Afisa mmoja wa serikali ya Uganda amethibitisha kwamba mtandao wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo umeshambuliwa na wadukuzi.
Sasa mtandao huo unaonyesha picha na ujumbe kutoka kwa wanaharakati wa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.
Katika moja wapo ya ujumbe huyo,
wadukuzu wameweka ujumbe kuonyesha kuwa Waziri Mkuu wa Uganda anaomba
mashoga radhi kwamba eti sasa anaunga mkono maandamano ya watu hao
wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.
Mapenzi ya jinsi moja ni hatia nchini Uganda na
wengi ya wanaoshukiwa kuwa miongoni mwao wamekuwa wakishambuliwa na hata
kutelekezwa na jamii.
Mapema mwaka huu , hoja ya kutaka sheria
ibadilishwe na kuongoze adhabu kwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia
moja kutoka miaka 14 hadi kifungo cha maisha iliwasilishwa kwa mara
nyegine bungeni.
Awali sheria iliyopendekezwa ilikuwa inasema
kwamba yeyote atakaye patikana na hatia ya kufanya mapenzi ya jinsia
moja na mtoto au mlemavu au mtu anayefanya hivyo akiwa na ukimwi ,basi
adhabu yake ni kunyongwa.
Mtandao wa kitengo cha sheria na uadilifu nchini Uganda pia unasemekana wiki hii ulidukuliwa.
Lakini kamishena wa habari na Teknolojia Bwana Ambrose Ruyooka,aliambia BBC kuwa tatizo hilo limerekebishwa.
Serikali ya Uganda imenzisha sheria kali ya tovuti na mtandano ilikukabiliana na ufalifu wa mtandao.
Inandaiwa kuwa mwanaharakati ajayejiita @DramaSett3r katika Twitter, ndiye anayehusika na udukuzi huo.
No comments:
Post a Comment