Sunday, April 28, 2013

DENT WA CHUO ALIVYOUWAWA!

MWANAFUNZI wa mwaka wa pili katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kilichopo Njiro jijini hapa, Henry Koga, ameuawa kikatili na hivi ndivyo
Kwa mujibu wa wanachuo wenzake ambao hawakutaka majina yao kuandikwa gazetini, Koga aliuawa kinyama kwa kuchomwa kisu shingoni na kundi la watu wasiofahamika wakati akitoka kujisomea nje ya chuo usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita.

Imeelezwa kuwa tukio la kuuawa kwa mwanafunzi huyo lilitokea saa 4 usiku ambapo marehemu huyo akiwa na wenzake walivamiwa na kundi la wahuni wapatao wanne katika eneo la CDA, jirani na chuo hicho na Koga kuchomwa kisu shingoni na kifuani.

Wanachuo wenzake walisema marehemu hakuwa anatoka kwenye starehe kama watu wengine wanavyodai bali alikuwa na wenzake wakitoka kujisomea nje kidogo ya chuo hicho kwa ajili ya kujiandaa na mitihani na walipofika eneo hilo, wakavamiwa na watu wasiojulikana. Baada ya tukio hilo, baadhi ya wanafunzi walijikusanya asubuhi yake na kuanza kuandamana kushinikiza uongozi wa chuo hicho kutoa tamko juu ya vitendo vya uhalifu vinavyojirudia mara kwa mara chuoni hapo. Kufuatia tukio hilo, wanachuo hao walifanya vurugu kubwa na kumlazimisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo kwenda chuoni hapo, alipofika kulitokea hali ya kutoelewana ambapo walimzomea na kumpiga mawe, hali iliyosababisha polisi kuingilia kati na kuwafyatulia mabomu ya machozi. Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema naye alijitahidi kuwatuliza bila mafanikio huku ikidaiwa yeye ndiyo chanzo cha vurugu hivyo kutakiwa kukamatwa. Mkuu wa mkoa alilazimika kuondoka eneo kuokoa maisha yake. Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Ibrahimu Kilongo akizungumzia tukio hilo, alisema wanachuo 10 wanashikiliwa na polisi kutokana na vurugu hizo na kwamba uchunguzi unaendelea.

GODBLESS LEMA ATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI

Jeshi la polisi mkoani hapa limemtia mbaroni mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mhe Godless Lema kwa tuhuma za uchochezi kwa wanafunzi kwenye chuo cha uhasibu mwanzoni mwa wiki katika vurugu zilizotokea chuoni hapo baada ya mwenzao kuuwawa juzi usiku huko maeneo ya njiro jijini hapa

Kamanda wa polisi mkoani hapa kamishna msaidizi wa polisi Liberatus Sabas alisema kuwa Mhe Lema alikamatwa huko nyumbani kwake Njiro majira ya saa 9 usiku.

Afande Sabas alisema jeshi hilo linaendelea na mahojiano na mtuhumiwa na kuwa katika tukio hilo zaidi ya watuhumiwa 14 walifikishwa mahakamani jana na kuwa hao hawezi kuwaongelea kwani kesi yao ipo kwenye chombo hicho cha sheria.

Pia kamanda Sabas alisema kuwa Mh Lema anashikiliwa kutokana na vurugu zilizotokea juzi kwenye chuo cha uhasibu na kuwa atafikishwa mahakamani siku ya jumatatu.

Kwa upande mwengine Kamanda Sabas alisema kuwa zaidi ya hao watu 14 na Mhe. Lema hakuna mtuhumiwa mwingine aliyakamatwa. Awali ilisemakana wakili wake Albert Msando nae amekamatwa.

Mnamo siku ya Jumatatu mwanafunzi mmoja aliuwawa kwenye mitaa ya Njiro jijini Arusha na watu wasiojulikana hali iliyoleta tafrani hadi wanafunzi hao walipoleta vurugu chuoni hapo na polisi kutumia mabomo ya machozi kuwatawanya.

