POLISI nchini Poland wameanzisha uchunguzi
dhidi ya Padri Marcin Kozyra wa Poland baada ya kupatikana kwa picha
zinazowaonyesha wanafunzi wa kike na kiume wenye umri wa miaka 13
wakilamba krimu iliyopakwa kwenye magoti yake.
Kozyra pia ni mwalimu mkuu wa Salesian High School ambako inasemekana kitendo hicho ni utamaduni wa ‘sherehe ya kuwapokea wanafunzi wapya’ kila mwaka.

Picha hizo zinamwonyesha Kozyra akiwa amekaa kitini na akiwa amevaa kaptura na akiwa na fimbo.
Picha zingine zinawaonyesha wanafunzi hao wakitambaa katika ngazi za ghorofani katika mstari ambapo serikali ya Poland na watu wengine wamemelaani kitendo hicho. Lakini pia baadhi ya wazazi wamemuunga mkono padre huyo wakidai pia kwamba inayoonekana kuwa ni krimu, ni dawa inayotumiwa wakati wa kunyoa ndevu.
Inasemekana padri huyo hatachukuliwa hatua yoyote lakini kitendo chake hicho kimelaaniwa.

Chanzo : http://www.dailymail.co.uk
No comments:
Post a Comment