Vita Club yaalikwa michuano ya CECAFA
Vita Club ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo imealikwa kushiriki katika michuano ya klabu ya
shirikisho la CECAFA, mashindano ambayo yataanza tarehe 14 mwezi Julai
hadi 28 mwaka huu wa 2012.
Jumla ya timu 11 zitashiriki katika mashindano
hayo ya wiki mbili, na ambayo yataonekana moja kwa moja kupitia
televisheni katika mataifa 48 ya Afrika.
Mataifa
mengine ambayo yatashiriki katika mashindano hayo ni Yanga, ambao ndio
mabingwa watetezi, Simba na Azam, kutoka Tanzania, Tusker ya Kenya, APR
ya Rwanda, Atletico ya Burundi, Ports ya Djibouti, Mafunzo ya Zanzibar,
Wau Salam ya Sudan Kusini na Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo.
Katika droo iliyofanyika mjini Dar es Salaam,
mabingwa Yanga wamepangwa kufungua mashindnao hayo kwa kucheza na
Atletico ya Burundi, tarehe 14 Julai.
Kulingana na katibu mkuu wa CECAFA, Nicholas
Musonye, CECAFA ina nia ya kuifanya michuano hiyo kuwa kati ya
mashindano maarufu zaidi ya soka barani Afrika.
"Ikiwa kuna wadhamini wa kutosha mwaka ujao,
huenda tukawa na timu 16, kufuatia vilabu zaidi vya Afrika kuvutiwa na
mashindano haya", alielezea Musonye kupitia taarifa ya CECAFA.
Mdhamini mkuu wa CECAFA, Rais Paul Kagame,
tayari ameahidi zawadi ya dola za Marekani elfu 60,000, ambazo
zitagawanywa na timu tatu bora katika michuano hiyo.
Vita Club ni kati ya vilabu kongwe na maarufu
vya soka katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, na ni kati ya vilabu
vinne ambayo viliomba kushirikishwa katika michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment