Italia kupambana na Uhispania katika fainali
Mario Balotelli alifunga magoli
mawili ya kupendeza mno na kuiwezesha timu yake ya Italia kuishangaza
Ujerumani kwa kuifunga magoli 2-1 katika nusu fainali ya Euro 2012, na
nafasi ya kucheza mechi ya fainali mjini Kiev dhidi ya Uhispania.
Mabao ya mshambulizi huyo wa klabu ya Manchester
City ya England, aliingiza goli la kwanza wavuni kupitia kichwa, na
pili kwa mkwaju wa kasi mno katika uwanja wa mjini Warsaw, na Italia
kuwathibitishia Wajerumani katika kipindi cha kwanza kwamba ilikuwa na
nia kamili ya kufika fainali.
Wajerumani,
kufuatia mshituko, walianza kucheza kwa makini zaidi, lakini bao lao la
penalti, ambalo lilipatikana katika dakika ya 92, kupitia Mesut Ozil,
lilichelewa mno, na halikuweza kuwaokoa.
Italia kamwe hawajawahi kushindwa na Ujerumani
katika mashindano makubwa, na wamefanikiwa sasa kucheza mechi nane dhidi
ya Ujerumani pasipo kushindwa.
Hii sasa itakuwa mara ya tatu kwa Italia kuingia
fainali za michuano hii ya mataifa ya Ulaya, na wataingia fainali kama
timu inayodhaniwa kuwa dhaifu ikilinganishwa na mabingwa watetezi
Uhispania.
Timu hii ya meneja Cesare Prandelli ilistahili
ushindi, kwani sio tu waliweza kupambana na Ujerumani ambayo iliwashinda
wapinzani wao kwa urahisi, bali pia walifunga mabao yao mapema katika
kipindi cha kwanza.
Timu hiyo ya Azzurri ilikuwa na nafasi
ya kujiongezea magoli, lakini ilicheza kwa tahadhari kwa kuhofia kwamba
iwapo ingeliongoza mashambulizi zaidi dhidi ya Italia, kulikuwa na
uwezekano wa ngome yao kuachwa ikiwa dhaifu, na Wajerumani
kuwashambulia.
No comments:
Post a Comment