kuelekea kitonga...Sasa nyie mnaopiga kipute Gizani mtajua la kufanya,eye contact mtaipata wapi gizani....

BREATHING CAN CHANGE YOUR SEXUAL EXPERIENCE,TRY IT AND SEE

NAHISI NICKI MINAJ NI MPARE..HII SIO KAWAIDA

Ndio maana siku hizi wadada wa kibongo nao wanafanya hii mambo...Ulaya na Marekani haya mambo yamekuwa kawaida kabisa.

Huyu anaitwa Nicki Minaj ambae mimi nahisi ni Mpare...wanawake wa kipare wanafahamika kwa sifa ya kuwa na Good shapes...Kama kweli anavyoonekana sasa hajafanya mchanganuo wowote ule katika kuongeza maujuzi,ama kwa hakika tusibishane,Nicki ni MPARE!


Tumezoe wazungu ni wembamba na Sony Wega nyuma...sasa huyu inakuwaje??


Kila mwaka akipigwa picha anaonekana duh...


Watu wamekuwa wanasuspect kwamba maybe Nicki huwa anafanya Surgery ya body parts...Lakini yeye mwenyewe akihojiwa mara kadhaa amekanusha hilo na kusema hawezi kuwazuia watu kuongea,na anapenda kuwa centre of attention ila ule mzigo kapewa na mama.


Swali ni Je,mbona ngoma imekua ghafla yaani,kama Graph ya demand and Supply bana....


Hebu tuangalie halafu tukubaliane,ni Surgery au Nicki ni Mpare???


MCHEKI NIKI BEFORE,MWAKA 2010 TU HAPO






HATISHI KIIVYO,HII HATA WACHAGA WANAYO



CHEKI...KAWAIDA TU YAANI



ANGALAU INGEBAKIA HIVI,MASWALI SI SAAANAAA





 CHEKI SHUGHULI YAKE SASA HIVI..GHAFLA BIN VUU KAMA ALIVYODAKWA NA WADAKU







DUUUUHHHH..IMAGINE


 ULALAH FUNDI KALALAH


SASA HII NDO CURRENT,YA JUZI TU AMBAYO WADAU WANASEMA AMEFANYA SURGERY YA 3....WHATS THIS FOR ANYWAYS???WADADA WANAJUA ZAIDI



ABIRIA ALAZIMISHWA KUKAA NA MAITI KWENYE KENYA AIRWAYS


Africa kuna mambo sana aisee.hii imetokea juzi tu hapa,Mwanamke mmoja raia wa Sweden alikuwa akisafiri kuja Tanzania kwenye Likizo yake kwa ndege ya KENYA AIRWAYS


Akielezea tukio hilo,mwanamke huyo anasema jamaa huyo aliyekaa nae alipandia ndege kwenye uwanja wa ndege wa Amsterdam.

Mshkaji alikuwa anaumwa na alionekana akitokwa na jasho jingi sana na kuchechemea,lakini alilazimisha kusafiri.

Muda mfupi tu baada ya Safari kuanza yule abiria alionekana kuzidiwa zaidi na wahudumu walijitahidi kuwa karibu nae muda wote lakini Izraili alionyesha Umafia wake wa ku-operate hadi angani,yule jamaa aliaga dunia wakiwa katikati ya Safari.

Mwanamke yule kuona vile ikabidi aombe kubadilishiwa Siti lakini kwa Mshangao akajibiwa kuwa ndege imejaa na hakuna popote wanaweza kumpeleka zaidi ya yeye kukaa palepale na ile maiti.

Masaa karibu 10 yule mwanamke alisafiri akiwa amepoze na ile maiti just next seat.

Mawanamke huyo,Lena Petterson,alipofika Dar es Salaam aliuandikia uongozi wa kenya Airways kulalamikia ishu hiyo na ndipo Uongozi ulipoamua kumrudishia Nusu ya Nauli yake kama part ya kumpoza moyo Mwanamama huyo.

Nauli aliyolipa Mwanamama Lena Petterson ilikuwa Dola 1400 na alirudishiwa Dola 700 kama Compensation kwa yeye kukalisha siti moja na Maiti na Mwanamama huyo alikubali Fidia hiyo na kuwa mpole.

Sasa kama hiyo ni Kenya Airways,ambao wako very smart kwenye operation zao,Usishangae Air Tanzania ukiambiwa ukae na Magunia ya Viazi uyapakate tena kwenye Siti,sitashangaa!

WEMA SEPETU ANAJIANDAA NA HARUSI

Wiki nzima iliyopita amehit kwenye Blogs,Magazeti,na kila mahali baada ya kumleta mwanadada Staa wa Nollywood, Omotola Jelade kwenye uzinduzi wa Movie yake mpya iitwayo SUPERSTAR pale Giraffe Hotel.Ilionekana kama haiwezekani ila ndo hivyo...Mdada akatua

Katika hali iliyowashtua wengi,Leo,Mwanadada ambae daima yuko kwenye Magazeti, Wema Isaac Sepetu ametoa taarifa kwamba anajiandaa na harusi.