Sekeseke hilo lilimalizwa na jeshi la polisi baada ya wanafunzi kutotii amri ya mkuu wa mkoa huo Magessa Mulongo na kuanza kuingia barabarani kuandamana.

ISHA MASHAUZI ASWEKWA NDANI KWA UTAPELI

MWIMBAJI ambaye pia ni bosi wa Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhan Makongo

alikumbwa na masaibu mazito kufuatia kudakwa na polisi wa Kituo cha Msimbazi, Dar akituhumiwa kukwapua mkoba wenye kitita cha shilingi laki saba, elfu hamsini na nane na mia mbili (758,200) mali ya Veronica Tarik.

ANASEPA: Mashauzi akiwakimbia Waandishi wa Global kuelekea kwenye Gari baada ya kutolewa dhamana

Chanzo cha habari kituoni hapo kilidai kuwa Jumanne iliyopita, Isha Mashauzi na shosti wake aliyejulikana kwa jina la Halima Shaban waliingia duka moja Mtaa wa Mafia na Jangwani, Kariakoo, Dar kwa lengo la kufanya ‘shopping’ lakini walipochomoka, Veronica alishangaa kutouona mkoba wake.

ISHA AKIMBIZWA Veronica aliwakimbiza wawili hao na kuwadaka mtaa wa pili na kuwasomea tuhuma zao kisha akawaomba awasachi kwenye mafurushi waliyobeba lakini Isha na mshirika wake waligoma, hali iliyosababisha kuzuka kwa timbwili wakidai mwanamke huyo alitaka kuwadhalilisha.

Baada ya Veronica aliyekuwa na wapambe ‘legelege’ kuzidiwa nguvu, waligeuka na kukimbilia Kituo cha Polisi Msimbazi ambako alifungua kesi ya wizi kwa Isha na shosti wake kwa jalada namba MS/RB/4023/2013.

MSAKO MTAA KWA MTAA WAANZA Maafande wenye difenda waliingia mitaani kuwasaka watuhumiwa hao mtaa hadi mtaa wakitumia mbinu mpya za kikachero na kufanikiwa kuwatia mbaroni Jumatano iliyopita. Isha akiwa selo, wapambe wake walimiminika kituoni hapo akiwemo Mtangazaji wa Kituo cha Redio Times FM cha jijini Dar, Hadija Shaibu ‘Dida’ kwa ajili ya kuhangaikia kuwachomoa wawili hao.

WAPAMBE WAMCHOMOA Saa 5:14 usiku, wapambe hao walifanikiwa kuwawekea dhamana lakini kasheshe nzito ilikuwa wakati wa kutoka rumande kwani wapambe wa Isha waligundua kuwa mapaparazi walikuwa wamekizingira kituo hicho na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kunasa picha zao. Isha alijaribu kujibanza ndani ya selo lakini wapambe walimpelekea taarifa kuwa mapaparazi nje walikuwa wakijipanga kukesha kituoni hapo mpaka siku itakayofuata. Baada ya kupata ujumbe huo, Isha alichomoka mahabusu kwa kasi ya mnyama swala na kukimbilia kwenye gari aliloandaliwa kumchukua huku wapambe wake wakiwa wamezikamata kamera za mapaparazi eti ili wasimpige picha.

MSIKIE ISHA MASHAUZI Kesho yake Alhamisi, paparazi alizungumza na Isha kwa njia ya simu ili aweze kuweka bayana juu ya sakata hilo lakini mwimbaji huyo alimjibu mbofumbofu. “Wewe andika unachotaka si ulikuwepo kituoni na umenipiga picha, sasa unataka nini? Yaani hata wewe unanifanyia hivyo duh! Leo nimeamini mapaparazi hawana undugu,” alisema Isha na kukata simu.

MAPYA YAIBUKA

MAPYA yameibuka kufuatia utata wa kifo cha Mwalimu Elizabeth Mmbaga (22) kilichotokea kwa madai ya kunyongwa usiku wa kuamkia Jumatatu, Aprili 15, mwaka huu nyumbani kwake, Kimara -Baruti, Kinondoni, jijini Dar.

Hapa ndipo ulipo kutwa mwili wa marehemu Elizabeth

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini mambo mapya kiasi cha kukifanya kifo hicho kihusishwe na mauaji ya kikatili yanayodaiwa kufanywa na mpenzi wake ambaye ni Mtanzania mwenye asili ya Kiasia aliyejulikana kwa jina la Srinivas, mkazi wa Mikocheni, Dar.

Ndugu wakifungua chumba cha marehemu

Timu ya wachunguzi wetu ilimtafuta mjomba wa marehemu anayeishi Mabibo, Dar ambaye inadaiwa ndiye aliyekuwa akiwasuluhisha Eliza na mpenzi wake na kumuuliza kuhusu kifo hicho na mambo mapya yaliyopo.

Mmoja wa ndugu wa marehemu akimtambua muuaji kwenya picha

“Nakumbuka wiki moja kabla ya mauaji, Elizabeth alinieleza kwa njia ya simu kuwa alipata taarifa toka kwa rafiki yake ambaye ni jirani yake akimwambia kwamba jamaa yake huyo yupo katika baa iliyopo jirani na nyumba aliyokuwa akiishi. “Ilinibidi nikutane na Eliza, tukafuatana naye hadi kwake kwa vile yule Mhindi alikuwa akimtishia kila mara kwamba atamuua kutokana na mgogoro wao wa kimapenzi.

Enzi za uhai wa marehemu

“Tulipokaribia yule Mhindi akawa anaondoka nyumbani hapo akifuatana na vijana wawili ambao hatujawahi kuwaona. Waliingia kwenye Bajaj, mimi niliwapigia winja, wakasimama, kijana mmoja alishuka na kunifuata. “Nilimwomba na yule Mhindi ashuke. Nikajitambulisha kwake mimi ni mjomba wa Eliza na kwamba nimepata taarifa anataka kumfanyia fujo Eliza, nikamuuliza kuna tatizo gani? “Alinijibu hawezi kufanya fujo. Hata hivyo, haikuchukua muda wakaanza kuzozana mbele yangu huku Mhindi akimuuliza ni kwa nini anampigia simu hapokei! “Ilibidi nimwombe Eliza aondoke mimi niongee na yule Mhindi ingawa Eliza hakuondoka. Nilimuuliza ana muda gani tangu aanze kufahamiana na Eliza, alijibu ni miezi saba. “Nilimuuliza kama hawajawahi kukorofishana hata siku moja? Alinijibu wamekuwa wakikorofishana mara kwa mara, nikamshauri aachane naye, akasema anampenda sana hawezi kumwacha. “Eliza aliingilia kati na kumwambia Mhindi kuwa yeye hampendi, Mhindi akasema yaishe naondoka lakini utaona. “Wakati huo ilikuwa kama saa tano usiku. Mhindi aliingia kwenye Bajaj na kuondoka na wale vijana wawili. Nilimwambia Eliza asilale kwake, alifanya hivyo ambapo alikwenda kwa mama’ke mdogo, Tabata -Barakuda. “Siku ya tukio, saa kumi jioni mama’ke alinipigia simu akinitaka tukutane kwa Eliza. Tulipofika tulikuta walimu wenzake wakilia, tuliwauliza wanacholilia hawakutujibu. “Mimi niliamua kuingia ndani kwa Eliza na kumkuta amelala, nilipomwangalia niligundua amefariki dunia. Alikuwa akitokwa damu mdomoni na puani. Ulimi ulikuwa nje huku akiwa na alama kama za kucha shingoni, nahisi alinyongwa kwa mkono. “Nilikwenda Kituo Kidogo cha Polisi Rombo na kutoa taarifa, nikafuatana na polisi wawili mpaka kwenye eneo la tukio. “Inauma sana! Hakuna kitu chake chochote kilichochukuliwa, hakika Eliza angetoa taarifa mapema polisi kama alivyoshauriwa kufuatia vitisho vya yule jamaa asingeuawa,” alisema mjomba mtu huyo. Mama mdogo wa marehemu, Anna Domisian naye alikuwa na haya ya kusema: “Siku hiyo ya Jumatatu, saa tisa alasiri nilipigiwa simu na mwalimu mmoja akinitaka nifike Kimara kwa Eliza, hawakuniambia kilichotokea. Nilipofika nikakuta mwili wa Eliza ukiwa juu ya kitanda. Nilipatwa na mshtuko mkubwa kwani Jumapili jioni aliniaga anarudi kwake. “Siku za nyuma aliwahi kunieleza juu ya fujo anazofanyiwa na mpenzi wake wa Kihindi na ndiyo maana nilimweleza mjomba wake aende akawasikilize.”

