Tuesday, August 21, 2012

MLELA AMTEMEA MBOVU HEMEDY


Yusuf Mlela (kushoto) akiwa na Hemedy Suleiman ‘PHD’.

KUFUATIA kauli mbovumbovu alizozitoa staa wa filamu na muziki Bongo, Hemedy Suleiman ‘PHD’ kuwa ameshatoka kimapenzi na mastaa 32, swahiba wake katika muvi, Yusuf Mlela amemtemea mbovu na kumtaka awe makini na ajitambue kama yeye kioo cha jamii.
Mlela aliiambia Bongowood kuwa japokuwa kila mtu ana uhuru wa kuzungumza anachotaka lakini Hemedy hakufanya vizuri kutoa kauli kama alizotoa kwani alishawahi kusema atafanya shindano kama la BSS kutafuta mwanamke wa kuoa.

WOLPER, WEMA HII INAWAHUSU


ZARINAH Zaitun Hassan ‘Zari’ ni mwanamuziki, mtangazaji na mfanyabiashara mrembo wa Uganda mwenye umri wa miaka 30, akiwa ni mama wa watoto wawili, aliyeolewa na Ivan Semwanga, utambulisho unatosha.
Katika makala hii, Zari ni mfano mzuri wa kuigwa na mastaa wetu wakiwemo waigizaji wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Masawe na Wema Isaac Sepetu kwani ni wa levo yake kiustaa.
Zari anatajwa kuwa ndiye mwanadada mzuri na mwenye mvuto zaidi Afrika Mashariki ambaye pia anashika namba moja kwa wanawake matajiri wa Uganda, akiongoza kwa kuingiza mshiko mrefu, kumiliki majumba na magari ya kifahari kama yale ya mastaa wa Kimarekani.
Zari amepata mafanikio makubwa  katika muziki na kipindi chake cha The Boss Lady kwenye Runinga ya UBC nchini humo, kinachomuingizia mkwanja mrefu kutokana na matangazo kikifananishwa na kile cha mwanamitindo wa Marekani, Kim Kardashian cha Keep Up With The Kardashians.
 Kwa mujibu wa Jarida la Times la Uganda, huenda Zari akaingia kwenye orodha ya wanawake matajiri zaidi Afrika siku chache zijazo endapo ataendelea kuzichanga.
Zari mwenye maskani yake Kampala na Afrika Kusini, anamiliki ndinga kibao za kisasa na zenye thamani kubwa kama BMW (2006) lenye thamani ya dola 47,000 (Sh. milioni 75.2), Black Chrysler (2008) linalouzwa dola 16,000 (Sh. milioni 25.6) na Audi Q7 (2010) linalogharimu dola 53,000 (Sh. milioni 84.8).
Mengine ni Silver Chrysler (2008) lenye thamani ya dola 13,000 (Sh. milioni 20.8), Jetta Volkswagen (2006) linalogharimu dola 27,000 (Sh. milioni 43.2), Mercedes Benz Convertible (2008) linalouzwa dola 26,000 (Sh. milioni 41.6), Range Rover Sport (2010) lenye thamani ya dola 109,000 (Sh. milioni 174.4), Lamborghini Gallardo (2010) linalogharimu dola 198,000 (Sh. milioni 316.8), Hummer H2 la dola 150,000 (Sh. milioni 240) na mengine mengi, yote yakiwa na jina lake badala ya namba za usajili.
Pia bidada huyo anamiliki maduka, hoteli na majumba ya kisasa kwenye miji mikubwa ya Pretoria na Cape Town nchini Afrika Kusini na Kampala, Uganda.
Lengo langu ni kutoa changamoto kwa mastaa wetu wanaotembelea magari ya kuazima, kukodisha au kuhongwa. Ipo mifano kibwena ya mastaa wa Kibongo wanaoishi kwa mizinga, kuhongwahongwa, ukuwadi lakini wenye mbwembwe na makeke mjini kumbe hawana lolote. Tujifunze kutoka kwa Zari!

MWANAMKE ALIYEUA, AKATAKA KUJIA, SASA ATAUAWA KWA KUPIGWA RISASI


Waokoaji wakishika miguu ya Fi asijirushe ghorofani jijini Zhanjiang, China
Binti wa Fi (wa pili kulia) aliyefika kumlaghai Fi asijiue. Binti huyo alikuwa hajui mama yake alikuwa amemwua mpwaye.
Sheng Fi, akiendelea kushikiliwa asijiue.
Fi akikokotwa kupelekwa kwenye usalama.
 SHENG FI, ni mwanamke anayeishi katika mji wa Zhanjiang, kusini mwa China.  Hivi majuzi, alimwua mtoto (mpwaye) wa wifi yake mwenye umri wa miaka minne na kumtupa kutoka juu ya jengo la ghorofa nne. Hii ni baada ya ugomvi na wifi yake huyo.
Baada ya hapo Fi  naye alitaka kujirusha  kwenda chini, lakini aliokolewa na wafanyakazi wa jengo hilo ambao  walipanga njama za kumzuia kujirusha chini kwa kumwita binti yake aliyekuja kumlaghai kwa maneno kabla hawajamkamata.
Kwa mujibu wa polisi, kwa kitendo hicho, mwanamke huyo atauawa kwa kupigwa risasi baada ya yeye kukiri kumwua mtoto huyo.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, China inashika nafasi ya tisa duniani kwa watu kujiua ambapo wahusika wakuu wa ‘mauaji’ haya makubwa kuliko yote nchini humo ni watu kati ya miaka 15 hadi 34.
Miongoni mwa nchi zinazoongoza duniani kwa kujiua ni Latvia, Kazhakstan na Korea ya Kusini.

