Wenyeji 12 wa Euro 2020
Michel Platini, rais wa
shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA, amesema michuano ya Euro 2020
huenda ikafanyika katika miji mbalimbali mwaka 2020, badala ya kuwa na
mji mmoja ambao utakuwa ni mwenyeji.
Utamaduni wa mashindano hayo huwa ni nchi moja,
au mbili, kushirikiana katika kuwa mwenyeji, kama ilivyo wakati huu
michuano hiyo kufanyika Poland na Ukraine.
Mashindano yajayo yatafanyika nchini Ufaransa, mwaka 2016.
"Euro 2020 inaweza kufanyika popote barani
Ulaya," alielezea Platini. "Yanaweza kufanyika katika nchi moja yenye
viwanja 12, au kufanyika katika uwanja mmoja katika miji 12 au 13 ya
Ulaya."
Platini ameelezea kwamba wazo hilo pia linaweza
kuokoa senti katika kuepuka gharama kubwa za ukarabati, na juhudi za
kujenga viwanja vipya na kuimarisha viwanja vya ndege.
Uturuki ilitazamiwa na wengi kupata nafasi ya
kuandaa mashindano ya mwaka 2020, lakini ombi la nchi hiyo limekumbwa na
tatizo, kwa kuwa nchi hiyo pia ina nia ya kuandaa michezo ya Olimpiki
mjini Istanbul, mwaka huohuo wa 2020.
Mataifa ya Uskochi, Wales na Jamhuri ya Ireland, rasmi pia yameelezea nia yao ya kuandaa michuano ya 2020.
Platini ametangaza kwamba uamuzi kamili utatangazwa kati ya mwezi Januari hadi Februari mwaka ujao.
No comments:
Post a Comment