Mtunzi: Godwill
Sanga
Makazi: Arusha,
Tanzania Contacts: 0657 35728
0756979566
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.21
Alikuwa ni Lulu ambaye alionekana kutokuwa na furaha yoyote ile na hii ilijidhihirisha wazi moja kwa moja toka usoni kwake hali iliyomfanya Sele kumkaribia na kumuuliza "kulikoni rafiki yangu?""niko sawa tu,kwani unaonaje,aliuliza Lulu."niambie ukweli kwani unaonyesha wazi kwamba hauko sawa, tafadhali niambie,Sele alisisitiza.Akiwa anajiweka sawa kwa kuelezea yote yanayo msibu alijikuta akitokwa na machozi mengi ,Sele alijaribu kumtuliza.Lulu aliongea kwa kwikwi "nawakumbu.......ka......wa.....za.....zi,alishindwa kuendelea kuzungumza huku kilio cha kwiki nacho kilimbana.Baada ya kutulia kidogo aliendelea"unajua Sele natamani sana kama wazazi wangu wangekuwepo katika mahafali haya,ningefurahi sana tena mno""usijali sahau hayo maana hiyo ni kazi ya Mungu na haina makosa ,acha basi kuwa mnyonge tusherekee vizuri,alisema Sele.Kwa shingo upande Lulu alikubali kuendelea na maandalizi ya mahafali yao.Muda wa mahafali uliwadia ,wageni nao walikuwa wamesha wasili,kwa bwembwe nyingi na shamra shamra sana wahitumu waliingia ndani ya ukumbi ulio pambwa vizuri na ukapambika haswa,punde si punde kelele zililindima ukumbini «««happy day,happy day»»»».Wazazi wa Selemani waliwasili ukumbini huku wakiwa wamekumbatia zawadi nyingi bila shaka zilikuwa kwa ajili ya mwanao , naye mjomba ake na Lulu sanjari na mkewe walikuwepo ukumbini.Burudani ziliendelea huku watu wakiserebuka na kula na kunywa.Wakati hayo yote yakiendelea Lulu alimwita Sele na kumnong'oneza kitu*********
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.20
Wanafunzi wa shule moja waliongoza katika mashindano yale ya debate na hawa si wengine bali ni Lulu na Seleman kutoka shule ya sekondari Jitegemee.Katika mashindano hayo Lulu na Seleman waliweza kuelezea vizuri sana namna ukosefu wa demokrasia katika nchi unavyoweza kuchangia kudidimiza maendeleo ya nchi.,kutokana na maelezo yao bora walizawadiwa computer moja kila mmoja.Jambo hilo lilikuwa la furaha sana kwao hivyo walipongezwa na wote waliohudhuria ile debate na wao pia walipongezana.Haya yote yaliendelea kuwatia moyo na kuwapa ari na hamasa kubwa ya kufanya vizuri zaidi katika masomo yao.Maisha yao ya shule yalikuwa ya kuigwa kwani kila mwanafunzi darasani mwao alipenda kwenda kuuliza maswali pamoja na kuomba ushauri wa kimasomo kwa Seleman na Lulu na hii ilikuwa kwasababu tu walikuwa na uwezo mzurri wa kimasomo.Hali haikuishia hapo waliendelea kupendwa na walimu wao kwani siku moja wakiwa darasani wanafunzi wenzao walipanga kumpiga mawe mwalimu wao wa kiingereza sambamba na kuchoma moto nyumba yake kisa alikuwa haingii darasani kufundisha na ifikapo mwisho wa muhula huingia na kutoa mtihani ,wakiwa katikati ya mazungumzo yao Lulu na Seleman walishauriana namna ya kutuliza jazba ile na hatimaye kutoa wazo la kumuita mwalimu husika na kumweleza shida yao na kumtaka awe anahudhuria vipindi.Uamuzi huo ulipokelewa na wanafunzi wote ambao walimwita mwalimu na kumweleza yote ,naye mwalimu alikiri akisema "nisameheni wanafunzi nitabadilika" na hii ilisababisha amani kutawala tena pale shuleni kwao.Miaka nayo ilizidi kwenda kadhalika pia siku nazo zilikuwa hazigandi Lulu na Seleman walimatiza kidato cha nne.Muda wa matokeo kutoka uliwadia ambapo shule ya sekondari Jitegemee ili faulisha wanafunzi wote kwa kiwango cha daraja la kwanza na la pili,kwa upande wao Lulu na Seleman walipata daraja la kwwanza yaani "division one" na ilikuwa ni bahati sana kwao kwani walichaguliwa kujiunga kidato cha tano katika shule moja.Maisha ya "high level" yalikwenda salama na hatimaye siku iliyokuwa ikingojewa iliwadia ambapo Lulu na Seleman walifika ukingoni mwa elimu yao ya sekondari yaani kidato cha sita.Siku ya mahafali yao iliwadia huku kila mmoja akiipokea kwa hamu kubwa na katika hali isiyotegemewa Selemani aliona kitu******
