HADITHI ZA KUSISIMUA

 

 

 

Mtunzi:   Godwill 
                 Sanga
Makazi:   Arusha, 
                 Tanzania Contacts: 0657 35728
                           0756979566
                 

 

 

JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.21

 

Alikuwa ni Lulu ambaye alionekana kutokuwa na furaha yoyote ile na hii ilijidhihirisha wazi moja kwa moja toka usoni kwake hali iliyomfanya Sele kumkaribia na kumuuliza "kulikoni rafiki yangu?""niko sawa tu,kwani unaonaje,aliuliza Lulu."niambie ukweli kwani unaonyesha wazi kwamba hauko sawa, tafadhali niambie,Sele alisisitiza.Akiwa anajiweka sawa kwa kuelezea yote yanayo msibu alijikuta akitokwa na machozi mengi ,Sele alijaribu kumtuliza.Lulu aliongea kwa kwikwi "nawakumbu.......ka......wa.....za.....zi,alishindwa kuendelea kuzungumza huku kilio cha kwiki nacho kilimbana.Baada ya kutulia kidogo aliendelea"unajua Sele natamani sana kama wazazi wangu wangekuwepo katika mahafali haya,ningefurahi sana tena mno""usijali sahau hayo maana hiyo ni kazi ya Mungu na haina makosa ,acha basi kuwa mnyonge tusherekee vizuri,alisema Sele.Kwa shingo upande Lulu alikubali kuendelea na maandalizi ya mahafali yao.Muda wa mahafali uliwadia ,wageni nao walikuwa wamesha wasili,kwa bwembwe nyingi na shamra shamra sana wahitumu waliingia ndani ya ukumbi ulio pambwa vizuri na ukapambika haswa,punde si punde kelele zililindima ukumbini «««happy day,happy day»»»».Wazazi wa Selemani waliwasili ukumbini huku wakiwa wamekumbatia zawadi nyingi bila shaka zilikuwa kwa ajili ya mwanao , naye mjomba ake na Lulu sanjari na mkewe walikuwepo ukumbini.Burudani ziliendelea huku watu wakiserebuka na kula na kunywa.Wakati hayo yote yakiendelea Lulu alimwita Sele na kumnong'oneza kitu*********

  

JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.20

 

Wanafunzi wa shule moja waliongoza katika mashindano yale ya debate na hawa si wengine bali ni Lulu na Seleman kutoka shule ya sekondari Jitegemee.Katika mashindano hayo Lulu na Seleman waliweza kuelezea vizuri sana namna ukosefu wa demokrasia katika nchi unavyoweza kuchangia kudidimiza maendeleo ya nchi.,kutokana na maelezo yao bora walizawadiwa computer moja kila mmoja.Jambo hilo lilikuwa la furaha sana kwao hivyo walipongezwa na wote waliohudhuria ile debate na wao pia walipongezana.Haya yote yaliendelea kuwatia moyo na kuwapa ari na hamasa kubwa ya kufanya vizuri zaidi katika masomo yao.Maisha yao ya shule yalikuwa ya kuigwa kwani kila mwanafunzi darasani mwao alipenda kwenda kuuliza maswali pamoja na kuomba ushauri wa kimasomo kwa Seleman na Lulu na hii ilikuwa kwasababu tu walikuwa na uwezo mzurri wa kimasomo.Hali haikuishia hapo waliendelea kupendwa na walimu wao kwani siku moja wakiwa darasani wanafunzi wenzao walipanga kumpiga mawe mwalimu wao wa kiingereza sambamba na kuchoma moto nyumba yake kisa alikuwa haingii darasani kufundisha na ifikapo mwisho wa muhula huingia na kutoa mtihani ,wakiwa katikati ya mazungumzo yao Lulu na Seleman walishauriana namna ya kutuliza jazba ile na hatimaye kutoa wazo la kumuita mwalimu husika na kumweleza shida yao na kumtaka awe anahudhuria vipindi.Uamuzi huo ulipokelewa na wanafunzi wote ambao walimwita mwalimu na kumweleza yote ,naye mwalimu alikiri akisema "nisameheni wanafunzi nitabadilika" na hii ilisababisha amani kutawala tena pale shuleni kwao.Miaka nayo ilizidi kwenda kadhalika pia siku nazo zilikuwa hazigandi Lulu na Seleman walimatiza kidato cha nne.Muda wa matokeo kutoka uliwadia ambapo shule ya sekondari Jitegemee ili faulisha wanafunzi wote kwa kiwango cha daraja la kwanza na la pili,kwa upande wao Lulu na Seleman walipata daraja la kwwanza yaani "division one" na ilikuwa ni bahati sana kwao kwani walichaguliwa kujiunga kidato cha tano katika shule moja.Maisha ya "high level" yalikwenda salama na hatimaye siku iliyokuwa ikingojewa iliwadia ambapo Lulu na Seleman walifika ukingoni mwa elimu yao ya sekondari yaani kidato cha sita.Siku ya mahafali yao iliwadia huku kila mmoja akiipokea kwa hamu kubwa na katika hali isiyotegemewa Selemani aliona kitu******

 

JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.19

 Mwili wa mama Lulu ulikuwa umekauka na hakukuwa na dalili yeyote ya yeye kupumua,akawataarifu wenzake na mara baada ya kumwangalia vizuri waligundua kwamba alikuwa amekwisha fariki dunia.Lulu alishuhudia kifo hicho cha mama yake kipenzi,Lulu alilia sana tena kwa uchungu na majonzi mengi kwani tayari alikuwa ameuanza ukurasa mpya wa kukosa mapenzi na malezi ya baba na mama yaani ukurasa wa uyatima,alikumbuka maisha aliyoishi na mama yake huku akibugujikwa na machozi tele.Taratibu za mazishi zilifanyika na ndugu wa Lulu waliwasili pale kimara na hatimaye mazishi yalifanyika katika makaburi ya kinondoni,mahali pale pale alipozikwa mzee John .Baada ya mazishi kumalizika wanandugu wa Lulu walikaa kikao na kuamua kwa pamoja kwamba mjomba ake na Lulu ndiye atakae mlea Lulu mpaka atakapofikisha umri wa kujitegemea.Wakati mama yake na Lulu anafariki dunia Lulu alikuwa akisubiri matokeo yake hasa mara baada ya kuhitimu darasa la saba.Hivyo Lulu alilazimika kuhamia Mbagala kwa mjomba ake,ambako alienda kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya jitegemee.Lulu alipokelewa vizuri katika familia ile ya mjombaake na maisha yalikuwa mazuri kwani alipewa mahitaji yote aliyoyahitaji.Alipendwa sana na shangazi yake na kila siku alimsisitizia kusoma kwa bidii.Lulu alionyesha kusikia na kushika vizuri yaleyote aliyoambiwa kwani kila mtihani alikuwa anakuwa wa kwanza darasani hali iliyompelekea kupendwa na kila mtu si wanafunzi wenzake tu bali hata walimu wake.Lulu aliendelea kujituma zaidi ili aweze kufaulu mitihani yake,pamoja na hayo yote alikutana na Seleman ambaye alikuwa classment wake katika shule ya sekondari jitegemee,walishirikiana vizuri sana katika masomo yao hivyo kuweka ushindani mkubwa sana katika nafasi ya kwanza na ya pili darasani mwao.Siku moja Lulu na Seleman walichaguliwa kwenda kuiwakilisha shule yao katika mashindano ya 'debate' ambapo shule zote za Tanzania zilihudhuria kupitia wawakilishi wao,ambapo katika mashindano hayo kulitokea kitu cha kushangaza********** Usikose Episode 20........

