Sunday, April 28, 2013

ISHA MASHAUZI ASWEKWA NDANI KWA UTAPELI

MWIMBAJI ambaye pia ni bosi wa Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhan Makongo

alikumbwa na masaibu mazito kufuatia kudakwa na polisi wa Kituo cha Msimbazi, Dar akituhumiwa kukwapua mkoba wenye kitita cha shilingi laki saba, elfu hamsini na nane na mia mbili (758,200) mali ya Veronica Tarik.

ANASEPA: Mashauzi akiwakimbia Waandishi wa Global kuelekea kwenye Gari baada ya kutolewa dhamana

Chanzo cha habari kituoni hapo kilidai kuwa Jumanne iliyopita, Isha Mashauzi na shosti wake aliyejulikana kwa jina la Halima Shaban waliingia duka moja Mtaa wa Mafia na Jangwani, Kariakoo, Dar kwa lengo la kufanya ‘shopping’ lakini walipochomoka, Veronica alishangaa kutouona mkoba wake.

ISHA AKIMBIZWA Veronica aliwakimbiza wawili hao na kuwadaka mtaa wa pili na kuwasomea tuhuma zao kisha akawaomba awasachi kwenye mafurushi waliyobeba lakini Isha na mshirika wake waligoma, hali iliyosababisha kuzuka kwa timbwili wakidai mwanamke huyo alitaka kuwadhalilisha.

Baada ya Veronica aliyekuwa na wapambe ‘legelege’ kuzidiwa nguvu, waligeuka na kukimbilia Kituo cha Polisi Msimbazi ambako alifungua kesi ya wizi kwa Isha na shosti wake kwa jalada namba MS/RB/4023/2013.

MSAKO MTAA KWA MTAA WAANZA Maafande wenye difenda waliingia mitaani kuwasaka watuhumiwa hao mtaa hadi mtaa wakitumia mbinu mpya za kikachero na kufanikiwa kuwatia mbaroni Jumatano iliyopita. Isha akiwa selo, wapambe wake walimiminika kituoni hapo akiwemo Mtangazaji wa Kituo cha Redio Times FM cha jijini Dar, Hadija Shaibu ‘Dida’ kwa ajili ya kuhangaikia kuwachomoa wawili hao.

WAPAMBE WAMCHOMOA Saa 5:14 usiku, wapambe hao walifanikiwa kuwawekea dhamana lakini kasheshe nzito ilikuwa wakati wa kutoka rumande kwani wapambe wa Isha waligundua kuwa mapaparazi walikuwa wamekizingira kituo hicho na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kunasa picha zao. Isha alijaribu kujibanza ndani ya selo lakini wapambe walimpelekea taarifa kuwa mapaparazi nje walikuwa wakijipanga kukesha kituoni hapo mpaka siku itakayofuata. Baada ya kupata ujumbe huo, Isha alichomoka mahabusu kwa kasi ya mnyama swala na kukimbilia kwenye gari aliloandaliwa kumchukua huku wapambe wake wakiwa wamezikamata kamera za mapaparazi eti ili wasimpige picha.

MSIKIE ISHA MASHAUZI Kesho yake Alhamisi, paparazi alizungumza na Isha kwa njia ya simu ili aweze kuweka bayana juu ya sakata hilo lakini mwimbaji huyo alimjibu mbofumbofu. “Wewe andika unachotaka si ulikuwepo kituoni na umenipiga picha, sasa unataka nini? Yaani hata wewe unanifanyia hivyo duh! Leo nimeamini mapaparazi hawana undugu,” alisema Isha na kukata simu.

1 comment:

  1. eToro is the best forex trading platform for newbie and advanced traders.

    ReplyDelete

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...