Tsvangirai atofautiana na waziri
Waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan
Tsvangirai, amemlaani waziri mmoja wa serikali, ambaye alitangaza kuwa
benki za kigeni ni sharti kuachia asilimia kubwa ya hisa zake kwa raia
wa nchi hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.
Bwana Tsvangirai amesema serikali ya nchi hiyo haijajadili au kuidhinisha tangazo hilo.
Tvangirai
ameshutumu waziri wa masuala ya kitaifa, Saviour Kasukuwere, kwa
kusambaza habari zinazoashiria kuwa serikali ya nchi hiyo inanuia
kunyakua umiliki wa kampuni na taasisi nchini humo.
Waandishi wa habari wanasema sera hiyo,
imegawanya serikali ya mseto ya nchi hiyo, inayoshirikishwa chama cha
Bwana Tsvangirai na chama cha Rais Robert Mugabe cha ZANU PF.
Ilitangazwa mapema Jumanne kuwa benki lazima
kuzingatia sheria ya mwaka 2007 ambayo inashurutisha asilimi 51 hisa za
benki zote kuwa mikononi mwa raia wa nchi hiyo.
Benki Kuu na Wizara ya Fedha zimesema kuwa hatua kama hii itahujumu uchumi wa Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment