Barabara yafunguliwa tena Pakistan
Serikali ya Pakistan imesema
itafungua upya barabara zinazotumiwa kusafirishia bidhaa za wanajeshi wa
muungano wa NATO nchini Afghanistan.
Hii ni baada ya kupokea rasmi ombi la msamaha
kutoka kwa serikali ya Marekani, kufuatia mashambulio ya anga
yaliyotekelezwa na wanajeshi wa marekani, yaliyopelekea kuuawa kwa
wanajeshji ishirini na wanne wa nchini Hiyo.
Waziri
wa mambo ya nje wa marekani, Bi Hillary Clinton, amesema serikali ya
Pakistan imeamua kufungua upya barabara hizo zinazotumiwa kusafirisha
bidhaa za wanajeshi wa muungano wa NATO, ambazo zilifungwa mwezi Novemba
mwaka uliopita.
Pakistan ilifunga barabara hizo baada ya
wanajeshi 24 wake kuuawa kwenye shambulio la anga lililotekelezwa na
wanajeshi wa muungano wa NATO.
Bi Clinton ameafiki tangazo hilo na kuomba radhi kufuatia shambulio hilo.
Amesema amefahamishwa na waziri wa mambo ya nje wa Pakistan kuwa barabara hizo zinafunguliwa tena.
Bi Clinton, amesema serikali ya Pakistan haitatoza ushuru zaidi bidhaa zitakazosafirishwa kupitia nchi hiyo.
Waziri mkuu wa Pakistan, Raja Pervez Ashraf
amesema ufunguzi tena wa barabara hizo muhimu utasaidia kuimarisha
uhusiano kati ya Pakistan na Marekani na pia ni mchango wa serikali yake
ya kuafikiwa kwa hali ya uthabiti na usalama katika nchi jirani ya
Afghanistan.
No comments:
Post a Comment