JK ATUNUKU NISHANI KATIKA SHEREHE ZA MUUNGANO


Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete (katikati, mbeke) akiwa katika picha ya pamoja na askari 30 aliowatunuku nishani mbalimbali, ikiwa ni moja ya shamrashamra ya kuadhimiasha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Ikulu, Dar es Salaam

Friday, April 26, 2013

TAB: Kim Kardashian Abandoned By Kanye West, Set to “Raise The Baby Alone”


Kim Kardashian is
“miserable,” declares Star ,
continuing in the pathetic
tabloid trend of trying to stir drama in the reality
star’s pregnancy.
The mag claims Kardashian is “distraught” over
her “ailing relationship” with Kanye West , quoting
a supposed “insider” as saying, “Kanye has been
nearly absent from Kim’s life since she got
pregnant.”
The “source” reveals, “He barely talks to her,
claiming he’s too busy recording in Paris.”
Star ’s so-called “insider” goes on to allege,
“Kanye refuses to record in the United States
because he claims he’s more ‘on point’ in Paris,”
adding, “He told Kim that his mind is so tangled
with baby thoughts and fears that it’s messing
with his creativity.”
“Baby thoughts and fears”? How incredibly vague.
Also, West made the decision to record in Paris
before he even got together with Kardashian, so
the claim that he went there to clear his head is
totally bogus.
Anyway, the tab’s mole says the Marriage
Counselor actress is “scared she’ll be left to raise
the baby alone — or, worse, that she’ll be back in
court, battling him for custody.”
Oh, please.
While Kardashian and West’s situation is of
course not ideal, the pair is making their
relationship work despite the distance.
The “Otis” rapper just spent this week in New
York with Kardashian, and he’s flown to L.A. to
be present for many of her doctor’s
appointments.
In any case, Gossip Cop once again checked in
with a Kardashian family insider, who tells us the
mag’s story is “tabloid nonsense.”

TAB: Kim Kardashian Abandoned By Kanye West, Set to “Raise The Baby Alone”


Kim Kardashian is
“miserable,” declares Star ,
continuing in the pathetic
tabloid trend of trying to stir drama in the reality
star’s pregnancy.
The mag claims Kardashian is “distraught” over
her “ailing relationship” with Kanye West , quoting
a supposed “insider” as saying, “Kanye has been
nearly absent from Kim’s life since she got
pregnant.”
The “source” reveals, “He barely talks to her,
claiming he’s too busy recording in Paris.”
Star ’s so-called “insider” goes on to allege,
“Kanye refuses to record in the United States
because he claims he’s more ‘on point’ in Paris,”
adding, “He told Kim that his mind is so tangled
with baby thoughts and fears that it’s messing
with his creativity.”
“Baby thoughts and fears”? How incredibly vague.
Also, West made the decision to record in Paris
before he even got together with Kardashian, so
the claim that he went there to clear his head is
totally bogus.
Anyway, the tab’s mole says the Marriage
Counselor actress is “scared she’ll be left to raise
the baby alone — or, worse, that she’ll be back in
court, battling him for custody.”
Oh, please.
While Kardashian and West’s situation is of
course not ideal, the pair is making their
relationship work despite the distance.
The “Otis” rapper just spent this week in New
York with Kardashian, and he’s flown to L.A. to
be present for many of her doctor’s
appointments.
In any case, Gossip Cop once again checked in
with a Kardashian family insider, who tells us the
mag’s story is “tabloid nonsense.”

