Wanafunzi wa chuo kikuu
cha Nairobi Kenya, wameandamana wakiitaka serikali kutatua mzozo wa
mishahara wa wahadhiri wa vyuo vikuu nchini.
Hatua ya wahadhiri hao kugoma kwa wiki tatu
imezitatiza shughuli nyingi ikiwa ni pamoja na kuwazuia wanafunzi hao
kufanya mitihani yao.
Polisi hata hivyo waliwatawanya wanafunzi hao waliokusanyika mjini kwa kutumia gesi za kutoa machozi.
Mapema leo serikali iliahidi kuwalipa wahadhiri hao shilingi za Kenya bilioni 7.8 ili waweze kurejea kazini Jumatatu wiki ijayo.
Hata hivyo malipo hayo yataweza kutolewa kwa awamu mbili kuazia Januari mwaka ujao.
Waziri wa elimu ya juu Margaret Kamar alitoa tangazo hilo akiwataka wahadhiri hao kurejea kazini Jumatatu.
Hata hivtyo wahadhiri hao wamesema hilo bado ni
pendekezo tu la serikali na itawabidi mwanzo kulidurusu kabla ya kufanya
uamuzi wowote.
Aidha wamesema wangali wanashauriana kabla ya kuamua lini watakapositisha mgomo wao.
Wahadhiri waligoma wakishinikiza mikakati mipya
ambayo itawawezesha kuongezwa mishahara maradufu na pia kuongeza
marupurupu yao.
Kwingineko, vuguvugu moja la wazazi limemutaka rais wa nchi hiyo Mwai Kibaki kuwafuta kazi
waziri wa leba John Munyes na mwanasheria mkuu Githu Muigai kwa migomo ya wafanyakazi ambayo imekumba nchi hiyo.
waziri wa leba John Munyes na mwanasheria mkuu Githu Muigai kwa migomo ya wafanyakazi ambayo imekumba nchi hiyo.
Chama cha kitaifa cha wazazi, kimemtuhumu waziri
wa leba kwa kupuuza migomo ya waalimu na wahadhiri wa vyuo vikuu ambayo
imekuwa ikiendelea sasa kwa zaidi ya wiki mbili.
Chama hicho kimeelezea kughadhabishwa na hatua ya serikali kuendelea kuchezea maisha ya watoto wao.
Chama hicho kinapanga kufanya maandamano makubwa
wiki ijayo yatakayowahusisha wanafunzi na wazazi kuonyesha kero lao
kuhusiana na serikali kujikokota kusuluhisha migomo ya walimu.
No comments:
Post a Comment