Mcheza soka mashuhuri duniani na
nyota ya Argentina, Diego Maradona amefutwa kazi kama Meneja wa klabu
ya nchini Imarati Al Wasl baada ya kuiongoza kwa kipindi cha miezi 14.
Mkongwe huyo alianza kuingia mashaka mnamo mwezi
Juni baada ya bodi nzima ya uongozi wa klabu kujiuzulu kufuatia matokeo
yasiyoridhisha na kuhitimisha msimu mzima bila kombe lolote.
Maradona,
mwenye umri wa miaka 51 alijiunga na klabu hio yenye makao yake mjini
Dubai mwezi May mwaka 2011 na hadi kupigwa mkasi alikuwa na mwaka mmoja
uliosalia kwenye mkataba wake.
Msimu uliopita klabu yake ya Al Wasl ilimaliza katika nafasi ya nane.
Taarifa iliyotolewa baada ya kikao cha Bodi ya
wakurugenzi wa Al Wasl football company kutathmini uongozi wa Diego
Maradona na wasaidizi wake, uwamuzi umefikiwa wa kumfuta kazi Maradona
pamoja na wasaidizi wake.
Itakumbukwa kuwa Maradona mshindi wa Kombe la
Dunia akiichezea nchi yake Argentina mnamo mwaka 1986 alitia for a mwaka
huu alipokabiliana na mashabiki wa upinzani kwa ujasiri.
Wakati wa mechi ambayo klabu yake Al Wasl
ilichapwa 2-0 na Al Shabab,inafahamika kuwa alikimbia hadi kiti
alichokuwa amekaa mke wake ili mashabiki waliokua wamejaa hasira
wasimdhuru baada ya kuwarushia matusi wake na marafiki wa wachezaji
wake.
Maradona aliajiriwa ili kuizidishia umaarufu
klabu ya Al Wasl ndani na nje ya uwanja, lakini ilimaliza msimu ikiwa
nyuma ya mshindi wa Ligi Al Ain kwa pointi 29.
No comments:
Post a Comment