Webber mshindi wa Silverstone
Mark Webber, dereva wa timu ya Red Bull, siku ya Jumapili aliibuka bingwa wa mashindano ya Uingereza ya magari ya Grand Prix.
Dereva huyo kutoka Australia, aliweza kumpita
Fernando Alonso kutoka Uhispania, katika raundi za mwishomwisho za
mashindano hayo ya Silverstone.
Alonso
aliweza kuongoza kwa muda mrefu tangu mwanzo wa mashindano, lakini
Webber aliweza kutumia mbinu kwa upande wa kubadilisha magurudumu, na
hatimaye kuweza kufukuzana kwa kasi na dereva huyo wa Uhispania.
Alonso hatimaye alimaliza katika nafasi ya pili,
na Mjerumani Sebastian Vettel, dereva wa timu ya Red Bull, alimaliza
katika nafasi ya tatu.
Felipe Massa, kutoka Brazil, na akiwa ni dereva wa Ferrari, alimaliza katika nafasi ya nne.
Lewis Hamilton, dereva wa McLaren, ilibidi
aridhika na kumaliza katika nafasi ya nane, huku Muingereza mwenzake,
Jenson Button, na pia akiwa katika timu ya McLaren, akishikilia nafasi
ya 10.
“Nimewahi kuibuka mshindi mara chache, lakini
ushindi huu bado haujaniingia akilini. Nilipata nafasi moja ya kuongoza,
na kamwe sikutazamie iniepuke,” alielezea Webber.
Webber sasa yumo katika nafasi ya nne katika
kuwania nafasi ya dereva bora zaidi msimu huu, akiachwa na Alonso kwa
pointi 37 sasa.
Vettel yumo katika nafasi ya tatu, na tofauti kati yake na Alonso ni pointi 29.
Timu ya McLaren, ambayo ilianza msimu ikiwa na
gari lenye kasi zaidi, sasa inaelekea wanaendelea kuachwa nyuma na Red
Bull na Ferrari, ambayo wamweza kuimarisha magari yao zaidi.
Mashindano ya Silverstone yaliamuliwa kupitia magurudumu.
Huku Ferrari wakiamua kumuanzisha Alonso kwa
kutumia magurudumu magumu zaidi, kama walivyofanya mafundi wa McLaren
pia waliohusika na Hamilton, kinyume na hayo, Red Bull waliamua kutumia
matairi ya kawaida yaliyo mepesi zaidi.
Ushindi huu umemfanya Webber, kama Alonso, kuwa
madereva wawili wa pekee msimu huu ambao wameweza kuibuka washindi
katika mashindano
No comments:
Post a Comment