TIMU ya Yanga imepata kashfa nzito baada ya kudaiwa fedha za pilau la hitima.
Yanga inadaiwa kiasi cha shilingi 433,000 na mama lishe ambao walipika chakula hicho wakati klabu hiyo ilipofanya hitima ya kuwakumbuka wanachama wa klabu hiyo waliofariki dunia.
Mmoja wa wapishi ambao aliomba jina lake lihifadhiwe alisema waliagizwa na uongozi wa Yanga kuandaa chakula hicho kwa ajili ya hitima hiyo ambayo ilifanyika klabuni hapo mitaa ya Twiga na Jangwani wiki iliyopita, lakini hadi leo hawajapewa fedha zao.
Alisema awali walikubaliana na Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali, kuwa baada ya kumaliza kupika watapewa chao hapohapo lakini mambo hayakuwa hivyo.
Mpishi huyo amesema baada ya kumaliza kazi, walipokwenda kudai haki yao walianza kupigwa danadana za mara leo, mara kesho.
Kufutia kitendo hicho, Championi lilimpigia simu Akilimali ambaye alikiri kudaiwa na wapishi hao na kuwataka watulie kwani suala lao linashughulikiwa.
“Ni kweli wanatudai 433,000/- lakini wasiwe na wasiwasi fedha yao ipo, tutawalipa, si unajua siku hizi mambo ya cheki? Sasa fedha inapokuwa kwa njia ya cheki huwezi kuipata haraka kama wanavyotaka wao, waambieni watulie ni kweli wanatudai lakini tutawalipa,” alimaliza kusema Akilimali.

No comments:
Post a Comment