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.19
Mwili wa mama Lulu ulikuwa umekauka na hakukuwa na dalili yeyote ya yeye kupumua,akawataarifu wenzake na mara baada ya kumwangalia vizuri waligundua kwamba alikuwa amekwisha fariki dunia.Lulu alishuhudia kifo hicho cha mama yake kipenzi,Lulu alilia sana tena kwa uchungu na majonzi mengi kwani tayari alikuwa ameuanza ukurasa mpya wa kukosa mapenzi na malezi ya baba na mama yaani ukurasa wa uyatima,alikumbuka maisha aliyoishi na mama yake huku akibugujikwa na machozi tele.Taratibu za mazishi zilifanyika na ndugu wa Lulu waliwasili pale kimara na hatimaye mazishi yalifanyika katika makaburi ya kinondoni,mahali pale pale alipozikwa mzee John .Baada ya mazishi kumalizika wanandugu wa Lulu walikaa kikao na kuamua kwa pamoja kwamba mjomba ake na Lulu ndiye atakae mlea Lulu mpaka atakapofikisha umri wa kujitegemea.Wakati mama yake na Lulu anafariki dunia Lulu alikuwa akisubiri matokeo yake hasa mara baada ya kuhitimu darasa la saba.Hivyo Lulu alilazimika kuhamia Mbagala kwa mjomba ake,ambako alienda kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya jitegemee.Lulu alipokelewa vizuri katika familia ile ya mjombaake na maisha yalikuwa mazuri kwani alipewa mahitaji yote aliyoyahitaji.Alipendwa sana na shangazi yake na kila siku alimsisitizia kusoma kwa bidii.Lulu alionyesha kusikia na kushika vizuri yaleyote aliyoambiwa kwani kila mtihani alikuwa anakuwa wa kwanza darasani hali iliyompelekea kupendwa na kila mtu si wanafunzi wenzake tu bali hata walimu wake.Lulu aliendelea kujituma zaidi ili aweze kufaulu mitihani yake,pamoja na hayo yote alikutana na Seleman ambaye alikuwa classment wake katika shule ya sekondari jitegemee,walishirikiana vizuri sana katika masomo yao hivyo kuweka ushindani mkubwa sana katika nafasi ya kwanza na ya pili darasani mwao.Siku moja Lulu na Seleman walichaguliwa kwenda kuiwakilisha shule yao katika mashindano ya 'debate' ambapo shule zote za Tanzania zilihudhuria kupitia wawakilishi wao,ambapo katika mashindano hayo kulitokea kitu cha kushangaza********** Usikose Episode 20........
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.18
Karatasi ya majibu ilionyesha kwamba mzee John alikuwa anaugua kansa ya tumbo ambayo ni ngumu sana kwa yeye kupona.Taarifa hii ya daktari ili wasononesha sana na kuwastua sana akina Lulu na mama yake,ambao macho yao haya kusita kuonyesha hisia kwa kutoka machozi mithili ya mvua nyikani.Siku ile mkewe na mzee John pamoja na mwanae hawakuondoka pale hospitalini.Ilipofika majira ya saa moja usiku hali ya afya ya mzee John ilianza kutia matumaini walau kidogo kwani aliweza kuongea japo kwa shida shida,mzee John akamwita mkewe sanjari na mwanae Lulu kisha kuwaambia"mke wangu nakuomba jitahidi sana umsomeshe mwanetu mpendwa,tunza zile mali zetu,wakati haya yote yakiendelea mkewe na mzee John alikuwa amejiinamia pembeni ya mumewe huku akibugujikwa na machozi, mzee John aliendelea "nawe mwanangu Lulu kazana kusoma na ushike sana elimu na usimwache aendezake maana huo ndio ufunguo wako wa maisha" kisha kusema hayo aliomba apatiwe maji maana alijihisi kubanwa na kiu,mkewe aliinuka haraka haraka na kuchukua maji na kuanza kumnywesha,akiwa bado anaendelea kumnywesha maji akaona mzee John akishua pumzi kwa haraka na mara akaona maji aliyokuwa akimnywesha yakitoka mdomoni mithili ya udenda,akajiribu kumtikisa huku akiita "mzee John!!"mzee John!!!,hakuna sauti iliyotoa jibu,mkewe alianza kulia kwa sauti huku akimwita daktari aje kumpa msaada.Mara baada ya daktari kuchukua vipimo kwa mzee John aliwageukia mkewe na John na mwanae,"kwakweli mzee hatunaye tena" kauli hiyo ilipokelewa kwa vilio vikali.Mwili wa marehu ulifunikwa na kuchukuliwa mpaka mochwari ambako