Bima ya afya kwa raia Marekani
Mahakama kuu ya Marekani
imeruhusu kisheria moja wapo ya mapendekezo ya Rais Obama kuhusu
kuufanyia mageuzi muswada wake wa afya ambao unakabiliwa na
changamotokwa misingi ya kikatiba
Mahakama hio imekataa madai kwamba muswaada huo
umevuka-mpaka kwa sababu ya kikwazi cha kuwataka wamarekani wote wanunue
bima ya afya.Mahakimu wanne kati ya mahakimu tisa wa mahakama ya juu walipinga pendekezo hilo.
Inaarifiwa kuwa mahakimu hao ni wahafidhina.
Muandishi wa BBC aliye mjini Washington amesema uamuzi huo wa mahakama kuu ni ushindi mkubwa sana kwa rais Obama.
No comments:
Post a Comment