Lopez ataka kura kuhesabiwa tena
Mgombea wa urais nchini Mexico,
aliyemaliza katika nafasi ya pili katika uchaguzi wa urais, Andres
Manuel Lopez Obrador, ameiomba tume ya uchaguzi nchini hume kurejelea
tena shughuli ya kuhesabu kura, ya uchaguzi uliofanyika siku ya
jumapili.
Bwana Lopez Obrador, wa chama cha mrengo wa
kushoto cha PRD, amesema kulikuwa na dosari nyingi katika vituo vingi
vya kupigia kura.Huku asilimia 60 ya kura zote zikiwa zimehesabiwa, Bwana Lopez Obrador, yuko asilimia 6 nyuma ya Enrique Pena Nieta wa chama cha PRI.
Baada ya kushindwa katika uchaguzi wa urais wa mwaka wa 2006, Bwana Lopez Obrador, aliongoza maandamano makubwa kupinga matokeo ya uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment