Sunday, April 28, 2013

MAPYA YAIBUKA

MAPYA yameibuka kufuatia utata wa kifo cha Mwalimu Elizabeth Mmbaga (22) kilichotokea kwa madai ya kunyongwa usiku wa kuamkia Jumatatu, Aprili 15, mwaka huu nyumbani kwake, Kimara -Baruti, Kinondoni, jijini Dar.

Hapa ndipo ulipo kutwa mwili wa marehemu Elizabeth

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini mambo mapya kiasi cha kukifanya kifo hicho kihusishwe na mauaji ya kikatili yanayodaiwa kufanywa na mpenzi wake ambaye ni Mtanzania mwenye asili ya Kiasia aliyejulikana kwa jina la Srinivas, mkazi wa Mikocheni, Dar.

Ndugu wakifungua chumba cha marehemu

Timu ya wachunguzi wetu ilimtafuta mjomba wa marehemu anayeishi Mabibo, Dar ambaye inadaiwa ndiye aliyekuwa akiwasuluhisha Eliza na mpenzi wake na kumuuliza kuhusu kifo hicho na mambo mapya yaliyopo.

Mmoja wa ndugu wa marehemu akimtambua muuaji kwenya picha

“Nakumbuka wiki moja kabla ya mauaji, Elizabeth alinieleza kwa njia ya simu kuwa alipata taarifa toka kwa rafiki yake ambaye ni jirani yake akimwambia kwamba jamaa yake huyo yupo katika baa iliyopo jirani na nyumba aliyokuwa akiishi. “Ilinibidi nikutane na Eliza, tukafuatana naye hadi kwake kwa vile yule Mhindi alikuwa akimtishia kila mara kwamba atamuua kutokana na mgogoro wao wa kimapenzi.

Enzi za uhai wa marehemu

“Tulipokaribia yule Mhindi akawa anaondoka nyumbani hapo akifuatana na vijana wawili ambao hatujawahi kuwaona. Waliingia kwenye Bajaj, mimi niliwapigia winja, wakasimama, kijana mmoja alishuka na kunifuata. “Nilimwomba na yule Mhindi ashuke. Nikajitambulisha kwake mimi ni mjomba wa Eliza na kwamba nimepata taarifa anataka kumfanyia fujo Eliza, nikamuuliza kuna tatizo gani? “Alinijibu hawezi kufanya fujo. Hata hivyo, haikuchukua muda wakaanza kuzozana mbele yangu huku Mhindi akimuuliza ni kwa nini anampigia simu hapokei! “Ilibidi nimwombe Eliza aondoke mimi niongee na yule Mhindi ingawa Eliza hakuondoka. Nilimuuliza ana muda gani tangu aanze kufahamiana na Eliza, alijibu ni miezi saba. “Nilimuuliza kama hawajawahi kukorofishana hata siku moja? Alinijibu wamekuwa wakikorofishana mara kwa mara, nikamshauri aachane naye, akasema anampenda sana hawezi kumwacha. “Eliza aliingilia kati na kumwambia Mhindi kuwa yeye hampendi, Mhindi akasema yaishe naondoka lakini utaona. “Wakati huo ilikuwa kama saa tano usiku. Mhindi aliingia kwenye Bajaj na kuondoka na wale vijana wawili. Nilimwambia Eliza asilale kwake, alifanya hivyo ambapo alikwenda kwa mama’ke mdogo, Tabata -Barakuda. “Siku ya tukio, saa kumi jioni mama’ke alinipigia simu akinitaka tukutane kwa Eliza. Tulipofika tulikuta walimu wenzake wakilia, tuliwauliza wanacholilia hawakutujibu. “Mimi niliamua kuingia ndani kwa Eliza na kumkuta amelala, nilipomwangalia niligundua amefariki dunia. Alikuwa akitokwa damu mdomoni na puani. Ulimi ulikuwa nje huku akiwa na alama kama za kucha shingoni, nahisi alinyongwa kwa mkono. “Nilikwenda Kituo Kidogo cha Polisi Rombo na kutoa taarifa, nikafuatana na polisi wawili mpaka kwenye eneo la tukio. “Inauma sana! Hakuna kitu chake chochote kilichochukuliwa, hakika Eliza angetoa taarifa mapema polisi kama alivyoshauriwa kufuatia vitisho vya yule jamaa asingeuawa,” alisema mjomba mtu huyo. Mama mdogo wa marehemu, Anna Domisian naye alikuwa na haya ya kusema: “Siku hiyo ya Jumatatu, saa tisa alasiri nilipigiwa simu na mwalimu mmoja akinitaka nifike Kimara kwa Eliza, hawakuniambia kilichotokea. Nilipofika nikakuta mwili wa Eliza ukiwa juu ya kitanda. Nilipatwa na mshtuko mkubwa kwani Jumapili jioni aliniaga anarudi kwake. “Siku za nyuma aliwahi kunieleza juu ya fujo anazofanyiwa na mpenzi wake wa Kihindi na ndiyo maana nilimweleza mjomba wake aende akawasikilize.”

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...