Zaidi ya watu 30 wauwawa katika makabiliano kati ya polisi na wachimba migodi wanaogoma Afrika kusini.
Waziri wa Polisi wa Afrika kusini amesema maafa hayo yalitokea siku ya Alhamisi katika mgodi wa Marikana.
Polisi walifyatua risasi baada ya kushindwa kuwatawanya wagomaji hao waliokuwa wamejihami kwa marungu na mapanga.
Mgodi huo wa dhahabu nyeupe unaomilikiwa na
kampuni ya Lonmin imekuwa ni sehemu ya mapigano makali kuhusu mzozo wa
malipo uliotokana na uhasama kati ya vyama viwili vya wafanyakazi.
Kisa hicho cha polisi ni moja wapo wa operesheni mbaya zaidi ya polisi tangu kumalizika kwa enzi za ubaguzi wa rangi.
Awali machafuko hayo yalioanza wiki iliyopita yalikuwa yamesababisha vifo vya watu 10 na polisi wawili.
Siku ya Ijumaa waziri wa Polisi ,Nathi Mthethwa
akizungumza na kituo kimoja cha Radio alithibitisha kuwa watu wengi
walijeruhiwa na wengine kuuwawa.
Chama kikuu cha wachimba migodi, National Union of Mineworkers ,kinasema idadi ya waliofariki ni 36.
Polisi walikuwa wamepelekwa kwenda kuwatawanya
wachimba migodi wapatao 3,000 ambao walikuwa wamekusanyika eneo la mlima
mkabala na mgodi wa Marikana, ambao uko kilomita 100 kaskazini
mangharibi mwa Johannesburg.
Wafanyakzi hao walikuwa wanataka nyongeza ya mshahara ya dola $1,000 kila mwezi.
Mazingira yaliofanya polisi waanze kufyatua
risasi bado haijajulikana , lakini taarifa kutoka kwa walioshuhudia
zinasema mauji hayo yalitokea wakati kundi la waandamani walipojaribu
kuwavamia polisi.
Hapo ndipo polisi waliokuwa wamejihami kwa bunduki na bastola wakaanza kufyatua risasi.
hatar 2pu jaman
ReplyDeleteMI NIMEONA KATIKA TAARIFA YA HABARI ITV YAANI JAMAA WAMEPIGWA RISASI KAMA KUKU BILA HURUMA DAH
ReplyDeleteingekuwa kibongo bongo hapo.. Nakwmbia mbn wangeibeba roho yng kwny tololi
Delete