Kwa mara ya kwanza kifaa cha
kujipima iwapo mtu ana virusi vinavyosababisha ukimwi kimeidhinishwa na
wataalam wanaodhibiti sekta ya Afya nchini Marekani.
Kifaa hicho kwa jina OraQuick kitawezesha watu kutumia mate kuchunguza kama wana virusi vya ukimwi.
Itachukua muda wa kati ya dakika 20 na 40 kubaini matokeo ya uchunguzi huo.
Kifaa hicho ambacho kitawezesha mtu kuchunguza
hali yake mwenyewe nyumbani au kokote anakotaka kitaanza kuuzwa nchini
Marekani mwezi Oktoba mwaka huu.
Serikali ya Marekani inatarajia kuwa kifaa hicho
kitasaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kubadili tabia
miongoni mwa watu wanaoishi na virusi bila kujua.
Inakadiriwa kuwa robo millioni ya Wamarekani wako katika kitengo hicho.
Utafiti wa kimatibabu unaoyesha kuwa majaribio
ya matokeo ya uchunguzi wa kifaa hicho cha Oraquick yananaweza kuwa
sahihi kwa asilimia tisini na mbili, miongoni mwa watu wanoishi na
virusi vya ukimwi.
No comments:
Post a Comment