Wanasayansi nchini Marekani wanasema kuna dalili wamegunduwa njia ya kutibu ugonjwa wa ukimwi.
Watafiti hao wanasema kuwa wamepata njia ya kuviondoa virusi vinavyo sababisha ukimwi mwilini kutumia dawa ya kukinga saratani.
Virusi vya ukimwi mara nyingi huwa huishi
mwilini kwa miaka mingi bila ya kutambulika, hivyo kuifanya kuwa vigumu
kutibu ugonjwa huo.
Katika nyaraka zao kwenye jarida la matibabu la
Nature, watafiti hao wanasema kuwa wamepata njia ya kuvimulika virusi
hivyo mwilini na kuwa baada ya kufanya hivyo wameweza kuviua kutumia
dawa za kuongeza nguvu mwilini.
Tayari majaribio kwa wagonjwa wanane zimefanikiwa.
Hata hivyo wamesema kuwa bado kunahitajika utafiti zaidi wa kuwezesha kuundwa dawa marudufu ya kumaliza ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment