Wafungwa Malawi watimka
Wafungwa kwenye gereza moja ya
Malawi wamefanya ghasia kupinga msamaha waliopewa baadhi ya wafungwa
wenzao, ambao wanaona haukuwa wa haki.
Rais Joyce Banda, siku ya Ijumaa aliwasamehe wafungwa karibu 400, lakini siyo wale waliofungwa kwa sababu ya mauaji au ubakaji.
Wafungwa katika gereza ya Zomba, mashariki mwa
nchi, walitoroka kwenye seli zao na kuwabughudhi wasimamizi, wakisema
wafungwa wawili waliosamehewa ni wahalifu wa mauaji na ubakaji.
Bibi Banda alisema wabakaji wanafaa kufa jela, hasa wale waliowabaka watoto.
Ubakaji wa aina hiyo unatokea mara kadha Malawi,
kwa sababu kuna wanaoamini kuwa kufanya mapenzi na msichana bikira
kunaleta mali na kunatibu HIV na UKIMWI.
No comments:
Post a Comment