Waasi DRC tayari kuzungumza na serikali
Kikundi cha wapiganaji wa
mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, kiitwacho M23, kmeuteka mji
muhimu kwenye mpaka wa Congo na Uganda.
Wakaazi wa Rutshuru walisema
wapiganaji hao wa kikundi cha M23, waliingia mjini bila ya kupigana, kwa
vile wanajeshi wa serikali na askari wa Umoja wa Mataifa walikuwa
wameshaondoka.
Kikundi hicho kimekuwa kikifanya mashambulio katika siku za karibuni, na kusababisha maelfu ya watu kukimbilia Uganda.
Afisa mmoja wa kikundi hicho cha M23, Kanali
Vianney Kazarama, aliliambia shirika la habari la Reuters, kwamba wao
hawatateka miji mengine iwapo serikali itakubali kuzungumza nao.
Mpiganaji huyo, Kanali Kazarama, piya alikanusha
tuhuma za ripoti ya Umoja wa Mataifa, kwamba makundi ya wapiganaji
nchini Congo, yanasaidiwa na Rwanda:
No comments:
Post a Comment