•KUOGELEA: Ryan Lochte
alimuangusha Mmarekani mwenziye akiwa ni mshindi wa medali za dhahabu
kwenye mashindano ya Olimpiki mara mbili Michael Phelps aliyezoa medali
nane mjini Beijing mwaka 2008 na kushinda dhahabu kwenye mbio za mita
400 kwa mashindano ya kuchanganya staili tofauti.
•BAISKELI: Tumaini la Uingereza kushinda medali
ya dhahabu katika mbio za baiskeli za masafa ya kilomita 250 Mark
Cavendish aliondoka mikono mitupu baada ya Alexandre Vinokourov wa
Kazakhstan kushinda mbio hizo.
•KUPIGA
MAKASIA: Helen Glover na Heather Stanning waliweka rekodi mpya ya
Olimpiki wakishinda mbio za mchujo ya washiriki wawili wawili.
•KUOGELEA: Sun Yang alijitokeza kuwa muogeleaji
wa kwanza mwanaume kutoka Uchina kushinda medali ya dhahabu katika mbio
za mita 400 freestyle akiweka rekodi ya mashindano haya kwenye Olimpiki.
•KUOGELEA : Ye Shiwen mwenye umri wa miaka 16 wa
Uchina akavunja rekodi ya dunia kwa kuondoa sekunde moja , na kushinda
mbio za mita 400 mchanganyiko wa staili.
•KUPANDA FARASI: Mary King wa Uingereza alimaliza siku ya kwanza katika nafasi ya tatu.
•KULENGA SHABAHA: Nur Suryan Mohamad wa Malaysia
licha ya kuwa mja mzito alishindwa kutimiza ndoto yake ya kufuzu kwa
fainali ya kulenga kutoka umbali wa mita 10 kutumia bunduki ya
upepo.Ingawa hakufaulu hakufa moyo.
•KULENGA SHABAHA: China ilijinyakulia medali
yake ya kwanza na pia ya kwanza kwenye mashindano haya ya London 2012
katika mashindano hayo hayo ambamo Nur alishindwa kufuzu.
•MASUMBWI: Anthony Ogogo aliamsha nyota ya
Uingereza na kikosi kizima kwa ushindi dhidi ya Junior Castillo Martinez
kwenye ukumbi wa ExCel.
TENNIS : Mabingwa wa mashindano ya Wimbledon
Roger Federer na Serena Williams walianza vizuri mashindano ya Olimpiki
kwa ushindi, ingawa Federer alikua na kibarua kuliko ilivyodhaniwa.
Raia huyo wa Uswizi alipewa mtihani mkali na
Alejandro Falla wa Colombia ambaye aliwahi kumsumbuwa kwenye mashindano
ya Wimbledon ya mwaka 2012.Hatimaye Federer akashinda 6-3 5-7 6-3.
Serena Williams alimshinda Jelena Jankovic wa Serbia 6-3 6-1.
Kim Clijsters wa Ubelgiji anayetazamia kustaafu mchezo huu akamshinda Roberta Vinci wa Italy 6-1 6-4.
Clijsters atapambana na Carla Suarez Navarro wa Uhspania wakati Williams atachuana na Urszula Radwanska wa Poland.
No comments:
Post a Comment