Tuesday, August 21, 2012

MWANAMKE ALIYEUA, AKATAKA KUJIA, SASA ATAUAWA KWA KUPIGWA RISASI


Waokoaji wakishika miguu ya Fi asijirushe ghorofani jijini Zhanjiang, China
Binti wa Fi (wa pili kulia) aliyefika kumlaghai Fi asijiue. Binti huyo alikuwa hajui mama yake alikuwa amemwua mpwaye.
Sheng Fi, akiendelea kushikiliwa asijiue.
Fi akikokotwa kupelekwa kwenye usalama.
 SHENG FI, ni mwanamke anayeishi katika mji wa Zhanjiang, kusini mwa China.  Hivi majuzi, alimwua mtoto (mpwaye) wa wifi yake mwenye umri wa miaka minne na kumtupa kutoka juu ya jengo la ghorofa nne. Hii ni baada ya ugomvi na wifi yake huyo.
Baada ya hapo Fi  naye alitaka kujirusha  kwenda chini, lakini aliokolewa na wafanyakazi wa jengo hilo ambao  walipanga njama za kumzuia kujirusha chini kwa kumwita binti yake aliyekuja kumlaghai kwa maneno kabla hawajamkamata.
Kwa mujibu wa polisi, kwa kitendo hicho, mwanamke huyo atauawa kwa kupigwa risasi baada ya yeye kukiri kumwua mtoto huyo.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, China inashika nafasi ya tisa duniani kwa watu kujiua ambapo wahusika wakuu wa ‘mauaji’ haya makubwa kuliko yote nchini humo ni watu kati ya miaka 15 hadi 34.
Miongoni mwa nchi zinazoongoza duniani kwa kujiua ni Latvia, Kazhakstan na Korea ya Kusini.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...