Diamond kuhojiwa na kamati ya Bunge
Aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa
benki ya Barclays, moja ya benki kubwa zaidi nchini Uingereza,
atahojiwa na kamati maalum ya bunge hii leo.
Bwana Bob Diamond, ambaye alijiuzulu hiyo jana
anatarajiwa kuhiojiwa kuhisana na sakata ya kuongezwa kwa viwango vya
riba iliyopelekea kujiuzulu kwake.
Diamond, alijiuzulu hiyo jana baada ya benki ya
Barclays kushutumiwa vikali kwa kuhujumu na kuongeza viwango vya riba
kinyume cha sheria.
Benki hiyo imepigwa faini mabilioni ya dola kufuatia kashfa hiyo.
Waandishi wa habari wanasema, Bwana Diamond
atahojiwa kuhusiana na mazungumzo aliyofanya na naibu gavana wa benki
kuu, wakati viwango hivyo vya riba viliongezwa.
poyeeeeeeeeeeeeeeeeee mzunguuuuuuuuuuuuuuu
ReplyDelete