DK ULIOMBOKA ATOROSHWA


Haruni Sanchawa na Makongoro Oging'
SIKU chache baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka (pichani), kurejea nchini akitokea Afrika Kusini kwa matibabu, sasa hajulikani alipo.
Taarifa kutoka kwa mmoja wa wanafamilia zinasema kuwa familia hiyo imekuwa ikihofia maisha ya ndugu yao  mara tu baada ya kutua nchini kutoka Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa kutokana na kutekwa na kuumizwa vibaya na hatimaye kutelekezwa katika Msitu wa Mabwepande na watu wasiojulikana, hivyo sasa wamemtorosha nyumbani kwake na kumpeleka wanakojua wao.
 “Alikotoroshewa ni siri ya ndugu na jamaa zake, hawataki kabisa watu wajue,” kilisema chanzo chetu cha habari.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa kutoroshwa kwa Dk Ulimboka kunatokana na hofu waliyokuwa nayo wanafamilia kwa madai kuwa maadui wa ndugu yao wanajua kile walichomfanyia na wanatambua kuwa maadam sasa ana akili timamu, anaweza kuwataja.
Uwazi lilifunga safari hadi Ubungo Kibangu ambako inahisiwa anaweza kupatikana Dk. Ulimboka lakini matokeo yake waandishi wetu walipofika na kuuliza wenyeji wa nyumba iliyotajwa walijibiwa kuwa hayupo na walipotaka kujua yupo wapi, watu hao walisema hawajui.
“Siyo rahisi kumuona Dk Ulimboka ndugu zangu, kila mtu hana imani na mtu anayetaka kuongea na daktari hata baadhi ya ndugu nafasi hiyo hawaipati,” alisema mtu huyo ambaye hakutaka kujitambulisha jina.
Habari zaidi zilidai kuwa baada ya kurejea nchini, Dk Ulimboka alitua kwa Mchungaji Josephat Gwajima kwa ajili ya kuombewa na kumshukuru Mungu kwa madai kuwa alinusurika kifo.
Taarifa zinadai kuwa baada ya kutoka kanisani hapo alienda Bagamoyo ambapo chanzo hicho hakijui alifika huko kwa lengo gani. Waandishi wetu walikwenda kanisani lakini hakuna kiongozi aliyekuwa tayari kumzungumzia Dk Ulimboka kwa madai kuwa msemaji ni Gwajima mwenyewe.
BABA MZAZI
Wiki iliyopita baba mzazi wa Dk Ulimboka alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa hayuko tayari kuongea lolote kuhusu mwanaye na kwamba yote amemwachia Mungu.

Monday, August 20, 2012

WEMA, SNURA WANAFIKI


Wema (kulia) akiwa na Snura.
http://api.ning.com/files/-xhPZ98Kq7naU4FFcReIiALFoGdWOAilKJUB-w9AWqD8WimuhkfJ-5zodXhv2iPTBKUqpP3pBieSWphQctsTvYvNOdfpYg7x/UZINDUZIWAFILAMUYA8.JPG
Wema na Snura.

USHOSTITO wa Wema Sepetu na Snura Mushi uliodumu kwa miezi kadhaa umeraruliwa ukidaiwa kuvunjika kwa kuwa ulikuwa wa kinafiki kutokana na kuvunja kiapo walichokula runingani kuwa hatawaachana, Ijumaa Wikienda limejazwa werawera na wabaya wao.
MTU WA KARIBU ATIRIRIKA
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa mastaa hao, Wema na Snura walikuwa marafiki vinyonga kwani kila mtu alijua muda siyo mrefu watasalitiana na kuanza kuvujisha siri zao na hicho ndicho kilichotokea.
KISA NI NINI?
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Wema alidai kuwa Snura amemsema vibaya kwa ndugu zake na kutangaza kwa wanahabari kuwa amerudiana na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, jambo ambalo lilimchukiza.
Chanzo kilitiririka kuwa baada ya urafiki huo kuvunjika, Wema alimnyang’anya Snura vitu vyote ambavyo alikuwa amemnunulia na kuanzia hapo mawasiliano baina yao yalikatika.
“Snura ameamua kuvunja kile kiapo alichokula runingani kwa machozi, sasa sijui atapata wapi yale mawigi aliyokuwa akipewa na Wema?,” kilihoji chanzo na kuingia mitini.
SNURA ANASEMAJE?
Alifunguka: “Mimi sijui sababu ya urafiki wetu kuvunjika kwa sababu Wema hajaniambia, angekuwa ni mtu mwenye akili na busara angenieleza.”
NYUMBANI KWA WEMA
Ili kupata mzani wa habari hiyo, Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Wema lakini haikupokelewa hivyo likatimba nyumbani kwake ambapo wakiongozwa na Vincent Kigosi ‘Ray’, wasanii hao walitumia nafasi yao kumkashifu mwandishi wetu kwa maneno mabaya yasiyoandikika gazetini, tunayafanyia kazi.

RAY C ATUA BONGO, ASAKA MUME


Rehema Chalamila ‘Ray C’.
MSANII ‘first class’ wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amerejea Bongo na kutangaza kusaka mume huku akiweka wazi vigezo anavyotaka awe navyo, Jelard Lucas anashuka nayo.
Akichonga na Over The Weekend juzikati, Ray C aliyekuwa amejichimbia nchini Kenya, alisema mwanaume atakayeweza kupata penzi lake anatakiwa kuwa na elimu ya kawaida, maendeleo, asiwe mwanamuziki wala pedeshee, awe na mvuto na mwenye kuyajua vizuri malavidavi.
Mwanadada huyo ‘chakaramu’ aliongeza kuwa mwenye sifa hizo akipatikana, atamzalia watoto wawili na kujenga naye familia bora kwani amechoshwa na maisha ya usela.
“Sina mume wala mpenzi, kwa sasa nipo single, ukiniulizia ishu za zamani ntakushangaa kweli, vigezo ndiyo hivyo, kama kuna mtu yupo tayari ajitokeze tufunge ndoa,” alisema Ray C.
Kuhusu kurudi kwenye gemu, Ray C aliwaahidi mashabiki zake kuwa baada ya mfungo kumalizika, yupo kwenye harakati za kuzindua albamu yake mpya aliyoipa jina la ‘Moyo Waniuma’ yenye nyimbo 10.
Aliongeza kuwa soko la muziki Bongo ni bovu sana ukilinganisha na Kenya hivyo bado mishemishe zake nyingi atakuwa akizifanyia nchini humo

