MADAKTARI WOTE 72 WAFUKUZWA KAZI MKOA WA MBEYA KWA KUKAIDI AMRI YA KURUDI KAZINI
***HABARI HII INALETWA KWENU EXLUSIVELY KWA HISANI YA WAANDISHI MAHIRI WA TONE RADIO-MBEYA*88
Katika kile kinachoonekana kuwa Serikali imeamua kudeal na hii ishu kiutu-uzima,wameanza kugawa kichapo kwa Madokta wabishi na kimeo kimeanzia kwenye mkoa ambao siku zote huwa unatoaga vitu critical, MBEYA
Baada ya Madokta kugoma na kuamriwa kurejea kazini ifikapo leo,wakagoma,jamaa wamefanya walichoahidi...WAMETIMUA WOTE
BODI ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewasimamisha kazi madaktari wote 72 kwa kosa la kutoingia kazini kwa siku tano jambo ambalo ni kinyume cha makubaliano ya mkataba.
Katika kile kinachoonekana kuwa Serikali imeamua kudeal na hii ishu kiutu-uzima,wameanza kugawa kichapo kwa Madokta wabishi na kimeo kimeanzia kwenye mkoa ambao siku zote huwa unatoaga vitu critical, MBEYA
Baada ya Madokta kugoma na kuamriwa kurejea kazini ifikapo leo,wakagoma,jamaa wamefanya walichoahidi...WAMETIMUA WOTE
BODI ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewasimamisha kazi madaktari wote 72 kwa kosa la kutoingia kazini kwa siku tano jambo ambalo ni kinyume cha makubaliano ya mkataba.
Imeelezwa
kuwa madaktari hao ambao 54 ni wale wa mafunzo ambao waliingia mkataba wa miaka
miwili na hospitali ya Rufaa na madaktari 18 ni wale walioajiriwa na Wizara ya
afya.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman
Sigara, alisema kitendo cha madaktari kutoripoti kazini kwa siku tano ni
ukiukwaji wa kanuni za utumisha wa umma toleo la 2009 kifungu namba F.16-F17 na
F. 27.
"Hivyo
kupitia kanuni hiyo madaktari hao wamesimamishwa kazi na kurudishwa
kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
kwa hatua zaidi za kinidhamu,"alisema Sigara.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Bodi, imeelezwa kuwa siku ya tarehe
23/6/2012 wafanyakazi 15 waliokuwa zamu(Intern Doctors 12 na
Registrars3) hawakufika kazini na tarehe 24/6/2012 wafanyakazi
19(Intern doctors 15 na Registrars 4) hawakufika kazini.
Alisema,
kuanzia tarehe 25/6/2012 hadi leo imethibitika kuwa Interns doctor 54
na Registrars 18 hawakufika kazini hadi leo tarehe 28/6/2012 ambapo
tarehe 25/6/2012 bodi ya hospitali ilifanya kikao cha dharura kujadili
hali ya utendaji kazi na utoaji huduma hospitalini na kutoa uamuzi.
Sigara,
aliyataja maamuzi hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi akutane na madaktari
ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika na kujadili
namna ya kumaliza matatizo hayo jambo ambalo madaktari hao waligoma.
Alisema,
baada ya madaktari hao kukaidi ombi hilo, Bodi ya hospitali ili
waandikia barua za kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu
kwa kuvunja mkataba walioingia na hospitali na pia kukiuka kanuni za
kudumu za utumishi wa umma nalo walilikaidi
WAANDISHI WALIOITWA WAKATI UAMUZI HUO UNATOKA
MGANGA MKUU WA HOSPITALI AKIFUATILIA UAMUZI ULIOTOLEWA KWA MAKINI
WAGONJWA WAKIWA HOSPITALI YA MBEYA-RUFAA
HAKUNA HUDUMA
Aidha, alisema kuwa kwa
ujumala madaktari hao waligomea barua zote mbili yaani ya kuitwa kwenye kikao
pamoja na ile ya kuwataka kujieleza hivyo Bodi imechukua hatua za kisheria za
kuwafukuza kazi.
Hata hivyo Mwenyekiti
huyo wa bodi, alisema kuwa tayari hospitali ya Rufaa kwa ushirikiano wa
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, madaktari watano wamepatikana ili kusaidia huduma
kwa hospitali hiyo
No comments:
Post a Comment