ulihifadhiwa kusubiri taratibu za mazishi.Tarattibu za mazishi zilifanyika na mwili wa marehemu ulipata nyumba ya milele katika makaburi ya kinondoni.Wakati mzee John anafariki dunia Lulu alikuwa na umri upatao miaka saba.Kifo cha mzee John kilimpa majonzi mengi na simanzi kubwa mama lulu hali iliyopelekea afya yake kudhoofu kutokana na msongo wa mawazo hali hiyo ilimpelekea kukosa nguvu na kumshawishi ajione mwenye mikosi na balaa tupu hapa duniani kisha kumlilia Mungu wake "kwanini mimi tu".Miaka ilizidi kusonga na hali ya mkewe na mzee John ilirejea katika hali yake ya kawaida hasa baada ya mawazo na kumbukumbu za kifo cha mumewe kuanza kupotea.Siku moja mkewe na mzee John alikuwa akitoka katika kazi yake ya kuuza mboga mboga za majani alijihisi kuumwa na kichwa lakini alifikiri kuwa hali hiyo ilisababishwa na jua kwani siku hiyo alishinda juani.Siku zilisogea hali ya mkewe na mzee John ilizidi kubadilika na kuwa mbaya,hali ya iliyomlazimu Lulu kumwendea jirani yao ,bwana Masele na kuomba msaada.Taarifa ziliwafikia pia majirani wengine ambao walimchukua na kumpeleka hospitali.walipokuwa njiani mmoja wa majirani aligungua kitu****
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.17
Je nini kitatokea??? usikose kufuatilia episode 18.......
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.16
Daktari aliitwa haraka na kwenda,alipofika alimkuta mkewe na kamanda akikata roho,akamfunika shuka kisha kuwaambia wale askari waliokuwa karibu kisha akatoka kwenda kuandaa cheti cha kifo,baada ya kumaliza askari waliutwaa mwili wa marehemu na kwenda kuuzika.Miaka mitano ilikuwa imepitaa ambapo Lulu alikuwa mkubwa kidogo,siku moja jioni mkewe na mzee John alimwita mwanae na kumuuliza"mwanangu ungependa kuja kuwa nani ukiwa mkubwa?","kuwa mwanasheria "Lulu aliendelea kwani ninapenda sana kuja kuwa mtetezi wa kinamama na watoto kwani mwalimu alitufundisha kuwa katika jamii zetu watoto na wanawake ndio watu wanaoonewa sana."sasa kazana sana na masomo".Maneno hayo yalimfurahisha sana mkewe na mzee John kwa furaha alimkumbatia mwanae.Maisha yaliendelea kwa amani na furaha lakini kwa upande mwingine maisha ya pale kimara yakizidi kuwa magumu,hali iliyomfanya mzee John awe anachelewa kurudi nyumbani sababu ya kusubili wateja katika toyo yake.Jioni ilipofika mzee John alimwita mkewe na mwanae na kuwaambia kuna jambo anataka wazungumze******
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.15
:Hazikupita dakika tano hakimu akasema"kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizo wekwa mtuhumiwa anahukumiwa kifungo cha maisha na kazi ngumu" kisha kumaliza halpo askari liita "court!!!!"""" watu wakasimama hakimu akatoka nje .Mkewe na kamanda alitokwa na chozi mara baada ya hukumu hasa pale alipokumbuka kwamba maisha aliyokuwa akiishi yalisababishwa na mumewe kamanda ambaye kamwe hakuwa chaguo lake la moyoni kwani wazazi wake ndio waliomlazimisha kuolewa nae hasa kutokana na tamaa ya pesa.Alikuwa ameshindwa kutoroka hasa kwa sababu alitishwa kuuwawa endapo angejaribu kutoroka,aliwaza pia ni namna gani ataenda kuishi gerezani kwani hali ya maisha hayo alikuwa akiiona kwenye television.Polisi wakamchukua na kumuingiza garini tayari kuelekea gerezani kutumikia adhabu yake.Njiani mkewe kamanda alionena kuweka kichwa dirishani ili awezekuiona dunia kwa mara ya mwisho.Ni miaka miwili sasa tangu mkewe na kamanda aanze kutumikia adhabu yake,umbo lake lilionekana kupungua na kuzoofu pia alikuwa mtu mwenye msongo wa mawazo.Mfungwa mmoja aliyekuwa rafiki yake alijaribu kumshauri kwamba ayakubali tu maisha hayo kwani ndio yaliyobaki na kuachana na mawazo,lakini ushauri huo ulikuwa kama upepo haya kupata hata chembe ya nafasi katika kichwa cha mkewe na kamanda chazaidi ni kwamba aliiendelea kujitenga na wenzake.Mwaka mmoja baadae hali ya mkewe na kamanda ilizidi kuwa mbaya kwani sasa ikuwa hali tena chakula hivyo mkuu wa gereza akaagiza apelekwe hospitali.Alichukuliwa haraka haraka mpaka hospitali na mara baada ya kuwasili walipokelewa na daktari kisha mgonjwa kulazwa chini ya uangalizi mkali wa askari na ilipofika mjira ya saa nane usiku hali ya mgonjwa ili badilika *****