Friday, August 17, 2012

Ferdinand atozwa faini


Rio Ferdinand
Beki wa Manchester United Rio Ferdinand ametozwa faini ya pauni za Uingereza 45,000 sawa na dola za kimarekani $71,000 na chama cha mpira cha England baada ya kupatikana na hatia ya kutumia lugha mbovu kuhusu beki wa Chelsea Ashley Cole.
Halmashauri huru imempata na hatia kwa kumkashifu Cole akitumia lugha inayopdhalilisha ukoo na kabila la mpinzani kwa msemo wa maneno 'Choc ice' kwa maana mtu mweusi nje na ndani mzungu.
Ferdinand alikanusha kua sivyo hivyo ila ni kwamba maanake ni mtu feki, au mnafiki.
Ashley Cole
Matamshi yaliyopeperushwa kwa mtandao wa Twitter yalitokea baada ya Ashley Cole kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya mdogo wake Rio aliyedai kua alitukanwa na John Terry. Terry hakupatikana na hatia.

Wachimba migodi 30 wapigwa risasi


Polisi wawafyatulia risasi wachimba mgodi
Zaidi ya watu 30 wauwawa katika makabiliano kati ya polisi na wachimba migodi wanaogoma Afrika kusini.
Waziri wa Polisi wa Afrika kusini amesema maafa hayo yalitokea siku ya Alhamisi katika mgodi wa Marikana.
Polisi walifyatua risasi baada ya kushindwa kuwatawanya wagomaji hao waliokuwa wamejihami kwa marungu na mapanga.
Mgodi huo wa dhahabu nyeupe unaomilikiwa na kampuni ya Lonmin imekuwa ni sehemu ya mapigano makali kuhusu mzozo wa malipo uliotokana na uhasama kati ya vyama viwili vya wafanyakazi.
Kisa hicho cha polisi ni moja wapo wa operesheni mbaya zaidi ya polisi tangu kumalizika kwa enzi za ubaguzi wa rangi.
Awali machafuko hayo yalioanza wiki iliyopita yalikuwa yamesababisha vifo vya watu 10 na polisi wawili.
Siku ya Ijumaa waziri wa Polisi ,Nathi Mthethwa akizungumza na kituo kimoja cha Radio alithibitisha kuwa watu wengi walijeruhiwa na wengine kuuwawa.
Chama kikuu cha wachimba migodi, National Union of Mineworkers ,kinasema idadi ya waliofariki ni 36.
Polisi walikuwa wamepelekwa kwenda kuwatawanya wachimba migodi wapatao 3,000 ambao walikuwa wamekusanyika eneo la mlima mkabala na mgodi wa Marikana, ambao uko kilomita 100 kaskazini mangharibi mwa Johannesburg.
Wafanyakzi hao walikuwa wanataka nyongeza ya mshahara ya dola $1,000 kila mwezi.
Mazingira yaliofanya polisi waanze kufyatua risasi bado haijajulikana , lakini taarifa kutoka kwa walioshuhudia zinasema mauji hayo yalitokea wakati kundi la waandamani walipojaribu kuwavamia polisi.
Hapo ndipo polisi waliokuwa wamejihami kwa bunduki na bastola wakaanza kufyatua risasi.

Waziri Mkuu Uganda adukuliwa


Mtandao wa Waziri Mkuu wa Uganda
Afisa mmoja wa serikali ya Uganda amethibitisha kwamba mtandao wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo umeshambuliwa na wadukuzi.
Sasa mtandao huo unaonyesha picha na ujumbe kutoka kwa wanaharakati wa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.
Katika moja wapo ya ujumbe huyo, wadukuzu wameweka ujumbe kuonyesha kuwa Waziri Mkuu wa Uganda anaomba mashoga radhi kwamba eti sasa anaunga mkono maandamano ya watu hao wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.
Mapenzi ya jinsi moja ni hatia nchini Uganda na wengi ya wanaoshukiwa kuwa miongoni mwao wamekuwa wakishambuliwa na hata kutelekezwa na jamii.
Mapema mwaka huu , hoja ya kutaka sheria ibadilishwe na kuongoze adhabu kwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja kutoka miaka 14 hadi kifungo cha maisha iliwasilishwa kwa mara nyegine bungeni.
Awali sheria iliyopendekezwa ilikuwa inasema kwamba yeyote atakaye patikana na hatia ya kufanya mapenzi ya jinsia moja na mtoto au mlemavu au mtu anayefanya hivyo akiwa na ukimwi ,basi adhabu yake ni kunyongwa.
Mtandao wa kitengo cha sheria na uadilifu nchini Uganda pia unasemekana wiki hii ulidukuliwa.
Lakini kamishena wa habari na Teknolojia Bwana Ambrose Ruyooka,aliambia BBC kuwa tatizo hilo limerekebishwa.
Serikali ya Uganda imenzisha sheria kali ya tovuti na mtandano ilikukabiliana na ufalifu wa mtandao.
Inandaiwa kuwa mwanaharakati ajayejiita @DramaSett3r katika Twitter, ndiye anayehusika na udukuzi huo.

