Mcheza soka maarufu wa Ureno
mwenye asili ya Msumbiji, aliyeichezea Timu ya Taifa ya Ureno na klabu
ya Benfica, Eusebio,ameagwa kutoka hospitali alikolazwa wakati wa kombe
la Euro 2012 nchini Poland.
Eusebio, mwenye umri wa miaka 70, alilazwa tena
mjini Lisbon baada ya kuwaswili kutoka Poland kwa ndege ambapo hali yake
haikuwaridhisha madaktari.
Mchezaji huyo mkongwe aliyepewa jina la Black
Panther akiwa ni balozi wa Ureno wa soka amekuwa akisumbuliwa na
shinikizo la damu. Eusebio anakumbukwa mno kwa mchango wake wa mabao
yaliyoiwezesha Ureno kumaliza ya tatu kwenye Kombe la Dunia la mwaka
1966 nchini England.
No comments:
Post a Comment