Kim Kardashian and Kanye West Have Dinner Date in New York


Kimye Takes New York!
Kim Kardashian and Kanye West have been
spotted all over the city this week since reuniting
on Monday .
PHOTOS BELOW
On Tuesday night, the parents-to-be were seen
leaving the Trump Soho to have dinner at ABC
Kitchen in Chelsea.
Despite bogus tabloid rumors that West has
deserted Kardashian during her pregnancy, the
couple is managing to make their relationship
work while the rapper spends time recording in
Paris.

RACHEL NDAUKA AANGUSHA PARTY LA NGUVU COCO BEACH

Mtangazaji wa Kituo cha Runinga cha Star, Rachel Ndauka jana aliangusha bonge la pati ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa ‘bethidei’ ambayo ilitawaliwa na shangwe za hapa na pale sambamba na vituko vya kila aina. Sherehe hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Hazina Lounge uliopo katika Ufukwe wa Coco jijini Dar ambapo Rachel alitimiza miaka 22 na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki na filamu huku suala la burudani likishika kasi mwanzo mwisho.

CHUZI AMSAJILI BATULI

Direkta wa Kampuni ya Tuesday Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ ameamua kumsajili mwigizaji anayekuja kwa kasi, Batuli ili kuimarisha kampuni yake.

Akizungumza na Centre Spred, Chuz alisema amefikia uamuzi wa kumchukua nyota huyo baada ya kuona uwezo wake katika kazi ambazo amezifanya na zimefanya vizuri sokoni. “Natarajia kumchezesha katika filamu yangu mpya ya Makaburi ya Kinondoni, uwezo wake ni mkubwa nina imani atafanya vizuri,” alisema Mr Chuz.

WANAUME WAMENIPOTEZEA MUDA

MNENGUAJI wa Bendi ya FM Academia, Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ amesema hahitaji mwanaume yoyote kwa sasa kwani wanampotezea muda kwa kipindi kirefu.

Akizungumza na Centre Spread Queen alisema wanaume wamekuwa wakimsumbua mara kwa mara kutaka kampani ya kimapenzi lakini wengi wao wanakuwa hawana mapenzi ya kweli hivyo anaona bora kuwapiga chini. “Bora niwe singo natafuta pesa kuwazawaza hawa wanaume nitaishia kuumia tu na kushindwa kufanya shughuli zang, tena waache kunifuatafuata kwa sasa,’’ alisema Queen Suzy. Mnenguaji huyo alishawahi kuwa na uhusiano na mwimbaji wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Kalala Junior ambaye alizaa naye mtoto mmoja baadaye akatembea na rapa wa FM Academia, G 7 ambao wote ameshamwagana nao.

LULU AINGIA LOCATION!

HATIMAYE staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameingia mzigoni na kufyatua filamu yake mpya baada ya kimya cha muda mrefu, Amani limeinyaka.

Kwa mujibu wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Lulu alitupia picha akiwa ‘location’ kuashiria kwamba amerudi kazini baada ya kusimama kuigiza kwa muda mrefu.

Baadhi ya picha hizo zinamuonesha Lulu akiwa na staa mwingine wa filamu Bongo, Hashimu Kambi mbele ya kamera kwa ajili ya kushuti filamu hiyo ambayo jina lake halijapatikana.

Mara baada ya kutupia picha hizo mtandaoni, watu mbalimbali walimtumia ujumbe kumsifia kwa kumwambia kuwa ana kipaji cha kazi hiyo.

Miss Tanzania namba mbili 2006, Jokate Mwegelo naye alichangia mada hiyo na kumsifu Lulu kwa uwezo wake wa kuigiza. Lulu amekuwa kimya kwa muda mrefu baada ya kupata msala wa kumuua bila ya kukusudia staa mwingine wa filamu za Kibongo, Steven Kanumba, Aprili 7, mwaka jana, hivi sasa yuko nje kwa dhamana.

MTANGAZAJI DIDA ARUDIANA NA MUMEWE G.

