Ujenzi wa bwawa umeanza tena Lao
Wanaharakati wa mazingira
wanasema wanasema serikali ya Laos imeanza ujenzi wa mradi wa bwawa la
maji katika mto Mekong, ambao umekuwa ukipingwa vikalu na mataifa
jirani.
Waandishi wa habari wa BBC, hawakuruhusiwa
kuzuru bwala hilo katika eneo la Xayaburi, lakini kwa mujibu wa picha za
video zilizonakiliwa na shirika la Kimataifa linalohusika na mikakati
ya kuhifadhi mito la International Rivers, mradi huo wa ujenzi
umeonekana kuanza.
Serikali ya Laos imesema kazi hiyo inayoendelea
ni matayarisho na hakuna uamuzi wowote ambao umeafikiwa ikiwa mradi huo
wa ujenzi wa bwawa la maji utaendelea au la.
Serikali ya Cambodia na Vietman pamoja na
mashirika mengine ya kutetea mazingira, wanataka utafiti wa athari za
mradi huo kwa mazingira, viwango vya samaki na viumbe vingine katika mto
huo kufanyika kabla ya mradi huo kuruhusiwa kuendelea.
No comments:
Post a Comment