Soma Alichoandika Sinta Kuhusu Wao Kuombana Msamaha na Agness Masogange Baada ya Picha za Utupu za Agness Kuvuja


Agness Masongange


"Sipendi uchonganishi jamani?? huyu dada alishaniomba msamaha na mimi na yeye tunaongea vizuri,,kama mtu anawashwa na yake kupitia funny blogs tafuten la kuandika

Wale mliokuwa mnaniongelea kwa Agnes  kaniambia yote nawaangalia tu, mimi simjui Agnes ila nikiona mtu kafanya makosa namsahihisha ndo mana alikuja kuniomba msamaha na sina kinyongo naye

Nimemsamehe sasa maneno mengine mnayatoa wapi? kama mtu ana picha zangu za ngono zitoeni jamani kwanini mnanitishia??haaaaa nimeshatoka huko kitambooo sana lolest,,labda mtengeneze na za kutengeneza tunazijua hivihivi mtasubiri sana tena sana ninajiamini 100%Agnes alinieleza mkanda mzima wa yaliyomtokea na nikaona wasichana wanadhalilishwa sana ktkana na pombe
Jamani yale maisha ya twendeni tukamnywe mbona yamepita? so msiendelezee maneno yenu ya ajabu mimi na Agnes tunaongea tena siku ile ile ndo maana nilifuta posts  na nimemsema sana nadhani ameanza kunisikiliza na akinisikiliza atafika mbali maana ni binti mzuri so mnaopenda watu wagombane poyeeeeeee,, mmeshushukaje??tafuteni mwingine kwangu ni fulllll stooooooop,, Agnes nakwambia hapa mbele ya watu huna marafiki ni wanafiki wao ndio wamenitumia video kwa mda wako uje nikuonyeshe waumbuke  na munch status zako zote walituma

 ONYO KWA MADADA

UWE NA HUBBY WAKO US SIJUI UK NA NCHI NYINGINE USIPIGE PICHA ZA UCHI UKAMTUMIA WANAUME SI WATU NA KWANZA SIKU HIZI MAISHA YA KUAMINIANA YAPO WAPI? " Says Sinta

Prezzo "World of opportunities ahead of me Stargame is no chip off my shoulder"
Kenyan rapper Prezzo’s near win at the just concluded Big Brother Africa Stargame is no chip off his shoulder, because according to him he has a world of opportunities ahead of him.
At a press conference in Nairobi Thursday a day after his return, the rapper revealed that though he thought the Stargame was his to take after Zimbabwean contestant Lady May’s exit, he has since understood that it was in South African Keagan’s ‘destiny to have won’ the Sh25m grand prize.
“To me Lady May was the competition. Because seeing her in the house, she was playing to the camera all the time. She had devised a game plan and was executing it. She was like a tortoise, always hiding under the shell and so I felt that she was a threat,” he said.
Wearing a glossy black shirt, sleek black pants and a golden chain dangling over several tattoos, Prezzo gloried over his recent appointment as ONE campaign ambassador against hunger.
“The campaign is looking at designing t-shirts with a slogan that I came up with ‘Swagger Farmer’ but they’re yet to send an email with details on what they want me to do,” he told Capital Lifestyle.
“I’m very excited about that project because it’s about giving back to society,” he beamed.
With his mother looking on, Prezzo revealed he was pleased that Goldie’s affections for him were genuine and stated that he was looking forward to inviting her to Kenya.
Other than striking it up with Goldie, Prezzo is hoping to pursue some acting and even politics as he goes on with the business of music and being a celebrity.

Huu ndio Utajiri wa Magari Alio na Zari Hassan Mwanamke Mrembo Kuzidi Wote Uganda
Zari Akiwa na Lambogin 


Zari Hassani Akiwa Na Benzi Yake

Yay! Omotola gets verified on Twitter!


  
Now, that's a superstar!

Ronaldo, Messi, Iniesta nominated for 2012 UEFA best player awardCristiano Ronaldo (Portugal, Real Madrid CF) Lionel Messi (Argentina, FC Barcelona) and Andres Iniesta (Spain, FC Barcelona) have been shortlisted by UEFA for the 2011/12 best player in Europe award.
The three Spain-based players came top of a poll of 53 journalists from UEFA's member associations. Andrea Pirlo of Juventus finished fourth, while Barcelona's Xavi came in fifth.

Messi won this award last year. Who do you think should win it this year? I think Ronaldo should, he was quite outstanding at the 2012 Euro Cup.

RIPOTI KAMILI MKE KUTEKETEA KWA MOTO NDANI YA GARITUKIO la mwanamke Rehema Nungu kukutwa ameteketea kwa moto ndani ya gari aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili T 883 BLA katika msitu wa Mabwepande, jijini Dar Agosti 1, 2012 linazidi kugusa akili za wengi hasa kutokana na utata wa tukio lenyewe na hii ndiyo ripoti kamili.
Taarifa zilizopenyezwa na ndugu mmoja wa Simon Sakilu ambaye ni mume wa marehemu, zinadai kuwa kabla ya tukio hilo, Rehema na mumewe walikuwa kwenye ugomvi mzito usiokuwa na dalili ya kumalizika.
MAELEZO YA UPANDE WA MWANAUME
Habari zinadai kwamba marehemu alikuwa akidaiwa fedha na mfanyabiashara mmoja (hakutajwa jina) lakini mumewe hakulijua deni hilo mpaka siku za mwisho za uhai wa Rehema ambapo hata hivyo hakumuuliza.
Aidha, ikadaiwa kwamba mfanyabiashara huyo alikuwa akimdai marehemu kwa vitisho kwamba asipolipa atamwambia mumewe, jambo ambalo mwanamke huyo hakutaka litokee.
Siku ya tukio, habari zinadai kuwa marehemu aliamka mapema na kufanya shughuli za nyumbani na baada ya muda inadaiwa alikunywa sumu ambayo haikujulikana ni ya aina gani.
Ikazidi kudaiwa kuwa baada ya kitendo hicho, mumewe alifanya juhudi za kumnywesha  maziwa ili kuokoa uhai wake lakini ilishindikana kufuatia mke kumzidi nguvu mumewe na kukimbilia kwenye gari na kuondoka nyumbani kwenda kusikojulikana.
 “Mwanamke alipokunywa sumu, mumewe (Simon)alifanya juhudi za kumpa maziwa ili kuokoa maisha yake lakini alizidiwa nguvu, mke akatoka na gari na kwenda kusikojulikana.
“Simon alikwenda kukutana na mdai wa mkewe na kumlipa fedha zake akiamini mkewe alikunywa sumu kwa sababu ya deni, baada ya malipo akampigia simu mkewe ili kumtaarifu lakini simu hiyo ilikuwa inaita na kukatika, baadaye haikupatikana kabisa,” alisema ndugu huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake gazetini.
Kuanzia hapo, ndugu walianza kumsaka Rehema mpaka Agosti 2 mwaka huu habari zilipopatikana habari  kwamba kuna gari limekutwa limeteketea kwa moto kwenye msitu wa Mabwepande. Mtu aliyedaiwa ndiye alikuwa dereva naye alikuwa ameungua na kubaki majivu na fuvu likiwa sehemu ya kiti.
Hata hivyo, ndugu hawakutaka kuweka msiba wakiamini aliyefariki dunia kwa moto huo anaweza asiwe Rehema. Ili kujiridhisha na hilo, walichukua mabaki hayo na kuyapeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa vipimo vya DNA.

MUME ANA SIRI NZITO?

Habari zaidi kutoka ndani ya familia hiyo zinadai kuwa huenda Simon ana siri nzito juu ya kifo cha mkewe Rehema kwani haingii akilini mume kuzidiwa nguvu na mkewe wakati wa kumsaidia kumnywesha maziwa.
Aidha, mpenyesha habari huyo aliendelea kufunguka kwamba ilikuwa ni kawaida kwa wanandoa hao kutibuana na mke kwenda anakojua hata kwa siku tatu bila mwanaume kujishughulisha kumtafuta.

MAELEZO UPANDE WA MKE

Agosti 6, 2012  mapaparazi wetu walifika nyumbani kwa marehemu Rehema, Mbezi Beach, Dar na kukuta watu wachache ikidaiwa hali hiyo ilitokana na wengi kutoamini kama Rehema alifariki dunia. Mume wa marehemu hakuwepo msibani hapo bila kujulikana alikokwenda.
Alipotafutwa ndugu wa marehemu kuzungumzia suala hilo, kila mmoja aliruka na kudai mwenye uwezo wa kuzungumzia jambo hilo ni mama mzazi ambaye naye aligoma kusema lolote.
“Mwenye uwezo wa kuzungumzia suala hilo ni mama mzazi lakini amegoma kwa madai kuwa hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa vile  anahisi kuna mchezo mchafu umefanyika,” alisema ndugu mmoja.
Hata hivyo, mtu mmoja wa karibu na familia ya marehemu alisema kuwa habari kamili juu ya msiba huo zitapatikana mara baada ya kupata vipimo kutoka kwa mkemia mkuu kubaini kama kweli aliyekutwa ameteketea kwa moto ndani ya gari ni Rehema.
“Ni vigumu kulizungumzia suala hili kwani linatatanisha, unaweza kusema aliyekufa ni Rehema na matokeo ya mkemia mkuu yakitoka yakaonesha tofauti, inaweza kuleta shida, tusubiri majibu kwanza,” alisema mtu huyo bila kutaja jina lake.

MAJIBU YA MKEMIA MKUU YATOKA

Agosti 10, 2012 mmoja wa ndugu wa marehemu alimpigia simu mwanahabari wetu na kumweleza kuwa majibu ya Mkemia Mkuu wa Serikali yametoka na kubaini kwamba aliyekufa ni Rehema Nungu.
“Kama unavyosikia vilio hivyo, nipo msibani, majibu ya mkemia mkuu yamebaini aliyekufa ni Rehema Nungu, taratibu za mazishi zinafanywa sasa ila naomba muende nyumbani kwa Simon mtapata habari kamili,” alisema ndugu huyo na kusisitiza kuwa kama msiba utafanyika kwa mume wa marehemu, hawatakwenda ila watakwenda makaburini tu.

NYUMBANI KWA SIMON

Baada ya kupata taarifa hizo, waandishi wetu walifika nyumbani kwa Simon, Tegeta Nyuki, Dar na kumkuta msemaji wa familia hiyo aliyejulikana kwa jina moja la Dedu.
Dedu alipopewa pole ya msiba na kutakiwa kueleza sababu za kifo cha marehemu, alisema waulizwe polisi yeye hawezi kusema chochote licha ya kukutwa na picha ya marehemu mkononi.
“Siwezi kusema chochote, kamuoneni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ana habari zote za msiba huu, naomba mniache niendelee na taratibu za hapa,” alisema Dedu.

HUYU HAPA KAMANDA WA MKOA WA PWANI

Agosti 10, 2012 mwandishi wetu alitinga katika ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu kwa lengo la kujua chochote kuhusu kifo cha mwanamke huyo lakini hakuwepo, ikabidi apigiwe simu yake ya kiganjani ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli majibu ya tukio hilo yametoka, mtu aliyeteketea kwa moto ndani ya gari ni Rehema lakini sipo katika nafasi nzuri ya kuongea kwani niko Muhimbili nashughulikia majeruhi wa ajali ya wanakwaya wa kutoka Kenya.
“Hata kesho (Agosti 11) sitakuwa ofisini kwani nitakuwa bado nashughulikia suala hilo, waliofariki ni raia wa nje hivyo ni vyema nikahakikisha wanasafirishwa kurudi kwao,” alisema Kamanda Mangu.