Ndoa ya mtangazaji wa Redio Times FM ya jijini Dar, Khadija Shaibu ‘Dida’ imerudi hewani baada ya hivi karibuni mwanadada huyo kuamua kurudiana na mumewe Gervas Mbwiga ‘G’.

Wakiwa wenye furaha siku ya ndoa

Chanzo chetu makini cha habari kilichoomba hifadhi ya jina lake kilieleza kuwa wawili hao waliamua kuihuisha ndoa yao waliyoifunga Julai mwaka jana baada ya kumaliza tofauti zao zilizosababisha watengane mwaka jana. Chanzo hicho kikadai kuwa aliyeomba warudiane ni mwanaume ambaye alimtaka Dida amsamehe kwa yaliyotokea na wafungue ukurasa mpya wa maisha yao.

siku ya sherehe ya ndoa yao

“Kwa kifupi sasa hivi wako ‘peace’, wamerudiana na mapenzi yao ya sasa yamekuwa moto kuliko ilivyokuwa awali,” alisema mtoa habari huyo. Katika kujua ukweli wa mambo, mwandishi wetu alimtafuta Dida kupitia simu yake ya kiganjani, alipopatikana na kutakiwa kuzungumzia ishu ya kurudiana na G alisema: “Ni kweli tumerudiana, tuliona tusahau yaliyopita na tuendelee na maisha yetu, sasa ni raha kwa kwenda mbele.”

MACHANGUDOA WANASWA COCO BEACH

NI aibu sana! Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Oparesheni ya Fichua Maovu iliyosimamiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar, OCD Wilbroad Mutafungwa na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai kwa kushirikiana na Global Publishers iliyonasa wanawake wanaojishughulisha na mambo ya ngono usiku kucha.

Katika oparesheni hiyo iliyofanyika usiku wa Jumapili iliyopita watu kibao walinaswa hasa katika Ufukwe wa Coco, jijini Dar akiwemo bibi harusi mmoja na mtoto wa kigogo (jina linahifadhiwa).

BIBI HARUSI LAIVU KWENYE BAJAJ Kwenye ufukwe huo, mwanamke mmoja ambaye jina halikupatikana, aliyedaiwa kufunga ndoa Ijumaa iliyopita, naye alikamatwa katika msako baada ya kunaswa na mwanaume wakifanya ngono kwenye Bajaj.

Katika tukio hilo, mwanaume alifanikiwa kutoka nduki huku akimwacha demu wake akijikusanya kwa kuvaa nguo. Mwanamke huyo naye alifanikiwa kuwatoka askari hao na kukimbilia chooni ambapo aliwakuta wanawake wengine waliojificha hivyo wakakamatwa wote kwa pamoja. Ili kuweka ushahidi, askari hao wa kazi waliikamata Bajaj hiyo.

ALIKWENDA KUKUMBUSHIA ENZI ZAKE Kwa mujibu wa mwanamke huyo, mkazi wa Kinondoni-Manyanya, usiku huo alifika mahali hapo kukumbushia enzi zake kabla ya kuolewa ambapo ilidaiwa kwamba alikuwa akijiuza ufukweni hapo. Alijitetea kuwa mume wake alisafiri hivyo akaona akakumbushie enzi zake kabla hata ‘hina’ aliyopakwa wakati wa harusi haijafutika mwilini. Pamoja na maelezo hayo, mwanamke huyo aliishia kwenye ‘difenda’ la polisi tayari kwa kupelekwa kituoni kwa maelezo zaidi.

BINTI WA KIGOGO Katika kundi hilo la wanawake na wanaume zaidi ya hamsini waliokamatwa ufukweni hapo usiku huo wa saa 9 na ushee, kulikuwa na mtoto wa kigogo mmoja serikalini katika idara nyeti ambaye alinaswa mchangani baharini akiwa kwenye kundi la makahaba. Mtoto huyo aligundulika kuwa ni binti wa mnene wakati wa kutoa maelezo kituoni Oysterbay.

MASIKINI ALIKUWA NA ‘BOIFRENDI’ WAKE Akijitetea wakati wa kutoa maelezo, binti huyo aliyeonekana mrembo na mwenye mvuto wa ajabu, alisema kwamba alikuwa na ‘boifrendi’ wake na kuwa alitoroka kwao usiku huo. Binti huyo aliomba chondechonde asipigwe picha kwani endapo itaonekana gazetini basi atakuwa amejipalia makaa nyumbani kwa vile hataeleweka kwa sababu anapatiwa fedha za matumizi pamoja na ada ya shule. Ukiacha mwanamke na binti huyo wa kigogo, wanawake wengine wengi walikamatwa, wengi wao walikutwa wakifanya vitendo vya ngono mchangani wakiwa ‘pea’.

MACHANGU WAFUNGUKA Kati ya wote waliokamatwa, wanawake kumi na tano walikiri kujishughulisha na biashara ya kuuza miili ambapo walisema wanafanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.

ACD MUTAFUNGWA ANASEMAJE? Kwa upande wake OCD Mutafungwa alisema wameamua kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi kwa kuvamia eneo hilo.

INSPEKTA SWAI ATIA NENO Naye Inspekta Swai aliyekuwa ‘front’ katika zoezi hilo alisema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu kila wiki ili kukomesha vitendo viovu katika ufukwe huo.

NI MATOKEO YA GAZETI LA RISASI Oparesheni hiyo ilikuja siku chache baada ya gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko, toleo namba 1000 la Jumatano ya Aprili 17-19 kuripoti ufuska unaofanyika katika ufukwe huo usiku wa saa 9 na kuendelea. Uchunguzi wa gazeti hilo ulieleza kiundani vitendo vya ngono, usagaji, ubakaji, ushoga na ujambazi vilivyokuwa vikifanyika eneo hilo hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni wakaona kuna kila sababu ya kufumua uozo huo kwa kuwa ni wachapakazi.

Tuesday, April 23, 2013

PADR AMCHARANGA MAPANGA KIMADA WAKE

Vitendo vya kikatili vimekuwa vikitekelezwa katika sura mbalimbali, ila tukio la mtumishi wa Mungu, Padri Celestine John Nyaumba, 35, kumgonga kwa gari makusudi na kumcharanga mapanga mzazi mwenzake ni aibu isiyo na mfano. Padri Celestine, anayetoa huduma kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Homboro, Dodoma, anatuhumiwa kumtendea unyama huo, mzazi mwenzake, Selestina Anania Kibena, 35, Jumamosi iliyopita, Kata ya Kiluvya, Pwani. Hii ni aibu isiyomithilika kwa sababu padri kufanya ukatili huo ni kashfa nzito, ongezea kwamba alimfanyia hivyo mzazi mwenzake, wakati kwa sheria za kanisa, ni mwiko kwa padri kujihusisha na mapenzi achilia mbali kufikia hatua ya kuzaa. Aibu hiyo, inapata uzito zaidi kwa kuwa Selestina (mzazi mwenza wa padri), alikuwa mtawa (sister), lakini usista ulimshinda baada ya kupata mimba, takriban miaka minne iliyopita.

TUKIO LILIVYOKUWA Padri Celestine, akiwa anaendelea na utoaji wa huduma kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, alipata nafasi ya kujiendeleza kimasomo, Chuo Kikuu cha Ardhi, Kitivo cha Ubunifu na Uchoraji wa Majengo, Dar es Salaam. Akiwa Dar, Padri Celestine anaishi Mbezi Shamba, wakati Selestina ni mkazi wa Maili Mbili, Dodoma. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, mapema wiki iliyopita, Padri Celestine, alimwita Selestina, aungane naye Dar es Salaam, ‘wapumzishane’ kwa siku chache, kwani inadaiwa kwamba uhusiano wao wa kimapenzi ulikuwa unaendelea kwa siri.

MPANGO WA KIKATILI Habari zinatiririsha mambo kama ifuatavyo: Ijumaa iliyopita, Selestina aliwasili Dar es Salaam na kufikia nyumbani kwa Padri Celestine. Siku hiyo (Ijumaa), walizungumza mengi, ikiwemo kupanga mambo mbalimbali kuhusu maisha yao na mtoto wao ambaye sasa ana umri wa miaka mitatu. Siku iliyofuata (Jumamosi iliyopita), Padri Celestine, alimwomba Selestina, waongozane kwenda Kiluvya, Pwani. Selestina hakuwa na shaka juu ya hilo lakini akataka sababu ya kwenda Kiluvya, badala ya sehemu nyingine. Celestine akamweleza kuwa Kiluvya kuna sehemu nzuri ya kupumzika, vilevile ana jambo la kikazi atalifanya akiwa huko.

UKATILI UKATENDEKA Ilipofika usiku wa siku hiyo (Jumamosi), Padri Celestine na Selestina, walianza safari ya kutokea Mbezi Shamba kwenda Kiluvya, wakiwa na gari aina ya Suzuki lenye namba za usajili T220 AJN. “Walipofika Kiluvya, Padri Celestine ambaye alikuwa anaendesha gari hilo, alikata kushoto kuelekea porini. Gari likiwa porini kabisa, Padri Celestine alisimamisha kisha akamwambia Selestina ashuke kuangalia chini, kwani alihisi kuna tatizo,” kilisema chanzo chetu na kuongeza: “Selestina alishuka akainama chini kwenye uvungu wa gari kuangalia tatizo, ile anafanya hivyo tu, Padri Celestine aliendesha gari kwa spidi ili amgonge Selestina. Bahati nzuri Selestina aliruka lakini gari lilimgonga kwenye paja la kushoto. “Baada ya hapo, Celestine aligeuza gari amgonge tena lakini Selestina alijirusha sehemu yenye kishimo fulani hivi, kwa hiyo gari lilikuwa haliwezi kumfikia. Kuona hivyo, Padri Celestine alianza kumpiga mawe Celestine. “Pengine aliona yale mawe hayana uzito wa kutimiza kile ambacho alitaka kukifanya kwa Selestina, kwa hiyo Padri Celestine alifuata panga kwenye gari, akamfuata Selestina, akamcharanga mapanga kichwani, kwenye mikono yote miwili na mguu wa kushoto. “Kabla hajaendelea zaidi, Selestina alimrukia, purukushani ikaendelea. Padri Celestine alimng’ata Selestina katika shavu la kushoto, mwanamke huyo naye akajibu mapigo, akamng’ata padri katika shavu la kulia. “Baada ya purukushani ya muda mrefu, Padri Celestine aliona mambo magumu, ikabidi amwombe msamaha Selestina kwamba shetani alimpitia, akamwomba ampeleke hospitali. “Selestina alikubali lakini ile Padri Celestine anafuata gari, Selestina alijitutumua na kukimbia mbali zaidi, Padri Celestine aliporudi pale alipomwacha, hakumwona tena.”

HOSPITALI NA POLISI TUMBI Chanzo chetu kilisema: “Selestina alijivuta mpaka Hospitali ya Mkoa wa Pwani, Tumbi. Vilevile alitoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Tumbi. “Polisi walianza kufanya upelelezi wao na kufanikiwa kumkamata Padri Celestine, Jumapili iliyopita jioni.”

RPC ANENA Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, alikiri kutokea kwa tukio hilo na akafafanua kwamba baada ya Padri Celestine kuhojiwa, alisema alipitiwa na shetani kutokana na usumbufu aliokuwa anaupata kutoka kwa Selestina. Kamanda Matei alisema, Padri Celestine alidai kuwa Selestina alikuwa anamuomba fedha nyingi za matumizi kwa ajili ya mtoto wao, kwa hiyo shetani alimpanda na kufikia hatua ya kufanya kile alichokitenda.

SELESTINA NAYE AZUNGUMZA Akiwa amelazwa Hospitali ya Tumbi, Selestina alisema: “Nashangaa kwa kila kilichotokea. Niliitwa na Padri Celestina kuja kupumzika, nashangaa mapumziko yamegeuka mateso.”

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...