Kvitova na Serena wafuzu raundi ya nne
Bingwa mtetezi wa mashindano ya
Wimbledon kwa upande wa kina dada, Petra Kvitova kutoka Jamhuri ya
Czech, na bingwa mara nne katika mashindano hayo, Mmarekani Serena
Williams, wote walifuzu kuingia raundi ya nne ya mashidano hayo siku ya
Jumamosi.
Williams, baada ya kulemewa na mpinzani kutoka Uchina, Zhenj Jie, hatimaye aliweza kupata ushindi wa 6-7 (5-7) 6-2 9-7
Kvitova alimshinda kwa urahisi mpinzani wake kutoka Marekani, Varvara Lepchenko, kwa 6-1 6-0.
Ana Ivanovic, ambaye amepangwa katika nafasi ya
14 katika orodha ya wachezaji bora wa kike katika mashindano ya
Wimbledon, aliweza kumshinda Mjerumani Julia Goerges 3-6 6-3 6-4, na
sasa atakutana na mchezaji aliyepangwa katika nafasi ya pili katika
mashindano hayo, Victoria Azarenka kutoka Australia.
Yaroslava Shvedova alikuwa mchezaji wa kwanza
kupata ushindi wa kirahisi na kufuzu moja kwa moja kusonga mbele, baada
ya mpinzani wake, Sara Eerrani kushindwa kupata pointi katika seti ya
mwanzo, na hatimaye kushindwa 6-0 6-4.
Shvedova, aliyepangwa katika nafasi ya 65 ya
mashindano hayo, sasa lazima ajiandae vyema kwa raundi ya nne, katika
kukutana na Serena, aliyepangwa katika nafasi ya 6 katika mashindano ya
mwaka huu ya Wimbledon.
No comments:
Post a Comment