 


JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.18

 Karatasi ya majibu ilionyesha kwamba mzee John alikuwa anaugua kansa ya tumbo ambayo ni ngumu sana kwa yeye kupona.Taarifa hii ya daktari ili wasononesha sana na kuwastua sana akina Lulu na mama yake,ambao macho yao haya kusita kuonyesha hisia kwa kutoka machozi mithili ya mvua nyikani.Siku ile mkewe na mzee John pamoja na mwanae hawakuondoka pale hospitalini.Ilipofika majira ya saa moja usiku hali ya afya ya mzee John ilianza kutia matumaini walau kidogo kwani aliweza kuongea japo kwa shida shida,mzee John akamwita mkewe sanjari na mwanae Lulu kisha kuwaambia"mke wangu nakuomba jitahidi sana umsomeshe mwanetu mpendwa,tunza zile mali zetu,wakati haya yote yakiendelea mkewe na mzee John alikuwa amejiinamia pembeni ya mumewe huku akibugujikwa na machozi, mzee John aliendelea "nawe mwanangu Lulu kazana kusoma na ushike sana elimu na usimwache aendezake maana huo ndio ufunguo wako wa maisha" kisha kusema hayo aliomba apatiwe maji maana alijihisi kubanwa na kiu,mkewe aliinuka haraka haraka na kuchukua maji na kuanza kumnywesha,akiwa bado anaendelea kumnywesha maji akaona mzee John akishua pumzi kwa haraka na mara akaona maji aliyokuwa akimnywesha yakitoka mdomoni mithili ya udenda,akajiribu kumtikisa huku akiita "mzee John!!"mzee John!!!,hakuna sauti iliyotoa jibu,mkewe alianza kulia kwa sauti huku akimwita daktari aje kumpa msaada.Mara baada ya daktari kuchukua vipimo kwa mzee John aliwageukia mkewe na John na mwanae,"kwakweli mzee hatunaye tena" kauli hiyo ilipokelewa kwa vilio vikali.Mwili wa marehu ulifunikwa na kuchukuliwa mpaka mochwari ambako ulihifadhiwa kusubiri taratibu za mazishi.Tarattibu za mazishi zilifanyika na mwili wa marehemu ulipata nyumba ya milele katika makaburi ya kinondoni.Wakati mzee John anafariki dunia Lulu alikuwa na umri upatao miaka saba.Kifo cha mzee John kilimpa majonzi mengi na simanzi kubwa mama lulu hali iliyopelekea afya yake kudhoofu kutokana na msongo wa mawazo hali hiyo ilimpelekea kukosa nguvu na kumshawishi ajione mwenye mikosi na balaa tupu hapa duniani kisha kumlilia Mungu wake "kwanini mimi tu".Miaka ilizidi kusonga na hali ya mkewe na mzee John ilirejea katika hali yake ya kawaida hasa baada ya mawazo na kumbukumbu za kifo cha mumewe kuanza kupotea.Siku moja mkewe na mzee John alikuwa akitoka katika kazi yake ya kuuza mboga mboga za majani alijihisi kuumwa na kichwa lakini alifikiri kuwa hali hiyo ilisababishwa na jua kwani siku hiyo alishinda juani.Siku zilisogea hali ya mkewe na mzee John ilizidi kubadilika na kuwa mbaya,hali ya iliyomlazimu Lulu kumwendea jirani yao ,bwana Masele na kuomba msaada.Taarifa ziliwafikia pia majirani wengine ambao walimchukua na kumpeleka hospitali.walipokuwa njiani mmoja wa majirani aligungua kitu****

 

JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.17

Kwakweli nimeamua kuwaiteni hapa ili kuwa fahamisheni kwamba "hali yangu ya kiafya inazorota''.kauli hiyo ilitoka kwasababu alikuwa amepatwa na uvimbe sehemu yake ya kulia ya tumbo lake,mkewe na mzee John alionekana mnyonge na mwenye simanzi kubwa,na akajikuta akitamka"pole baba lulu tumwombe Mungu atatusaidia,maana sisi sote ni watoto wake na ipo siku utapona" kisha kusema hayo Mzee John aliiendelea na wewe mwanangu kipenzi cha roho yangu kazana sana kusoma na hakikisha unaongoza darasani"sawaee""ndio baba" Lulu alijibu,mzee aliendelea, maana hiyo elimu ndio ukombozi wako,mimi na mama yako unavyotuona hapa hatukufanikiwa kusoma enzi zetu na ni kwasababu wazazi wetu hawakuwa na uwezo wa kutulipia ada,ila wewe mwanetu umebahatika kusoma tumia nafasi hiyo ili uje uwe na maisha mazuri na ya raha, si umenielewa,"ndio baba" Lulu alijibu kwa ujasiri mkubwa kisha kumalizia"baba na mama kamwe sitawaangusha".Kadiri siku zilivyozidi kwenda ndivyo Lulu alivyozidi kukua na wakati hali ya afya ya mzee John ilikuwa bado haieleweki yaani haijatengamaa na hivyo kupelekea yeye kulazwa katika hospitali ya Lugalo.Madaktari walimpokea na kumfanyia vipimo,vipimo vilipo kamilika familia ya mzee John ilitwa na daktari,baada ya mkewe na mzee John kuketi daktari aliwapa pole kisha kufungua karatasi ya majibu*******
 
   Je nini kitatokea??? usikose kufuatilia episode 18.......

 

JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.16

Daktari aliitwa haraka na kwenda,alipofika alimkuta mkewe na kamanda akikata roho,akamfunika shuka kisha kuwaambia wale askari waliokuwa karibu kisha akatoka kwenda kuandaa cheti cha kifo,baada ya kumaliza askari waliutwaa mwili wa marehemu na kwenda kuuzika.Miaka mitano ilikuwa imepitaa ambapo Lulu alikuwa mkubwa kidogo,siku moja jioni mkewe na mzee John alimwita mwanae na kumuuliza"mwanangu ungependa kuja kuwa nani ukiwa mkubwa?","kuwa mwanasheria "Lulu aliendelea kwani ninapenda sana kuja kuwa mtetezi wa kinamama na watoto kwani mwalimu alitufundisha kuwa katika jamii zetu watoto na wanawake ndio watu wanaoonewa sana."sasa kazana sana na masomo".Maneno hayo yalimfurahisha sana mkewe na mzee John kwa furaha alimkumbatia mwanae.Maisha yaliendelea kwa amani na furaha lakini kwa upande mwingine maisha ya pale kimara yakizidi kuwa magumu,hali iliyomfanya mzee John awe anachelewa kurudi nyumbani sababu ya kusubili wateja katika toyo yake.Jioni ilipofika mzee John alimwita mkewe na mwanae na kuwaambia kuna jambo anataka wazungumze******
JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.15

:Hazikupita dakika tano hakimu akasema"kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizo wekwa mtuhumiwa anahukumiwa kifungo cha maisha na kazi ngumu" kisha kumaliza halpo askari liita "court!!!!"""" watu wakasimama hakimu akatoka nje .Mkewe na kamanda alitokwa na chozi mara baada ya hukumu hasa pale alipokumbuka kwamba maisha aliyokuwa akiishi yalisababishwa na mumewe kamanda ambaye kamwe hakuwa chaguo lake la moyoni kwani wazazi wake ndio waliomlazimisha kuolewa nae hasa kutokana na tamaa ya pesa.Alikuwa ameshindwa kutoroka hasa kwa sababu alitishwa kuuwawa endapo angejaribu kutoroka,aliwaza pia ni namna gani ataenda kuishi gerezani kwani hali ya maisha hayo alikuwa akiiona kwenye television.Polisi wakamchukua na kumuingiza garini tayari kuelekea gerezani kutumikia adhabu yake.Njiani mkewe kamanda alionena kuweka kichwa dirishani ili awezekuiona dunia kwa mara ya mwisho.Ni miaka miwili sasa tangu mkewe na kamanda aanze kutumikia adhabu yake,umbo lake lilionekana kupungua na kuzoofu pia alikuwa mtu mwenye msongo wa mawazo.Mfungwa mmoja aliyekuwa rafiki yake alijaribu kumshauri kwamba ayakubali tu maisha hayo kwani ndio yaliyobaki na kuachana na mawazo,lakini ushauri huo ulikuwa kama upepo haya kupata hata chembe ya nafasi katika kichwa cha mkewe na kamanda chazaidi ni kwamba aliiendelea kujitenga na wenzake.Mwaka mmoja baadae hali ya mkewe na kamanda ilizidi kuwa mbaya kwani sasa ikuwa hali tena chakula hivyo mkuu wa gereza akaagiza apelekwe hospitali.Alichukuliwa haraka haraka mpaka hospitali na mara baada ya kuwasili walipokelewa na daktari kisha mgonjwa kulazwa chini ya uangalizi mkali wa askari na ilipofika mjira ya saa nane usiku hali ya mgonjwa ili badilika ***** 


 JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.14

Walielekea kule damu ilikokuwa inatokea mpaka walipofika mbele ya mlango wa chumba cha mkewe na kamanda.Polisi walipeana ishara za kijeshi wakiwa na lengo la kujipa tahadhari hasa kwa kutojua ninini kilichopo ndani na ninani aliyopo huku,polisi wawili waliingia kwa tahadhari huku bastola zao zikiwa mbele.Mkewe na kamanda aliendelea kutokwa na damu nyingi zilizotokana na majeraha ya risasi,akiwa bado chini ya nguo aliweza kuona polisi wakiingia na bastola zao,akajaribu kujipapasa na kuangalia kama anabastola lakini alikua ameisahau pale sebuleni,akaamua kusubiri kitakacho tokea na kitokee,kisha polisi kuingia waliangalia kila kona kisha kuzirudia zile damu na kukuta zimeishia kwenye lundo kubwa la nguo,wakazipangua zile nguo haraka haraka na kukutana uso kwa uso na mke wa kamanda,wakamchukua mkukumkuku na kumpeleka kwenye gari la polisi hukuakiwa ndani ya pingu na kuambia kuwa yeye ni muuaji,maneno yaliyoenda sanjari na kipigo.Polisi wengine walianza kuipekua nyumba nzima ya kamanda na kufanikiwa kukuta kilogram mia mbili za madawa ya kulevya,wakayachukua na kwenda nayo kituoni.Jalada la kesi lilifunguliwa kama kesi ya mauaji na ya kukitwa na madawa ya kulevya.Mawakili wa pande zote mbili waliendelea kubishana kisheria.Kwa ujumla kesi ilikuwa imebalansi kiasi kwamba hukumu ilikuwa haitabiri .Hatimaye siku ya hukumu iliwadia mkewe na kamanda alipandishwa kizimbani chini ya ulinzi mkali wa askari polisi hukuwakizongwazongwa na waandishi wa habari waliotaka kupamba vyombo vyao vya habari.Punde si punde hakimu aliingia mahakamani ,watu wote wakasimama kama ilivyo ada ya mahakamani,kisha hakimu kukalia kiti cha akaanza kutoa maelezo mafupi kuhusu ile kesi huku vifungu vya sheria vikitumika na sasa akaanza kutoa hukumu,watu ndani ya mahakama walitulia tuli kusubiri hiyo hukumu huku mawakili wa pande zote mbili wakionekana kutokuwa na wasiwasi huku kila mmoja akiamini upande wake utashinda*****

 JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.13

Mzee John na mkewe waliingia ndani kisha kumfuata mtoto wao Lulu, mzee John hakuweza kujizuia chozi lilimdondoka hasa kutokana na mapenzi ya kweli kwa mwanae,alimpakata kisha kumbusu.Mzee John alianza kwa kuulizia kama wavuvi wenzake walikuwa hai na ndipo alipopata habari za kuhuzunisha kwamba walikwisha fariki na matanga yao yamekwisha fanyanywa,kwa kweli ilimuuma sana akabaki kuwa ombea Mungu.Ule wasaha wa mzee John kuelezea nini kilimpata ukafika ambapo alieleza yote aliyofanyiwa na kumshukuru mkewe kwa maombi yake kwa kipindi chote alipokuwa hatari.Kisha mongezi hayo mzee John alichomoa kibunda cha hela alichokuwa amepewa na mkewe na kamanda kisha kuanza kuzihesabu pamoja na mkewe,iliwachukua takribani saa moja kumaliza kuhesabu pesa ambazo zilikuwa shilingi millioni mbili na nusu,loo! ilikuwa ni pesa kubwa kwao hivyo wakaamua kukarabati nyumba yao na kununua toyo(pikipiki).Naam zile risasi mbili zilimwingia mkewe na kamanda barabara na kumpeleka chini,alianza kulia na kuhangaika kwa mauvivu makali akijaribu kujiokoa pasipo matumaini Lakini ghafla alisikia milio ya king'ora nje ya nyumba akajaribu kujikongoja mpaka dirishani na kuchungulia njeLo!walikuwa ni pollisi ambao walianza kuizingira nyumba huku wengine wakianza kuingia ndani,mkewe na kamanda akajivutavuta toka pale dirishani mpaka chumbani kwake.Akiwa ndani alisikia tangazo"yeyote aliyomo ndani ya nyumba hii ajisalimishe" kusikia vile mkewe na kamanda alichukua rundo la nguo na kujifunika ili kujificha.Polisi nao hawakuchelewa waliingia ndani na kukuta maiti ya kamanda na wale walinzi lakini baada ya kuangalia vizuri wakaona michirizi ya damu ikienda mbele wakaamua kuifuatilia

 JINSI JINIALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.12 

kamanda alibwatuka"pumbavu sana,wajinga nyie poteeni nataka mmlete hapa sasa hivi" kamanda alizunguka zunguka zunguka kwa hasira kali huku akiwaza kwamba kama atakuwa ametoroka basi ndo utakuwa muda wa yeye kuanikwa hasa kwa biashara yake haramu ya madawa ya kulevya.Wale walinzi walipita kila chumba ndani ya jumba lile huku wasambarua kila kitu labda pengine watampata mzee John.waliendelea kumtafuta lakini hawakumwona,wakaamua kurudi kwa kamanda na kuripoti kuwa hawaja mwona.Ile kamanda anapokea ile taarifa alichomoa bastola yake na kuwapiga wale walinzi,walinzi wote walianguka chini na kufa papo hapo .Damu ilisambaa chumba kizima.Kamanda aliondoka kwa hasira mpaka chumbani kwake kwa leo la kumuua mkewe lakini alistaajabu kuona kitanda kiwazi,aliangalia uvunguni na mlangoni lakini akaambulia patupu hivyo alizidi kupandwa na hasira akaamua kufungua droo yake na kutoa burungutu la pesa pamoja na vitambulisho vyake vya kusafiria ili aweze kutoroka.Alifanya hivyo himahima na kisha kuiweka bastola yake kiunoni,alifungua mlango na kutoka nje kuelekea car park tayari kwa kutoroka.Lakini alipokuwa akishuka ngazi kuelekea chini alishitushwa na risasi iliyogonga kioo cha dirisha kubwa lililokuwa mbele yake.Kamanda alibonyea chini kwa ustadi mkubwa kisha kuchomoa bastola yake na kujibu mapigo na huo ukawa ndo mwanzo wa kurushiana rasasi lakini mkewe na kamanda alitumia ustadi mkubwa akamlenga kamanda risasi ya bega"paaaa!!!!!" "aaaaghhhhh"kamanda aliguna.Mzee John nae alikaribia mazingira ya nyumbani kwake kimara kisha kubisha hodi"hodiiii""karibu"aliitikia mkewe na mzee John,ile mkewe na mzee John anatoka nje kufungua mlango akakutanisha macho yake na mzee John,ila hakuamini akaamua kuita mzee Johnnn!!!naam mama Lulu .Kuona vile mkewe na mzee John aliruka na kumkumbatia mzee John kwa furaha kubwa hali iliyompelekea kutoa machozi.Kamanda alianguka chini"puu" na kutulia kimya huku damu zikiendelea kumtoka,mkewe na kamanda alijihakikishia kwamba amemaliza jazi hivyo alimsogelea kamanda ili aweze kuchukua hela,akiwa anasogea kamanda alinyanyuka ghafla na kumfyatulia risasi mbili za kifua kwa mkewe ****

 

JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.11
Ule mlio uliwashitua lakini wakaamua kuendelea ila kwa tahadhari kubwa.Waliendelea kupanda ngazi mpaka walipo fika ghorofa ya juu,walipofika huko walikuta kibalaza cha kupumzikia ambapo ukiwa pale unaweza kuona mji wote.Mkewe na kamanda alitoo burungutu la manoti ya elfu kumi na elfu tano kisha kumkabizi mzee John na kumwambia "hizo zitakusaidia nauli ukifika chini chukua taxi itakayo kupeleka mpaka bahari huko utaingia boti litakalokupeleka mpaka dar es salaam sawa!!?"sawa asante "alijibu mzee John na kulitia burungutu lile mfukoni.Kwa mara nyingine tena mkewe na kamanda alitoa kamba ndefu kisha akaifunga vizuri kwenye nguzo iliyokuwa karibu na kumwambia mzee John kwamba atatumia kamba hiyo kushuka mpaka chini.Basi mzee John alipanda kamba haraka haraka na kuanza kushuka kufuata ile kamba taratibu,ilimchukua dakika kama kumi kufika chini,baada ya kufika chini mzee John alinyanyua mkono juu na kumuaga mkewe na kamanda.Mkewe na kamanda aliivuta ile kamba harakaharaka na kurudi chumbani kwake ambapo alimkuta kamanda akiwa bado anakoroma.Huku nako mzee John alisimamisha taxi ambayo ili mchukua mpaka bahari.Mzee John alimpa ujira yule mwenye taxi.kisha kufika bahari alitafuta boti ya kwenda Dar es salaam kwa muda kidogo hatimaye akaipata na kuingia tayari kuelekeaDar es saalam.Safari ilichukua karibu saa moja na nusu ambapo waliwalisili Dar es saalam majira ya saa kumi na mbili asubuhi.Mzee John alishuka haraka na kutafuta daladala ya kuelekea kimara.Kwenye lile jumba kamanda aliagiza kwa walinzi wake mzee John alletwe mbele yake na kisha kupigwa risasi na alisema akiwatoroka tu cha moto watakiona.Basi walewalinzi walienda mara chumbani kwa mzee John na kufungua mlango ghafla,wakaangaza huko na huko na kupekua kona zote hawa kumwona mtu wakarudi na kumuarifu kamanda********  


 JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.10

 Kwanza nataka nikufahamishe kwamba sisi tulikuokoa wewe kule baharini ulipokuwa ukikaribia kuzama na tukaamua kukuleta huku kambini maana kuna kazi muhimu tunayotaka wewe ufanye na ukikataa tu mwisho wa maisha yako utakuwa umefika.Sisi tunajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya ,hivyo sisi tutakupa wewe chochote kile utakacho na utakipata ila sisi tunataka wewe kujaza madawa ya kulevya katika pakiti hafu zitapelekwa kwenye mashine tayari kwa kufungwa hatimaye kusafirishwa,haya tuambie basi uko tayari au la?.Mzee John aliinamisha kichwa chini huku akitafakari nimaamuzi gani ayachukue,picha ya mkewe pamoja na mwanae Lulu zilimjia na kumuhimiza kurudi nyumbani kuwasaidia maana wanateseka,Mzee John aliipima kazi aliyokuwa akienda kuifanya akakumbuka jinsi alivyo wahi kujiapiza kwamba hata kaa kujihusisha na madawa ya kulevya lakini upande mwingine bado alihitaji kuiona familia yake.Baada ya tafakuri ya muda wa takribani dakika tano,Mzee John alijibu"niko tayari",boss alicheka"ha...ha....ha" safi sana nenda kapumzike tutaanza kazi. Baada ya miaka mitatu kupita pasipo kumwona mumewe mkewe na mzee John alikata tamaa na kuamini kwamba huenda mumewe alikwisha fariki dunia.Mzee John aliendelea na kazi yake ya kujaza madawa kwenye pakiti ambapo ilimlazimu kujaza pakiti mia tatu kwa siku ambapo alitakiwa kuanza saa kumi na mbili asubuhi mpaka jioni,kwa muda wote aliokuwa kwenye lile jumba hakuwahi kutoka nje hivyo hakujua ni wapi alipo.Siku moja akiwa anaendelea na kazi aliona mlango ukifunguliwa na dada mmoja mweusi wastani mrefu kidogo aliingia ndani kisha kumsalimu mzee John"shikamoo mzee""marahaba""nikusaidiaje?" nataka kukuuliza jitu sijui ukotayari "ulizatu''asante yule dada aliendelea,mimi ni mke wa kamanda kiongozi wa hili kundi ningependa kujua ulifikaje huku maana si eneo zuri hafu nimekuwa nikikuonea huruma sana.Mzee John alieleza kila kitu mpaka yeye kufika pale lakini aliendelea "natamani sana kurudi kuiona familia yangu kwani nilimwacha mke wangu na mtoto mdogo hana hata mwaka hafu sijui wako hai au la,machozi yalimtoka mzee John kisha aliendelea nimeambiwa sitatoka humu ndani hafu sijui niko wapi mimi" pole usilie mzee,alijibu mkewe na kamanda,ki ukweli toka uingie humu mume wangu"kamanda" amekuwa akizungumzia juu ya kukuua kwani anaogopa kwamba utatoa siri kwa kweli kesho ndio siku ya kifo chako ila mimi nataka nikusaidie.Nitashukuru sana alijibu mzee.Sasa kesho saa nane usiku nitakugongea mlango ili kukutorosha.Baada ya maongezi hayo waliachana.Usiku ulipoingia Mzee John hakulala hamu ya kuiona familia yake ilizidi ,ilipotimu saa nane mlango uligongwa,mzee John alifungua haraka na kumwona mkewe na kamanda akiwa amevalia mavazi ya kijeshi,akamwambia nifuate.Safari ya kutoka nje ya jumba ilianza walipandisha ngaz kwa haraka na tahadhari,lakini ghafla wakasikia mlio mkubwa '"paa!!!!!! ********

 

  JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.9.

Haikupita hata dakika mbili mzee John alikuwa amepitiwa na usingizi mzito muda huo ilikuwa ya pata saa kumi na moja jioni .Huku nyuma mkewe na mzee John alibaki akilia kwa uchungu sana huku akimtizama mwanae lulu , aliwaza mengi sana kiasi kwamba mochozi ndo yakawa yanatiririka kama maji . Polisi nao waliendelea na upelelezi wao pasi kupata majibu.Familia za wale wavuvi wawili ziliamua kuomboleza msiba kwaajili ya ndugu zao lakini kwa upande wa mkewe na mzee John hali haikua vile aliendelea kumuomba Mungu ili aweze kumwona tena mume wake kipenzi.Mkewe na mzee John aliamua kulima bustani ya mboga ili aweze kuuza hiyo mboga kisha kujikimu kimaisha hasa ukizingatia kwamba mtoto wake bado mdogo na anahitaji matunzo.Ilikuwa ni asubuhi nyingine tena ambapo mzee John aliamka kisha kufikicha macho na kujinyoosha akaangalia kushoto na kulia, juu na chini kisha kuachwa na bumbuwazi mara baada ya kujiona yupo kwenye chumba kizuri sana cha kifahari chenye malumalu,sofa kubwa la kupumzikia na friji kwa pembeni bila kusahau television akiwa haamini anachokiona mzee John alilinganisha maisha ya nyumbani kwake kimara na pale akaona yuko sehemu ghali sana akiwa bado anawaza mara mlango ulifunguliwa akaingia binti mrembo mithili ya mabinti wa kigogo,akamwambia"habari ya asubuhi" "nzuri" "umeamkaje?" "salama" , yule dada aliendelea, naomba unifuate.Basi mzee John aliondoka na yule dada mpaka mbele ya mlango mmoja,walipofika mlango ulijifungua wakaingia ndani.Mlendani walimoingia ilikuwa ni sebule kubwa na ya kisasa .Mzee John alikaribishwa chai nzito kisha kumaliza walitoka nje ya sebule na kuanza kupandisha ngazi kuelekea juu a mbapo walikutana na mlango mmoja.Yule dada alibisha hodi na mlango ukafunguliwa kisha dada yule alisema"huyu hapa boss" "sawa waweza kwenda" boss alijibu.Dada alitoka nje.Boss alimkaribisha kiti mzee John kisha kumwuliza"waitwa nani wewe na waishi wapi??! "naitwa mzee John naishi kimara" mzee John alijibu.sawasawa kunajambo nyeti nataka kukueleza********
JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.8
Mzee John alikaakimya huku kengele ya hatari ikiendelea kulia kichwani mwake lakini kwa upande mwingine nafsi ilimwambia avute subira kidogo ili aone nini kitafuatia.Safari iliendelea kimyakimya na hatimaye wakafika nchi kavu na baada ya kufika hapo mzee John aliamuriwa kushuka botini haraka sana naye alifanya hivyo bila kuleta ubishi wa aina yoyote.Mara tu baada ya mzee John kushuka kiongozi wakundi aliyejulikana kama kamanda aliamuru "MFUNGENI KITAMBAA USONI" Kitambaa kilifungwa haraka haraka .Baadae kidogo mlio wa gari lililokuwa kasi ulisikika ukikaribia eneo walilokuwepo akina mzee John.Hatimaye gari lilifika eneo walilokuwapo akina mzee John , mzee John alichukuliwa mkukumkuku kisha kutupwa ndani ya gari na kwa kasi gari liliondoshwa.Njiani mzee John alitamani kuuliza ni wapi walikokuwa wanakwenda na kwanini wamemfunga kiasi kile ila yote hayo hayakuwezekana kwani tayari alikuwa amekwisha fungwa kitambaa mdomo hali iliyomfanya kushindwa kutoa sauti.Moyoni mwake aliwaza "hawa watakuwa ni majangili basi hapa lazima nitauawa lakini yote na mwachia Mungu".Gari lilisimama ghafla honi kali ilipigwa "piiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii kisha geti lilisikika likifunguliwa gari lilisimama milango ilifunguliwa,mzee John alichukuliwa mpaka kwenye chumba kimoja kisha kuwekwa humo.Alifunguliwa vitambaa vyote .Kabla mzee John hajaongea lolote mlango wa chumba walimokuwamo ulifunguliwa na kufungwa haraka ambapo aliingia dada mmoja na kuweka chakula mbele ya mzee John kisha amri ilitolewa"MALIZA CHAKULA CHOTE HARAKA" kisha amri hiyo kutolewa mlango ulifunguliwa na wote wakatoka kumwacha mzee John akila chakula.Huyu kamanda ambaye ndio kiongozi wa kundi ambalo linajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya nje na ndani ya nchi.Ilimchukua muda kidogo mzee John kuamua kula kile chakula kwani kuna wakati alihisi labda kinaweza kuwa na sumu lakini tena upande mwingine njaa ilikuwa inamuuma sana,akakatashauri kukila kile chakula na alifanya hivyo ila mara baada ya kula kile chakula mzee John alijikuta akiishiwa nguvu na mwili kulegea akataka kupiga kelele kuomba msaada ********

 JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.7

  mzee akaamua kunyosha mkono juu ili wale waliopo kwenye lile boti waweze kumwona na kumpa msaada.Kisha kufanya hivyo mzee John alijisemea moyoni "kama ni kufa wacha nikafie mbali" akazama tena majini huku akipiga mbizi kuelekea upande ilikokuwa ile meli,pamoja na jitihada zake nguvu nazo hazikuwai tena upande wake kwa kule kutokula chochote kwa muda mrefu na kuogelea umbali mrefu kulimfanya awe mchovu zaidi.Huku kwa wavuvi wenzake na mzee John hali ilikuwanitete kwani wote walikuwa wamekwisha poteza lakini upande walioelekea kulikuwa hakuna msaada wowote ule basi kwa matumaini hafifu na yenye harufu kali ya kifoi waliendelea kupiga mbizi ili kuitafuta nchi kavu.Wale watu waliokuwemo kwenye ile boti walifanikiwa kuona mkono wa mtu kwa mbali ambaye alikuwa akiomba msaada, wakasemezana wao kwa wao kisha kukubali kwenda kumwokoa yule mtu(mzee John).wakaendesha ile boti kwa kasi kubwa kuelekea mahali alipokuwa mzee John walipofika pale mmoja wao,ambaye alikuwa kiongozi wao alitoa amri"zamieni majini haraka kisha mwokoeni huyo" .wale jamaa waliruka haraka na kuingia majini huku wakiangaza huko na kule , baada ya dakika tano hivi kupita mzee John alikwisha okolewa, akiwa anahema kwa tabu sana hali iliyowapelekea wao kumpa huduma ya kwanza kisha kufanya hivyo waligeuza boti lao na kurudi kambini kwao.Wale wenzake na mzee John walijaribu kujiokoa lakini wapi nguvu ziliwaishia taratibu walianza kuelemea huku mmoja wao akinywa maji yale kwa kasi.Lo! maskini mvuvi yule alianza kuzama vivyo hivyo na mwenzake ambae tayari alikuwa amekwisha zama.Baada ya nusu saa maiti mbili zilionekana kuelea juu ya maji ,samaki nao hawakuwa nyuma kwani walishambulia zile maiti na kuacha mafuvu na mifupi vikishuka chini ya maji.Huku nyuma mkewe na mzee John alikwenda kuripoti polisi juu ya kupotea kwa mumewe,polisi wakaanza upelelezi wao mara baada ya kupokea taarifa hizo.Mzee John alipokea huduma ya kwanza iliyomfanya kuanza kujielewa.Baada ya kuangaza macho huku na huko akagundua kuwa yuko kwenye boti huku akiwa amezungukwa na watu asio wajua.Safari ya kuelekea kambini ili endelea hakuna mtu aliyekuwa akiongea chochote hali iliyomfanya mzee John kushituka kidogo akaamua kuuliza"samahani ninyi ni akina nani? akiwa na matumaini ya kupata jibu zuri mara alisikia sauti nzito ilioambatana na ukali"kimya""funga domo lako""
    • JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.6.

  •  ile wimbi liliibetua ile boti kisha kuipindua kabisa basi mzee John na wenzake wakakupwAhuko na kuiacha boti ikielea peke yake.Basi mzee John na wenzake walijitahidi kilammoja kupiga mbizi ili kuikaribia ile boti,kutokana na upepo mkali ile boti ilizidi kwenda karibu na kilindini.Mzee John aliizama na kuibuka huku akijaribu kwenda kwa kasi sana ili awezekulifikia botti,alifanya kuhudi sana na kufanikiwa kulikuta boti ambalo sasa lilikuwa umbali wa mita kama sabini hivi toka pale lilipopindukia basi pasi kukawia mzee John alilikwea lile boti kisha kuliwasha.kila alipojaribu kuliwasha lilikataa kuwaka alijaribu kwa mara ya mwisho huku akirushwa rushwa na mawimbi ya baharini,wale wenzake nao wakaifikia boti mara baada ya kupiga mbizi vya kutosha.walipofika tu wakakutana na taarifa kutoka 8 mara ikawaka wote wakashangila y....e...ssssssss.Safari ya kurudi inchi kavu ilianza tena sasa wakikatika mwendo wa tahadhari,wakiwa bado safarini na huku mvua kubwa ikinyesha mara wakaona samaki mkubwa akijichomoza mbele ya boti yao kisha kuzama.Hilo halikuwatisha sana akina mzee John kwani ni kitu cha kawaida katika bahari ya hindi .Basi waliendelea na safari yao,wakiwa theluthi moja ya safari alitoke samaki mkubwa akaipindua ile boti na kuwatupa mbali akina mzee John na ilikuwa saa kumi na moja kasorobo.kila mmoja alijitahidi kupiga mbizi ili kunusuru maisha yake.Lile boti nalo likazama na huo ndo ukawa mwisho wa boti.Mzee John aliendelea kupiga mbizi huku akijaribu kuangaza huku na huko akijaribu kuomba msaada,Mzee John alianza kuishiwa nguvu huku njaa kali ikiwa imembana,aliendelea kupiga mbizi.Huku nyuma mkewe na mzee John alianza kuingiwa na hofu mara baada ya kuona kwamba mumewe harudi kwani haikuwa mazoea yake kuchelewa kurudi kiasi kile akaamua kuendelea kusubiri zaidi.Ilipofika majira ya saa mbili asubuhi mzee John akiwa hoi bin taabani alikatatamaa na kuamua kusubiri kifo huku hisia kali za kumbukumbu ya mwanae Lulu pamoja na mkewe kumjia kwa machungu yote akawa anaona sasa kwamba mwanzo wa maisha magumu kwa mwanae na mkewe umewadia.Akiwa katika dimbwi zito la mawazo Mzee John akasikia sauti kwa mbali alipo nyanyua kichwa aliona boti ikiwa inaelekea upande wake***********je NINI KITAENDELEA? USIKOSE EPISODE 7!!!!

