Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akisalimiana na
mpiga picha wa gazeti la Daily News Yusuf Badi Katika maonyesho ya 36 ya
biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere
barabara ya Kilwa jijini Dar.
Dkt.
Alberic Kacou (kulia) akikaribishwa na Msaidizi (Ushirikishwaji Habari
Umma) wa UNHCR Bw. Austin Makani alipotembelea katika banda la Umoja wa
Mataifa Tanzania.
Bw.
Austin Makani (kushoto) akitoa maelezo kwa Dkt. Kacou kuhusiana na
shughuli zinazofanyika katika banda hilo wakati wa maonyesho hayo.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou (katikati)
akizungumza na Afisa Mawasiliano wa Shirika la Kazi nchini (ILO) Bw.
Magnus Minja (kulia) pamoja na Bw.Austin Makani wa UNHCR alipotembelea
banda la Umoja wa Mataifa.
Dkt.
Kacou (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mata
Enterprises Company Bi. Tabby Oguma ambaye ni mmoja wa wajasiriamali
wanaowezeshwa na shirika la Kazi Duniani (ILO) kuhusu bidhaa
wanazotengeneza ikiwemo jiko la kupikia (Cooking Basket).
Dkt. Alberic Kacou akitazama magauni ya Batiki yanayotengenezwa na Kampuni hiyo.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou akiweka saini kitabu cha
wageni katika banda la UN Tanzania lililopo katika banda kubwa la Ali
Hassan Mwinyi katika maonyesho ya 36 ya Sabasaba yanayoendelea jijini
Dar. Kulia ni Bw. Magnus Minja wa ILO na Kushoto ni Bw. Austin Makani wa
UNHCR.
Dkt.
Alberic Kacou katika picha ya pamoja na wafanyakazi shirika la Umoja wa
Mataifa wanaotoa huduma katika banda la shirika hilo.
No comments:
Post a Comment