Wema yuko bize akiwaza aina gani ya gauni litamfaa na ameshaomba ushauri kwa watu kadhaa kuhusu choice ya nguo hiyo muhimu

Kwenye page yake ya Twitter,ameandika hili ingawa watu wengi hawakuamini na walimuuliza maswali kadha wa kadha awahakikishie kama ni kweli au ni Movie naye bila hiyana akawaambia ITS FOR REAL

CHEKI TWEET YAKE HAPA CHINI-FOR YOUR INFORMATION,USIPOAMINI HAIYAH ILA NDO HIVYO SASA...DADA HUYOOOOOOO ANAOLEWA!ILA MAHARI BADO

 
MADAKTARI WOTE 72 WAFUKUZWA KAZI MKOA WA MBEYA KWA KUKAIDI AMRI YA KURUDI KAZINI 

***HABARI HII INALETWA KWENU EXLUSIVELY KWA HISANI YA WAANDISHI MAHIRI WA TONE RADIO-MBEYA*88

Katika kile kinachoonekana kuwa Serikali imeamua kudeal na hii ishu kiutu-uzima,wameanza kugawa kichapo kwa Madokta wabishi na kimeo kimeanzia kwenye mkoa ambao siku zote huwa unatoaga vitu critical, MBEYA


Baada ya Madokta kugoma na kuamriwa kurejea kazini ifikapo leo,wakagoma,jamaa wamefanya walichoahidi...WAMETIMUA WOTE

BODI ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewasimamisha kazi madaktari wote 72 kwa kosa la kutoingia kazini kwa siku tano jambo ambalo ni kinyume cha makubaliano ya mkataba.





Imeelezwa kuwa madaktari hao ambao 54 ni wale wa mafunzo ambao waliingia mkataba wa miaka miwili na hospitali ya Rufaa na madaktari 18 ni wale walioajiriwa na Wizara ya afya.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara, alisema kitendo cha madaktari kutoripoti kazini kwa siku tano ni ukiukwaji wa kanuni za utumisha wa umma toleo la 2009 kifungu namba F.16-F17 na F. 27.





"Hivyo kupitia kanuni hiyo madaktari hao wamesimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi za kinidhamu,"alisema Sigara.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Bodi, imeelezwa kuwa siku ya tarehe 23/6/2012 wafanyakazi 15 waliokuwa zamu(Intern Doctors 12 na Registrars3) hawakufika kazini na tarehe 24/6/2012 wafanyakazi 19(Intern doctors 15 na Registrars 4) hawakufika kazini.
Alisema, kuanzia tarehe 25/6/2012 hadi leo imethibitika kuwa Interns doctor 54 na Registrars 18 hawakufika kazini hadi leo tarehe 28/6/2012 ambapo tarehe 25/6/2012 bodi ya hospitali ilifanya kikao cha dharura kujadili hali ya utendaji kazi na utoaji huduma hospitalini na kutoa uamuzi.
Sigara, aliyataja maamuzi hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi akutane na madaktari ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika na kujadili namna ya kumaliza matatizo hayo jambo ambalo madaktari hao waligoma.
Alisema, baada ya madaktari hao kukaidi ombi hilo, Bodi ya hospitali ili waandikia barua za kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvunja mkataba walioingia na hospitali na pia kukiuka kanuni za kudumu za utumishi wa umma nalo walilikaidi

KAIMU MKUU WA MKOA WA MBEYA AMBAYE NI MWENYEKITI WA BODI HIYO,NORMAN SIGALA


WAANDISHI WALIOITWA WAKATI UAMUZI HUO UNATOKA



MGANGA MKUU WA HOSPITALI AKIFUATILIA UAMUZI ULIOTOLEWA KWA MAKINI



WAGONJWA WAKIWA HOSPITALI YA MBEYA-RUFAA


HAKUNA HUDUMA


"Iwapo madaktari ambao hawakuripoti au kueleza sababu za kuridhisha ifikapo tarehe 28/6/2012. Kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma, madaktari hao watasimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,"alisema.
Aidha, alisema kuwa kwa ujumala madaktari hao waligomea barua zote mbili yaani ya kuitwa kwenye kikao pamoja na ile ya kuwataka kujieleza hivyo Bodi imechukua hatua za kisheria za kuwafukuza kazi.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa bodi, alisema kuwa tayari hospitali ya Rufaa kwa ushirikiano wa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, madaktari watano wamepatikana ili kusaidia huduma kwa hospitali hiyo

RAY AZINDUA FILAMU YA SOBING SOUND KWA KUTOA MSAADA AKISHIRIKIANA NA STEPS...!!!

 Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entertainment ya jijini Dar es salaam leo kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre  kilichopo Kinondoni, Bi. Zainabu Bakari. Vyakula mbalimbali vimetolewa vyenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu katika kituo hicho kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage.
 Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entertainment ya jijini Dar es salaam leo kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre  kilichopo Kinondoni, Bi. Zainabu Bakari. Vyakula mbalimbali vimetolewa vyenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu katika kituo hicho kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage.
Msanii wa Filamu Nchini Vicent Kigosi 'Ray' katikati na Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps Ignatus Kambarage wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Ray kugawa vyakula mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre vilivyotolewa na Kampuni ya Steps wakati wa Uzinduzi wa filamu yao Mpya ya Sobing Sound.
---
MSANII wa filamu nchini  Vicent Kigosi 'Ray'  amezindua filam yake  mpya inayojulikana kama 'SOBING SOUND'.

Filamu hiyo imezinduliwa kwa staili tofauti ambapo badala ya kuzindua Ukumbini kama ilivyozoeleka na wengi, msanii huyo amezindua filamu hiyo katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 1.5  kwa niaba ya Kempuni ya Steps Entertainment ya jijini Dar es salaam

Akizungumza mara baada ya kuzindua filamu hiyo akiwa pamoja na watoto yatima wa kituo hicho, Ray alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba  watu wengi wamekuwa wakifurahia maisha huku wengine wakiendelea kutaabika kitendo ambacho si kizuri.

Alisema ujio wa filamu hiyo ni kama azma yake aliyoipanga tangu awali kuhakikisha filamu zake zote zinafanya vizuri na atahakikisha japo anatoa kidogo kwa namna yoyote ile kwa kuwakumbuka watoto yatima kwa kila filamu anayotoa.

Alisema msaada uliotolewa kwa watoto yatima hautaishia kwao bali ataendelea kutoa kile atakachokipata kupitia filamu hiyo kuwasaidia na wale wasiojiweza amesema kampuni ya  Steps Entertaiment imekuwa msaada mkubwa kwa wasanii kutambulika na kutushawishi tuwe tunawakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira magumu.


Nae mmoja wa wakilishi wa Kampuni ya Steps Ignatus Kambarage amesema swala la watoto yatima ni letu sote na wala halichagui kwa kuwa tunawajibu na angalau kidogo tunachokipata kupitia filamu zetu tunarudisha kwa kutoa shukrani zetu.
-- 
Rajabu Mhamila Super D

 ALICHOSEMA WAZIRI MKUU LEO BUNGENI KUHUSU KUJIUZULU NA MGOMO WA MADAKTARI.....

.
Leo ndio siku ambayo waziri mkuu Mizengo Pinda aliahidi kutoa jibu la serikali bungeni kuhusu itakachofanya kuhusu mgomo wa Madaktari.
Kuhusu kujiuzulu kutokana na mgomo wa sasa likiwa ni swali kutoka kwa mbunge Tundu Lisu wa Singida Mashariki amesema “yako mazingira unaweza ukawajibika kwa njia hiyo lakini sio lazima yakawa yoote na mimi sioni kama hili ni moja ya maeneo ambayo unaweza ukasema kistahiki hivi unaweza kufikia hatua hiyo, ninachokubali tu ni kwamba tatizo hili ni kweli ni la muda mrefu na nimefanya kila njia kujaribu kulitatua kwa kiasi kikubwa sana, inabidi tukubali kwamba bado lina changamoto nyingi kwa sababu ya mambo mengi tu ambayo yameingiliana na mgogoro wenyewe”
Freeman Mbowe kiongozi wa kambi ya Upinzani bungeni alisimama na kumuuliza Waziri Mkuu kwamba “ulitoa kauli ambayo kama mzazi au kama baba imetia hofu kubwa sana katika taifa pale ulipokua unazungumzia mgomo wa Madaktari na hatimae ukasema na LITAKALOKUWA NA LIWE, vilevile zilipatikana taarifa nyingine kwamba rais wa Madaktari ametekwa juzi usiku, ameteswa, kavunjwa meno, kango’lewa kucha.. unalieleza nini taifa kuhusu kauli yako ya LITAKALOKUA NA LIWE? na serikali inafanya nini cha ziada?
Hili ndio jibu alilotoa Waziri mkuu kwa Freeman Mbowe: “Kwanza nikiri kwamba ni kweli nilitamka hivyo jana lakini kilichokua kinanisumbua kichwani ni kwa sababu nilijua jambo hili liko mbele ya mahakama kuu, kuhusu yaliyompata Dr Ulimboka naonyesha masikitiko yangu juu ya jambo hili na ninamtakia kila la kheri na apone haraka”
Kuhusu alichoahidi kukiongea leo kuhusu Mgomo unaoendelea Waziri Mkuu amesema “tumezungumza na vyombo mbalimbali ili tuone katika mazingira tuliyonayo ni namna gani tutawahudumia wagonjwa, tumewaomba wenzetu wa LUGALO tutumie hospitali ile kuhakikisha wagonjwa hawakosi hiyo huduma, hata hospitali zake nyingine ndogo zote tumeamue tuzitumie kwa njia hiyo, lakini pia tumeona ni vizuri kama kutakua na madaktari wengine waliostaafu na wengine waliopo wizarani pale wote tumeomba sasa watafutiwe njia mbalimbali ili warudi waweze kutoa hiyo huduma kwa Watanzania”

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...