Wahamiaji haramu wakwama baharini
Meli moja ya jeshi la wanamaji wa Australia imewasili katika eneo ambako meli iliyobeba wahamiaji haramu ipo.
Wakuu wa serikali ya Australia wanasema, hali
mbaya ya anga imezuia wahamiaji hao haramu kuabiri meli hiyo ya kijeshi
lakini wanamaji hao bado wanadadisi hali ilivyo.
Meli
hiyo inasemekana kubeba wahamiaji haramu kati ya 130 na 180, ilitoa
ujumbe wa kutaka msaada wa dharura wakati ilipokuwa katika eneo la
bahari kati ya Indonesia na Kisiwa cha Christmass.
Tukio hilo limejiri siku moja tu baada ya
viongozi wa mataifa hayo mawili, kuahidi kushirikiana katika harakati za
kuzuia na kuthibiti ulanguzi wa watu, baada ya meli nyingine mbili
iliyokuwa imebeba wahamiaji haramu kuzama mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na shirika
linalosimamia na kuthibiti safari za meli nchini Australia, AMSA, meli
moja ya mizigo ilikuwa karibu na manuwari hiyo ya kijeshi ilikuwa
ikielekea katika eneo hilo.
Manuwari hiyo ya jeshi la wanamaji wa Australia ijulikanayo kama HMAS Wollongong inasemekana kuendlea kuchunguza hali hiyo.
'' kuna ishara za kuthibitisha kuwa meli hiyo
ipo hatarini, na hali hiyo itachunguzwa baada ya wanamaji wetu kuabiri
meli hiyo na wakati hali ya anga itakapoimarika'' taarifa hiyo ilisema.
Waziri wa mambo ya ndani Jason Clare, amesema
meli hiyo ilituma ujumbe wa kutaka msaada wa dharura kwa kuwa lilikuwa
inavuja maji.
No comments:
Post a Comment