Dk. Ulimboka: Nakumbuka kila kitu
NI juu ya kilichompata alipotekwa na watu wasiojulikana, muda mfupi
baada ya kuokotwa akiwa taabani, mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari
nchini, Dk. Steven Ulimboka amefunguka kuwa alinusa kifo.
Akisimulia tukio hilo, Dk. Ulimboka alisema kuwa alipigiwa simu na
mtu aliyejitambulusha kwake kuwa anaitwa Hemed, aliyemwambia kuwa
anahitaji kuongea naye, ndipo walipopanga kuonana kwenye Viwanja vya
Leaders Kinondoni, Dar.
Dk. Ulimboka aliyekuwa akizungumza kwa tabu, alisimulia kuwa wakati
akiongea na mtu huyo anayekiri kuwa alikuwa wakifahamiana naye kabla,
alikuwa na wasiwasi kwani kila mara mtu huyo alikuwa akipokea simu na
kuwasiliana na watu wengine ambao hawakuwapo eneo hilo.
Dk. Ulimboka alisema kuwa baada ya muda alishangaa kuona wanaongezeka
watu wengine watano wakiwa na silaha, kisha wakamwambia kuwa
anahitajika kituo cha polisi na kumvuta na kumuangusha barabarani kabla
ya kumuingiza katika gari lenye rangi nyeusi na kuondoka naye.
Dk. Ulimboka alisema kuwa, wakiwa njiani walimpiga na kumfikisha
katika Msitu wa Pande na kuendelea kumpiga mpaka alipopoteza fahamu.
Ilielezwa kuwa jamaa hao walimwacha na kuondoka wakiwa na uhakika
kuwa amekufa kumbe alikuwa amepoteza fahamu tu hadi alipookotwa asubuhi.
No comments:
Post a Comment