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.14
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.13
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.12
JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.11
Ule mlio uliwashitua lakini
wakaamua kuendelea ila kwa tahadhari kubwa.Waliendelea kupanda ngazi
mpaka walipo fika ghorofa ya juu,walipofika huko walikuta kibalaza cha
kupumzikia ambapo ukiwa pale unaweza kuona mji wote.Mkewe na kamanda
alitoo burungutu la manoti ya elfu kumi na elfu tano kisha kumkabizi
mzee John na kumwambia "hizo zitakusaidia nauli ukifika chini chukua
taxi itakayo kupeleka mpaka bahari huko utaingia boti litakalokupeleka
mpaka dar es salaam sawa!!?"sawa asante "alijibu mzee John na kulitia
burungutu lile mfukoni.Kwa mara nyingine tena mkewe na kamanda alitoa
kamba ndefu kisha akaifunga vizuri kwenye nguzo iliyokuwa karibu na
kumwambia mzee John kwamba atatumia kamba hiyo kushuka mpaka chini.Basi
mzee John alipanda kamba haraka haraka na kuanza kushuka kufuata ile
kamba taratibu,ilimchukua dakika kama kumi kufika chini,baada ya kufika
chini mzee John alinyanyua mkono juu na kumuaga mkewe na kamanda.Mkewe
na kamanda aliivuta ile kamba harakaharaka na kurudi chumbani kwake
ambapo alimkuta kamanda akiwa bado anakoroma.Huku nako mzee John
alisimamisha taxi ambayo ili mchukua mpaka bahari.Mzee John alimpa ujira
yule mwenye taxi.kisha kufika bahari alitafuta boti ya kwenda Dar es
salaam kwa muda kidogo hatimaye akaipata na kuingia tayari kuelekeaDar
es saalam.Safari ilichukua karibu saa moja na nusu ambapo waliwalisili
Dar es saalam majira ya saa kumi na mbili asubuhi.Mzee John alishuka
haraka na kutafuta daladala ya kuelekea kimara.Kwenye lile jumba kamanda
aliagiza kwa walinzi wake mzee John alletwe mbele yake na kisha kupigwa
risasi na alisema akiwatoroka tu cha moto watakiona.Basi walewalinzi
walienda mara chumbani kwa mzee John na kufungua mlango
ghafla,wakaangaza huko na huko na kupekua kona zote hawa kumwona mtu
wakarudi na kumuarifu kamanda******** JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.10
Kwanza nataka nikufahamishe
kwamba sisi tulikuokoa wewe kule baharini ulipokuwa ukikaribia kuzama na
tukaamua kukuleta huku kambini maana kuna kazi muhimu tunayotaka wewe
ufanye na ukikataa tu mwisho wa maisha yako utakuwa umefika.Sisi
tunajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya ,hivyo sisi tutakupa wewe
chochote kile utakacho na utakipata ila sisi tunataka wewe kujaza
madawa ya kulevya katika pakiti hafu zitapelekwa kwenye mashine tayari
kwa kufungwa hatimaye kusafirishwa,haya tuambie basi uko tayari au
la?.Mzee John aliinamisha kichwa chini huku akitafakari nimaamuzi gani
ayachukue,picha ya mkewe pamoja na mwanae Lulu zilimjia na kumuhimiza
kurudi nyumbani kuwasaidia maana wanateseka,Mzee John aliipima kazi
aliyokuwa akienda kuifanya akakumbuka jinsi alivyo wahi kujiapiza kwamba
hata kaa kujihusisha na madawa ya kulevya lakini upande mwingine bado
alihitaji kuiona familia yake.Baada ya tafakuri ya muda wa takribani
dakika tano,Mzee John alijibu"niko tayari",boss alicheka"ha...ha....ha"
safi sana nenda kapumzike tutaanza kazi. Baada ya miaka mitatu kupita
pasipo kumwona mumewe mkewe na mzee John alikata tamaa na kuamini kwamba
huenda mumewe alikwisha fariki dunia.Mzee John aliendelea na kazi yake
ya kujaza madawa kwenye pakiti ambapo ilimlazimu kujaza pakiti mia tatu
kwa siku ambapo alitakiwa kuanza saa kumi na mbili asubuhi mpaka
jioni,kwa muda wote aliokuwa kwenye lile jumba hakuwahi kutoka nje hivyo