 

JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.5.

Mzee John na wenzake walichukua ndo zilizokuwamo mle kwenye boti kisha kuanza kutoa maji yaliyokuwamo kwenye boti, walijitahidi kutoa maji haraka haraka ili mradi boti yao isizame.Hiyo botiwanayoitumia ilikuwa ni boti ya kijiji ambayo hukodishwa kwa vikundi mbalimbali vya wavuvi basi na sasa ilikuwa mikononi mwa kundi la akina mzee John.Waliendelea kutoa maji ambayo sasa yalionekana wazi kuanza kupungua.Upepo mkali uliendelea kuvuma kwa kasi zaidi hali8 iliyowapelekea akina mzee John kuendelea kuogopa lakini walijipa moyo kwamba hali hiyo ya upepo ni ya muda mfupi tu.Tayari ilikwisha8 timu saa saba usiku wakiwandani ya bahari mzee John na wenzake walijaribu kutega nyavu zao ili waweze kuambulia chochote,basi walifanya hivyo haraka haraka hukuwakiogopa isije kufika asubuhi wangali bado hawaja pata kitu.shughuli nzima ilimalizika na wao akina mzee John wakatulia botini huku wakiwa wamewasha taa zao ilikuwavuta samaki.Dakika ishirini mbele hali ya hewa ilianza kubadilika taratibu wingu zito lilianza kujikusanya angani.Mzee John alihamaki kuona hali ile lakini wenzake wakamshauri kwamba wasubiri kidogo ili waweze kubahatisha samaki wanakurudi nao nyumbani .Wote wakakatashauri kusubiri kwa muda kidogo.Wakati wakiendelea kusubiri radi nazo zilianza kuunguruma mvululizo hivyo kuzidi kuogopesha,mzee John alipepesa macho kulia kushota,kaskazini kusini na mashariki magharibi bila kuona taa yoyote iliyokuwa ikiwa hivyo kuashiria kwa kulikuwa nakuna wavuvi wengine karibu katika bahari kubwa ya Hindi.Kuona hivyo alishauri waondoke mida hiyo lakini wenzake walionekana kulipinga hilo wazo.Huku wakiendelea kubishana mara mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali ulioshahabiana na radi za kutosha ilanza.Mzee John na wenzake wakaamua kuvuta nyavu zao haraka haraka ilikuangalia kama watakuwa wamepata walau kidogo basi walifanya hivyo na wakahesabu .....moja.....mbili....tatu kisha wakavuta nyavu zao kwa haraka.Lo!!!! walikuwa wameambulia samaki kumi tu.Mvua kubwa iliendelea kunyesha huku upepo nao ukizalisha mawimbi makubwa sana.Mzee John na wenzake wakaanza safari ya kurudi nchi kavu lakini kiisha kwenda umbali wa mita kumi boti ilianza kujaa maji huku mawimbi yakiisukuma sukuma na kutaka kuipindua.Wakaanza tena shughuli ya kutoa maji nje, wakiwa katikati ya shughuli lilikuja wimbi moja kubwa likaibetua ile boti ambayo sasa ikawa ipo wimawima*********

 

JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.4.

Daktari alimsogelea dereva kisha kumgusa sehemu ya moyo na kuinamisha kichwa chake .daktari hakuamini alichokuwa anakishuhudia akaamua kuweka kifaa chake cha kupimia mapigo ya moyo katika sehemu ya usawa wai moyo na kukivaa vizuri masikioni mwake.Loo!!!maskini dereva alikuwa amekwisha aga dunia(kwisha fariki) basi daktari akamwagiza nesi kumfunika marehemu kisha kufanya taratibu za kumpeleka mochwari ,hati ya kifo iliandaliwa na kila la kitu kilikuwa sawa kusubiri taratibu za mazishi. Mzee John pamoja na mkewe walifika nyumbani kwao salama salimi,basi wote kwa pamoja walimshukuru Mungu kwa kuwaepusha na ajali mbaya sana ya gari. Maisha mapya kwa Mzee John yalianza hasa baada ya mwanafamilia mmoja kuongeza.Mzee John alizidisha upendo wake kwa mkewe hata kufikia kumpikia chakula hakika kila mmoja wao alifurahia maisha ya ndoa huku akiomba mwenzake aishi maisha marefu.Baada ya miezi mitatu kupita mkewe na mzee John alirejea katika hali yake ya kawaida yaani alikuwa amepona kabisa,tayari walikwisha mpa jina mtoto wao ambaye sasa anaitwa Lulu.Mzee John alirejea katika shughuli yake ya uvuvi katika bahari ya hindi na siku hiyo ilikuwa ni jumatatu ndipo mzee John alikwenda baharinni na kukutana na wavuvi wenzake walio mtania wakisema"annhaa mzee John naona nyavu zako zimecheuaa...na sasa ka mwaka haka umepata kabinti"hahaha!!! wote walicheka.Baada ya makaribisho hayo yote mzee John aliuliza,jamani kazi zinaenda????!wakamjibu kwa tabu sana.kisha mazungumzo walikubaliana kwamba usiku wataenda kuvua,waliagana na kilammoja akaenda nyumbani kwake kujiandaa na safari ya usiku.Mkewe na mzee John alimsubiri mumewe kwa hamu na mara mzee John alitokea basi mkewe alimuwao kisha akamkaribisha chakula nao wote wakajumuika katika chakula hicho.Ilipofika jioni mzee John alimuaga mkewe tayari kwa safari ya baharini.Majira ya saa mbili usiku wavuvi wote waliingia ndani ya boti yao kuanza safari.Mara walipokaribia kilindi boti ilianza kuyumba kwa kasi huku maji yakiingia ndani hasa sababu ya upepo mkali uliokuwa ukivuma baharini**********

 JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.3. 