UTATA

Asubuhi ya Agosti 11, 2012, wanahabari wetu walidamkia nyumbani kwa Simon ili kutaka kujua taratibu za mazishi.
Nje ya nyumba alikuwepo Dedu na mzee mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake, akasema yeye ni makamu mwenyekiti wa kamati ya mazishi. Wawili hao waligoma kuongea chochote kwa madai yaleyale, suala liko polisi.
Hata hivyo, muda huohuo simu ya Dedu iliita, alipopokea ilionekana kupigwa na ndugu mmoja wa marehemu ambaye alisema mazishi ya mabaki ya mwili wa Rehema (fuvu na majivu) yangefanyika Jumamosi au Jumapili iliyopita lakini baada ya kupata kibali kutoka kwa mkemia mkuu.
Baadaye habari kutoka ndani ya familia ya Rehema zilisema kibali cha kuzika masalia ya mwili wa marehemu kilikuwa kipatikane jana Jumatatu.
Marehemu Rehema ameacha watoto wawili, Ngimba na Muheri.

MUME: MKE WANGU KANIIBIA NYETIUNAWEZA usiamini lakini ukweli ni kuwa Juma Ali (48), mkazi wa Mtoni jijini Dar es Salaam amedai kwamba mkewe, Hadija Chande (40) (pichani) amemchezea kishirikina, hivyo kujikuta hana nyeti ya kiume.
Taarifa kutoka katika vyanzo vyetu vya habari zimedai kwamba Ali kwa sasa hana uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa kuwa nyeti yake imetoweka kimiujiza na shutuma zote anambebesha mkewe kwamba ndiye aliyefanya ‘mchezo’ huo.
Habari zinadai kuwa kutokana na hilo, kumezuka mgogoro mkubwa kati ya wanandoa hao kwani mume amekuwa akimdai mkewe  arejeshe nyeti yake, jambo ambalo halijawezekana.
Imedaiwa kuwa Hadija, mara baada ya kufunga ndoa na Ali mwaka 1996 alikuwa na wivu wa kupindukia, hivyo kuamua kutafuta dawa na kumfanyia mumewe ili ndoa yao izidi kuimarika lakini mara baada ya kutenda alichoambiwa afanye kama dawa, nyeti ilitoweka na kubaki na ‘kipande’ kidogo cha kusaidia kutoa haja ndogo.
“Kutokana na madai ya Ali, mkewe aliamua kufungasha virago na kutoweka nyumbani na kwenda kusikojulikana wakati mumewe yupo kazini,” kilisema chanzo.
Gazeti hili baada ya kusikia habari hizo za kushangaza, lilimtafuta Ali ambaye baada ya kuulizwa kuhusu mkasa huo alititirisha maneno kama ifuatavyo:
“Ni kweli hayo uliyoambiwa. Kwa sasa ninachomdai mke wangu aliyetoweka ni nyeti yangu, naomba anirudishie kwani ufumbuzi wa mgogoro wetu hauwezi kupatikana kamwe kama hatazirudisha.
“Hapa unaponiona ndugu mwandishi mimi siyo mwanaume tena. Sina ‘kitu’, hapa kimebaki ‘ kipande’ kama kalamu ambayo haifanyi kazi yoyote. Mke wangu nilipomuoa alinikuta nina watoto sita niliozaa na mke niliyemuacha mwaka 1994, sasa hivi siwezi kufanya tendo la ndoa.
“Mgogoro wa kutoweka na nyeti yangu ulianzia mke wangu alipoanza kunilalamikia kuwa natembea nje ya ndoa na akaniahidi kuwa ni lazima atanidhibiti. Madai yake niliyapinga lakini nguo zangu za ndani zikaanza kupotea. Nilipomuuliza alisema angeninunulia nyingine, nilikuwa na mashaka naye, nikamuomba anirudishie lakini hakufanya hivyo.
“Mara tu chupi zangu zilipoanza kupotea, nikawa sisikii hamu ya tendo la ndoa. Mwezi uliopita, nyeti yangu ikawa imetoweka, nilipomuuliza akawa mbogo. Ilipofika Julai 28, mwaka huu, saa sita mchana, nilitoka kazini na kurudi nyumbani lakini sikumkuta mke wangu na nguo zangu za ndani na soksi hazikuwepo pia.
“Licha ya nguo, picha zangu nazo alizichukua na nilipomuuliza mtoto wangu Karim akasema mama yao amesema kabeba vitu vyake vyote ndani ya nyumba na hakumuambia anakokwenda.
“Nilikaa siku tatu, nikaamua kwenda serikali ya mtaa wetu ya Mtoni na wakanishauri nikaripoti polisi ambako nilipokwenda walifungua jalada namba namba MTG/RB/2054/2012. Polisi waliniambia nitakapomuona popote niwaarifu ili wamkamate.
“Nilisafiri kwenda mikoani na niliporudi nilikuta barua kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) wilayani Temeke ikinitaka niende katika ofisi zao kwa kuwa mke wangu kafungua shauri la kutaka talaka, jambo nililogundua kuwa alishauriwa na rafiki zake ili nimpe nyumba.
“Najua kilichomtoa mke wangu nyumbani ni kushindwa kunirejeshea nyeti yangu, hapa ameshaniua hivyo siyo rahisi kwake kurudi kwani hatafurahia tendo la ndoa. Ili kesi hii iishe sharti ni moja tu kwamba anirudishie nyeti yangu,” alisema Ali.
Mke wa Ali, Hadija alipohojiwa kuhusu sakata hilo alikuwa na haya ya kusema:
“Mbona na mimi sizai na sina hata mtoto wa dawa? Kuhusu kwamba nimetoweka na nyeti yake ni kwamba mimi sijui mambo hayo, asinifuatefuate.”
Mjomba wa Hadija, Abdalah Chande alipoulizwa kuhusu sakata hilo, alikiri kuelezwa na Ali kuhusu mgogoro huo na kudai kuwa alimzushia kuwa yeye ndiye anayemharibu mpwae (Hadija) na akampiga marufuku kukanyaga nyumbani kwake, akaahidi kushirikiana na baba yake mdogo kutatua tatizo hilo.
Baba mdogo wa Hadija  aliyejitambulisha kwa jina moja la Juma alipoulizwa kuhusu mgogoro huo alisema hautambui lakini alimlaumu mwanaye huyo kwa kupeleka shauri hilo Bakwata kabla ya kulifikisha kwake.