hakujua ni wapi alipo.Siku moja akiwa anaendelea na kazi aliona mlango
ukifunguliwa na dada mmoja mweusi wastani mrefu kidogo aliingia ndani
kisha kumsalimu mzee John"shikamoo mzee""marahaba""nikusaidiaje?" nataka
kukuuliza jitu sijui ukotayari "ulizatu''asante yule dada
aliendelea,mimi ni mke wa kamanda kiongozi wa hili kundi ningependa
kujua ulifikaje huku maana si eneo zuri hafu nimekuwa nikikuonea huruma
sana.Mzee John alieleza kila kitu mpaka yeye kufika pale lakini
aliendelea "natamani sana kurudi kuiona familia yangu kwani nilimwacha
mke wangu na mtoto mdogo hana hata mwaka hafu sijui wako hai au
la,machozi yalimtoka mzee John kisha aliendelea nimeambiwa sitatoka humu
ndani hafu sijui niko wapi mimi" pole usilie mzee,alijibu mkewe na
kamanda,ki ukweli toka uingie humu mume wangu"kamanda" amekuwa
akizungumzia juu ya kukuua kwani anaogopa kwamba utatoa siri kwa kweli
kesho ndio siku ya kifo chako ila mimi nataka nikusaidie.Nitashukuru
sana alijibu mzee.Sasa kesho saa nane usiku nitakugongea mlango ili
kukutorosha.Baada ya maongezi hayo waliachana.Usiku ulipoingia Mzee John
hakulala hamu ya kuiona familia yake ilizidi ,ilipotimu saa nane mlango
uligongwa,mzee John alifungua haraka na kumwona mkewe na kamanda akiwa
amevalia mavazi ya kijeshi,akamwambia nifuate.Safari ya kutoka nje ya
jumba ilianza walipandisha ngaz kwa haraka na tahadhari,lakini ghafla
wakasikia mlio mkubwa '"paa!!!!!! ********
JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.9.
JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.8
Mzee John alikaakimya huku kengele ya hatari ikiendelea kulia kichwani
mwake lakini kwa upande mwingine nafsi ilimwambia avute subira kidogo
ili aone nini kitafuatia.Safari iliendelea kimyakimya na hatimaye
wakafika nchi kavu na baada ya kufika hapo mzee John aliamuriwa kushuka
botini haraka sana naye alifanya hivyo bila kuleta ubishi wa aina
yoyote.Mara tu baada ya mzee John kushuka kiongozi wakundi
aliyejulikana kama kamanda aliamuru "MFUNGENI KITAMBAA USONI" Kitambaa
kilifungwa haraka haraka .Baadae kidogo mlio wa gari lililokuwa kasi
ulisikika ukikaribia eneo walilokuwepo akina mzee John.Hatimaye gari
lilifika eneo walilokuwapo akina mzee John , mzee John alichukuliwa
mkukumkuku kisha kutupwa ndani ya gari na kwa kasi gari
liliondoshwa.Njiani mzee John alitamani kuuliza ni wapi walikokuwa
wanakwenda na kwanini wamemfunga kiasi kile ila yote hayo hayakuwezekana
kwani tayari alikuwa amekwisha fungwa kitambaa mdomo hali iliyomfanya
kushindwa kutoa sauti.Moyoni mwake aliwaza "hawa watakuwa ni majangili
basi hapa lazima nitauawa lakini yote na mwachia Mungu".Gari lilisimama
ghafla honi kali ilipigwa "piiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii kisha geti
lilisikika likifunguliwa gari lilisimama milango ilifunguliwa,mzee John
alichukuliwa mpaka kwenye chumba kimoja kisha kuwekwa humo.Alifunguliwa
vitambaa vyote .Kabla mzee John hajaongea lolote mlango wa chumba
walimokuwamo ulifunguliwa na kufungwa haraka ambapo aliingia dada mmoja
na kuweka chakula mbele ya mzee John kisha amri ilitolewa"MALIZA CHAKULA
CHOTE HARAKA" kisha amri hiyo kutolewa mlango ulifunguliwa na wote
wakatoka kumwacha mzee John akila chakula.Huyu kamanda ambaye ndio
kiongozi wa kundi ambalo linajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya
nje na ndani ya nchi.Ilimchukua muda kidogo mzee John kuamua kula kile
chakula kwani kuna wakati alihisi labda kinaweza kuwa na sumu lakini
tena upande mwingine njaa ilikuwa inamuuma sana,akakatashauri kukila
kile chakula na alifanya hivyo ila mara baada ya kula kile chakula mzee
John alijikuta akiishiwa nguvu na mwili kulegea akataka kupiga kelele
kuomba msaada ********JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.7
- JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.6.