Tayari gari lilikuwa limetumbukia mtaroni na watu wa mitaa ya karibu nao hawakuchelewa kuona vile walisogea chapuchapu ili kujaribu kuokoa.Baada ya dakika mbili hivi kupita tayari watu wengi walikuwa wameshajaa kulizunguka gari ili kutaka kujua nini kinaendelea.Basi raia mmoja akashuka chini na kuukaribia mlango wa dereva kisha kuchungulia ndani na kumwona dereva akiwa anavuja damu kwenye paji lake la uso huku akiwa hajitambui.Kuona hivyo akaamua kuita watu wengine ili waweze kumsaidia kumtoa yule dereva kupitia dirisha la lile gari.kisha kumtoa yule dereva yule raia alirudi kwenye gari na kuchungulia kwenye mlango wa katikati na kuona watu kwa mbali alipoangalia vizuri alimwona mwanamke mmoja pamoja na mwanaume wakiwa wameshika katoto kadogo.Basi aliwaita wenzake na kuanza kuwatoa.Mara tu baada ya kutolewa kwenye lile gari mzee John na mkewe waliwashukuru wote kwa kuja kuwaokoa kwani wao walitoka salama , wote wakaongozana mpaka pale alipokuwa amelazwa yule dereva taxi.Wakajaribu kumpima kasi ya mapigo ya moyo wakaona yana piga taratibu sana hivyo ikawalazimu kukodi taxi nyingine ili kumuwahisha yule dereva hospitalini.Mzee John na mkewe walipasika kukodi taxi nyingine mpaka nyumbani kwao kimara.Baada ya yule dereva kufikishwa hospitali manesi wa zamu walipokea haraka haraka na kumpeleka ICU madaktari walianza kumuhudumia.Baada ya masaa mawili dereva aliweza kuzinduka na kujielewa lakini baada ya dakika kumu dereva alilaanza kulalamika kuwa kifua kinambana sana,nesi kuona vile akakimbia kumwita daktari, daktari alipofika alimwona mgonjwa akizidikuishiwa nguvu,daktari akaita « dereva»sauti kwa mbali iljibu«na...a...a..m» daktari akaita tena «dereva»kwa mara hii hakuna sauti iliyosikika ikijibu chochote**********je nini kitaendelea? check out episoe 4!!

 JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.2.

Dkt.Martin aliguna kwa mshangao mara baada ya kuona mapigo ya moyo yakienda kasi yaani presha ilikuwa juu sana,daktari akaamua kuchukua maamuzi ya haraka kwa kumwekea mgonjwa mashine ya kumsaidia kupumua.Madaktari wengine waliendelea kuzuia damu zisiendelee kutoka zaidi na hatimaye walifanikiwa,kazi iliyobaki ilikuwa ni kushusha presha(mapigo ya moyo).Dkt. Martin aliangalia tena kile kipimo kwa umakinizaidi kisha akasema"dah!! tumshukuru Mungu hali yake imewezakutengamaa" mapigo ya moyo yakienda kwa kasi ya kawaida. Jopo zima la madaktari lilimgeukia kichanga aliyezaliwa na kukikuta kikiwa kinalia,hii ilikuwa ni ishara tosha kwamba kichanga kilikuwa hai.Huku nje wasiwasi ulizidikumtawala mzee John kwani muda ulizidikwenda pasipo yeye kupokea majibu yeyote yanayohusu hali ya mkewe,hali iliyompelekea mzee John kuzungukazunguka kwenye benchi aliliokuwa amekalia.Punde kidogo dkt.Martin alitoka nje na kumpahongera mzee John ,alimshukuru sana daktari kwa kazi nzima ya kumuhudumia mkewe na akamwomba aingie kumwona mkewe pamoja na mtoto wake,daktari alimruhusu huku akimsitisizia asikawie kutoka kwani mgonjwa bado anahitaji mapumziko.Pasi kuchelewa mzee John aliingia wodini na kumpahongera mkewe na kukigeukia kichanga chake kwa furaha iliyopitiliza akakibusu "mwaaa".Mzee John alianza kufuatilia ruhusa kwa daktari ili waweze kuondoka siku ile ile.Ilikuwa yapata majira ya saa mbili usiku ndipo walipopata ruhusa ya kurudi nyumbani kwao kimara.Majira ya saa tatu kasorobo( na dakika arobaini na tano) usiku safari ya kuelekea kwao9 ilianza hasa baada ya kukodi taxi toka Lugalo hospitali.Safari ilianza vizuri huku mzee John na mkewe wakifurahia ujio wa mtoto wao mpendwa.Wakiwa njiani kuelekea nyumbani mzee John alimhimiza dereva aongeze mwendo ili wawahi kufika nyumbani,naye dereva bila ubishi alitii kwani alichokuwa anajali yeye ni pesa yake tu.Basi wakiwa ndani ya mwendokasi huo mara taa za mbele za gari zilizimika ghafla na mara dereva alipiga kelele" tunakufaaaaa,kisha mshindo mkubwa ukasikika"paaa" kisha ukimya mkubwa ukatanda****************unataka kujua nini kilifuata? shuka chini katika episode.3!!

 JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide 1 

Ilikuwa ni alhamisi tulivu yenye upepo mwanana huku watu wakiendelea na shughuli za ujenzi wa taifa.Madaktari nao walikuwa bise na taaluma yao ya kuokoa roho za watu.Ndani ya hospitali ya lugalo wagonjwa wengi walifurika huku madakaktari nao wakiendelea kutoa huduma, kama ilivyo ada ndugu wa wagonjwa walikaa nje kusubiri taarifa za maendeleo ya wagonjwa wao, basi hali ilikuwa hivyo kwa mzee John ambaye alikuwa akimngoja mkewe amletee nuru dunia yaani ameletee mwana atakae kuwa mrithi wake wa baadae. Akiwa amejiinamia mzee John aliwaza sana ni namna gani atampenda huyo mtoto wake mpendwa atakae zaliwai ukizingatia kuwa huyo ndie atakae kuwa kifungua mimba chake pasi wazo hilo kuisha jingine la jinsia yai mtoto liliingia la hasha! hilo halikumchanganya sana mzee John kwa alijikuta akisema”yote namwachia Mungu”. Ndani ya hospitali ya Lugalo madaktari waliendelea kumhudumia mkewe na mzee John, hali haikuwai nzuri sana kwa upande mkewe na mzee John kwani alitokwa na damu nyingi sana wakati wa kujifungua hali iliyomfanya Dr.Martin awaambie madaktari wenzake “doctors her condition is get worse she bleed a lot” baada ya kauli hiyo daktari akamwagiza nesi ampeleke mgonjwa chumba cha wagonjwa mahututi( I C U) bila kupoteza wakati mgonjwa alikimbizwa ICU kisha jopo la madaktari watatu kufuata.Juhudi za kunusuru maisha ya mtoto na mama ziliendelea, lakini mara dkt.Martin aligeukia kipimo kilochokuwa kikionyesha mwendo wa mapigo ya moyo ya mgonjwa.oooopssss daktari aliguna kwa mshangao……….

je nini kitaendelea? kesho usikose kuingia somewhere blog ili kujua mwendelezo wa story hii….utamuu ndo huooo umeanza songa nayo episode 2. hapo juu......


 

 

Mtunzi:   Godwill 
                 Sanga
Makazi:  Arusha,      
                Tanzania
Contacts:0756 979566 
               : 0657 35728

 

4 comments: