Friday, April 26, 2013

MTANGAZAJI DIDA ARUDIANA NA MUMEWE G.

Ndoa ya mtangazaji wa Redio Times FM ya jijini Dar, Khadija Shaibu ‘Dida’ imerudi hewani baada ya hivi karibuni mwanadada huyo kuamua kurudiana na mumewe Gervas Mbwiga ‘G’.

Wakiwa wenye furaha siku ya ndoa

Chanzo chetu makini cha habari kilichoomba hifadhi ya jina lake kilieleza kuwa wawili hao waliamua kuihuisha ndoa yao waliyoifunga Julai mwaka jana baada ya kumaliza tofauti zao zilizosababisha watengane mwaka jana. Chanzo hicho kikadai kuwa aliyeomba warudiane ni mwanaume ambaye alimtaka Dida amsamehe kwa yaliyotokea na wafungue ukurasa mpya wa maisha yao.

siku ya sherehe ya ndoa yao

“Kwa kifupi sasa hivi wako ‘peace’, wamerudiana na mapenzi yao ya sasa yamekuwa moto kuliko ilivyokuwa awali,” alisema mtoa habari huyo. Katika kujua ukweli wa mambo, mwandishi wetu alimtafuta Dida kupitia simu yake ya kiganjani, alipopatikana na kutakiwa kuzungumzia ishu ya kurudiana na G alisema: “Ni kweli tumerudiana, tuliona tusahau yaliyopita na tuendelee na maisha yetu, sasa ni raha kwa kwenda mbele.”

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...