- ile wimbi liliibetua ile boti kisha kuipindua kabisa basi mzee John na wenzake wakakupwAhuko na kuiacha boti ikielea peke yake.Basi mzee John na wenzake walijitahidi kilammoja kupiga mbizi ili kuikaribia ile boti,kutokana na upepo mkali ile boti ilizidi kwenda karibu na kilindini.Mzee John aliizama na kuibuka huku akijaribu kwenda kwa kasi sana ili awezekulifikia botti,alifanya kuhudi sana na kufanikiwa kulikuta boti ambalo sasa lilikuwa umbali wa mita kama sabini hivi toka pale lilipopindukia basi pasi kukawia mzee John alilikwea lile boti kisha kuliwasha.kila alipojaribu kuliwasha lilikataa kuwaka alijaribu kwa mara ya mwisho huku akirushwa rushwa na mawimbi ya baharini,wale wenzake nao wakaifikia boti mara baada ya kupiga mbizi vya kutosha.walipofika tu wakakutana na taarifa kutoka 8 mara ikawaka wote wakashangila y....e...ssssssss.Safari ya kurudi inchi kavu ilianza tena sasa wakikatika mwendo wa tahadhari,wakiwa bado safarini na huku mvua kubwa ikinyesha mara wakaona samaki mkubwa akijichomoza mbele ya boti yao kisha kuzama.Hilo halikuwatisha sana akina mzee John kwani ni kitu cha kawaida katika bahari ya hindi .Basi waliendelea na safari yao,wakiwa theluthi moja ya safari alitoke samaki mkubwa akaipindua ile boti na kuwatupa mbali akina mzee John na ilikuwa saa kumi na moja kasorobo.kila mmoja alijitahidi kupiga mbizi ili kunusuru maisha yake.Lile boti nalo likazama na huo ndo ukawa mwisho wa boti.Mzee John aliendelea kupiga mbizi huku akijaribu kuangaza huku na huko akijaribu kuomba msaada,Mzee John alianza kuishiwa nguvu huku njaa kali ikiwa imembana,aliendelea kupiga mbizi.Huku nyuma mkewe na mzee John alianza kuingiwa na hofu mara baada ya kuona kwamba mumewe harudi kwani haikuwa mazoea yake kuchelewa kurudi kiasi kile akaamua kuendelea kusubiri zaidi.Ilipofika majira ya saa mbili asubuhi mzee John akiwa hoi bin taabani alikatatamaa na kuamua kusubiri kifo huku hisia kali za kumbukumbu ya mwanae Lulu pamoja na mkewe kumjia kwa machungu yote akawa anaona sasa kwamba mwanzo wa maisha magumu kwa mwanae na mkewe umewadia.Akiwa katika dimbwi zito la mawazo Mzee John akasikia sauti kwa mbali alipo nyanyua kichwa aliona boti ikiwa inaelekea upande wake***********je NINI KITAENDELEA? USIKOSE EPISODE 7!!!!
mnaonaje hadithi hii.
ReplyDeletezipo mzuka ila jitahidi ku update coz episode zinachelewa sana
ReplyDeletestory inauzwa bei poa nicheki 0756979566
ReplyDeleteNimeipenda Sana
ReplyDelete