  

MWANAFUNZI ABAKWA, ANYONGWA, AZIKWA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Bw. Zelothe Sephen.
MWANAFUNZI wa darasa la saba Shule ya Msingi Hogolo, wa umri wa miaka 14 (jina limehifadhiwa) ambaye ni Mkazi wa Mtaa wa Ikulu Kijiji cha Hogolo wilayani Kongwa, mkoani Dodoma ameuawa kwa kunyongwa na kuzikwa kwenye shimo nyuma ya nyumba yao karibu na choo baada ya kubakwa.
Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha mauaji hayo yaliyofanyika Jumamosi iliyopita ni wivu wa kimapenzi kwani marehemu enzi za uhai wake, anadaiwa alikuwa amevunja uhusiano na mpenzi wake wa muda mrefu, Heri Aboubakar na kuanzisha uhusiano mpya na Wilfredy Muhaha maarufu Kabo.
Hata hivyo bado haijafahamika muuaji halisi wa marehemu huyo licha ya polisi kuwashikilia watu kadhaa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo akiwemo mpenzi wake wa sasa, Muhaha.
Mbali na Muhaha wengine wanaoshikiliwa Polisi ni Ashad Jafari ambaye ni mkulima na mkazi wa Mtaa wa Nyerere Hogolo ambaye ni rafiki wa marehemu na Rino Mazoea, mkulima na mkazi wa Ikulu Hogolo wilayani Kongwa ambaye ni kaka wa marehemu.
Kamanda Zelothe Steven alisema wanamtafuta Aboubakar ambaye amekimbia kijijini hapo na hajulikani alipo mpaka sasa. Katika tukio hilo, kaka wa marehemu ambaye pia anashikiliwa Polisi, katika maelezo yake ya awali alidai kusikia purukushani zikitokea usiku wa tukio hilo la mauaji lakini hakutoka usiku huo kushuhudia nini kinaendelea.
Marehemu alikuwa akiishi na babu na bibi yake hapo kijijini na siku ya tukio , walezi hao, walikuwa wameondoka kwenda katika vijiji vya jirani, ambapo bibi yake alikuwa amekwenda Kongwa kwa ajili ya kujengea makaburi na babu yake alikwenda Kijiji cha Banyi Banyi kutembelea wagonjwa.

What! Kanye West calls Kim K 'Bitch' while 50cent labels her 'Trash'!Does a man always have to trash his rival's girlfriend or wife to get to him? Ok, we all know Kanye called his girlfriend, Kim K, 'perfect bitch' but does that give 50cent the audacity to term her Trash? *Just asking oh*. Really, the Kadashians are not my favourite TV personalities but then, they're doing their thing and gaining popularity not to talk of making some good money from it.

According to mailonline:
50 Cent hit rival Kanye West below the belt by branding his girlfriend Kim Kardashian 'trash'.
The Get Rich or Die Tryin' star has surely kicked off a new feud with his old sparring partner with his latest comments.
He told XXL Magazine: 'You know how it is? One man’s trash is another man’s treasure.'
The 37-year-old New Yorker made the quip as he shared his thoughts on the The College Dropout's touching ode to his lover, the charmingly titled Perfect Bitch.

He said: 'I mean, if that man feel like she's perfect, then she’s perfect.
'He could mean it and you’ll end up singing the words to it because he’s Kanye.'
But he also issued a note of caution, pointing out his doubts that there is such a thing as the perfect woman.
The In Da Club favourite said: 'I’m not sure. The smartest guys I know have lost being a bad judge of character in that area.'
50 Cent has been a rival of Kanye's throughout his career, and in 2007 he infamously promised to quit music if his Curtis album was outsold by West's platter Graduation.
Of course the latter went on to top the charts after selling 957,000 copies in the first week, while 50 took the number two spot, selling 691,000 units.
Despite his previous assertions, 50 Cent went on to release Before I Self Destruct in 2009

DJ Khaled - I Wish You Would / Cold ft. Kanye West & Rick Ross (Official...

ALAWI JUNIOR - NAKUPENDA WEWE( BONGO FLAVA-RADIO MBAO)

Hii ndio Video ya Alawi Junior Iliyofanywa Nyumbani Kwa Wema Sepetu

TANZANIA BONGO FLAVA - DIAMOND - MAWAZO

TANZANIA BONGO FLAVA - DIAMOND - MAWAZO

Barack Obama Ana Kiwanda Cha Bia ndani ya White House


Source: http://leotainment.blogspot.com/
Kuongoza nchi kubwa kama Marekani yataka moyo! Ndio maana Barack Obama aliamua kuwa na kiwanda cha bia kwenye ikulu ya White House ili kupunguza stress za cheo hicho kikubwa duniani. Isitoshe kipindi hiki ni kigumu kwake kwakuwa anaelekea kwenye uchaguzi, so kupiga mtungi si jambo la kushangaza kwake.
 Amekuwa rais wa kwanza wa hivi karibuni nchini Marekani kunywa bia inayotengezwa kwenye Ikulu.


Bia inayotengenezwa humo imepewa jina la ‘White House Honey Ale’ ikiwa na rangi mbalimbali.

Asali kidogo inayopatikana kwenye bia hiyo inatoka kwenye mizinga ya nyuki anayofuga mkewe Michelle Obama kwenye bustani yao
.

MMOJA AUAWA, MWINGINE ANUSURIKA KWA TUHUMA ZA KUIBA PIKIPIKI MKOANI MORO


Kijana aliyenusurika akiwa hoi baada ya kipigo kutoka kwa wananchi.
...Kijana huyo akiwa mikononi mwa wananchi.
Vijana hao wawili waliosadikiwa kuwa vibaka wakiwa kwenye gari la polisi.
Pikipiki inayodaiwa kuibiwa na vijana hao.
KIJANA mmoja ameuawa wakati mwenzake anayesadikiwa kuwa ni Ustadh kwa mavazi aliyokuwa amevaa, akinusurika kuuawa baada ya kutuhumiwa kuiba baiskeli eneo ya Kihonda mkoani Morogoro jana jioni. Kwa mujibu wa jeshi la Polisi, mtuhumiwa huyo aliye hai amelazwa katika hospitali ya Rufaa mkoani hapa kwa matibabu.

NISHA ALINADI PENZI JIPYA


Salma Jabu ‘Nisha’.
SIKU chache baada ya kutangazwa kuwa amemwagana na mpenzi wake Godfrey,  mcheza sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ameibuka na kujinadi kuwa amepata kifaa kipya.
Kupitia akaunti yake ya Facebook, Nisha alibainisha kuwa tayari yupo ndani ya himaya mpya ya mapenzi ingawa pia bado hawezi kuiweka hadharani kwa sababu ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.
“Love him to death…Oh God im in loooove. Ah baada ya muda mrefu kuumia..” ameandika Nisha mtandaoni na kupongezwa na wadau wake.

NORA AWABWATUKIA MASTAA WA KIKE BONGO


Nuru Nassoro ‘Nora’.

MSANII wa filamu za Kibongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ amewabwatukia wasanii wa kike wanaoendekeza tamaa ya fedha na kuharibu tasnia nzima ya uigizaji.
Akichezesha taya na Tollywood Newz hivi karibuni, Nora alisema anaumizwa sana na wasanii ambao hawana msimamo wanaofanya sanaa ya uigizaji kuwa ni sehemu ya kuuzia sura jambo ambalo linaweza kuifanya hata serikali kushindwa kuisaidia sanaa hiyo kutokana na skendo za mara kwa mara zinazowakumba wasanii.
Aidha, alisema wasanii wa kike wanatakiwa kujitambua na kuachana na kujichanganya na mambo yanayowaharibia sifa katika jamii kwani wana nafasi kubwa ya kuitangaza sanaa nje ya nchi kama ilivyofanywa na marehemu, Steven Kanumba.
“Huwa inaniuma sana kuona wasanii wa kike wanavyokuwa na skendo nyingi kuliko kufanya kazi, kwa nini wasiachane na mambo hayo ya hovyo na kujikita katika kazi?
“Lakini kwa upande mwingine hata waandaaji wa filamu wanachangia kwani wakimuona msichana ana sura nzuri au umbile zuri wanamchukua hawajui kwamba kuigiza ni kipaji, matokeo yake ndiyo haya, wanafanya uigizaji ni sehemu ya kuuza sura”, alisema Nora.

Yahoo Axis: A Complete New Web Browser


Logo


 Internet browsers have recently gained considerable limelight as the world is becoming online. Now when physical businesses are turning into the virtual ones and new online methods to make money are productive enough to facilitate the talent across the globe, the competition among the internet browsers is inevitable. We saw that gradually yahoo maintained its pace and somehow has overpowered hotmail when it comes to search engines, it was expected that yahoo will soon come up with its own internet browser as MSN enjoys internet Explorer (thanks to Microsoft) , and the youngest competitor Google that came up with Google Chrome. Realizing the importance of launching a new browser with its tag, Yahoo released its browser, Yahoo! Axis, few months back.
 What’s different?
It is true that the upcoming decades are all about embedded devices. Yahoo is lucky enough to take this step at this stage, grabbing huge attention due to its innovative new mobile browser and desktop plug-in that gives visual search results to people. This works like a magic where people find a new, direct way to choose what they were searching for.
Not only this, but Axis is now available for our Apple iOS devices, (get one from here) apart from its major, HTML5 enabled desktop browser to enjoy a new change in your life which is worth adopting.
Its Features
Yahoo! Axis offers some exceptional features that are solely responsible for its big success in no time. When you choose Axis as your web browser, you are actually said yes to equipped handy features that unify searching and browsing. 
As stated above, the visual search has simply made the back button obsolete. Not only this, but axis also offers a personalized homepage that contains your most recently visited sites along with your bookmarks and the sites you are actually following.
Yahoo Axis On Your Desktop
The best part about Yahoo Axis is, it is easy to install with user friendly layout. You can download the desktop browser from Axis website and get the plug-in for your current browser.
Yahoo axis for desktop
After installation, a black search bar will appear bellow the browser window. Typing in this search bar will scroll down the visual thumbnails of the appropriate results from where you can choose the right option, saving your time.
If you are a busy person and a socialite who wants to keep a track of everything happening at all ends, then Axis is the best choice. Once you signed in with your Yahoo, Facebook or Google account, you can set your favorites and can make your access much quick to your pages.
Yahoo Axis On Your iPhone and iPad
Yahoo axis for embedded devices
Whether you take it as a merit or demerit, but unlike the desktop version, axis is an individual browser application for iOS. It offers a search bar at the top of the screen. The visual search option is more or less same here, giving search a new look. The only features that are a part of interface are the back and forward buttons, bookmarking option, and a share feature to email or tweet a page. The browser can also do tabbed browsing, and you create a tab via the tiny icon at the bottom left of the screen.

With its Launch, Yahoo’s Axis has somehow given a new way to explore internet with a faster and easier access. It has turned out to be a shock that Axis has attracted many followers in no time and it is expected that in coming months, it will be one of the tough competitors of Chrome and Internet Explorer.

DULLY 'MTOTO WA KARIAKOO' OFFICIAL VIDEO ...teentz.com

Final baadae HD teaser new

See Inside P-Square Mansion
Peter Okoye of P-Square uploaded photos from inside his 'Squareville' home on Instagram. See more photos when you continue...

 

 
 
 
 

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...