Wahamiaji 42 wafa kwenye lori Tanzania
Wahamiaji haramu arobaini na
wawili wamepatikana wakiwa wamekufa ndani ya lori walimokuwa wakisafiria
katika mkoa wa Dodoma, nchini Tanzania.
Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania,
Pereira Silima, amesema kuwa watu hao waliokuwa wamesongamana ndani ya
lori waliaga dunia kutokana ukosefu wa hewa safi.
''Taarifa
tuliyopata ni kwamba kulikuwa na wasafiri waliokuwa wakisafirishwa
kwenye lori, ambalo lilikuwa kama kontena na halikuwa na hewa ya
kutosha''.Bwana Silima ameambia BBC.
wahamiaji walikuwa wanatoka Ethiopia
Amesema wahamiaji hao haramu kutoka Ethiopia walikuwa wakijaribu kuingia Malawi.
Kulingana na bwana Silima wahamiaji hao walianza
kufariki dunia wakiwa safarini. Jihudi za wahamiaji hao kumjulisha
dereva kuhusiana na hali yao hazikufanikiwa, na hivyo kusababisha maafa
ya watu arobaini na moja ndani ya lori hilo.
Kulingana na naibu waziri huyo wa mambo ya ndani
tukio hilo lilifanyika Jumatatu usiku. Na baada ya dereva huyo kugundua
kuwa watu wamefariki, aliondoa miili yao na kuitupa nje kabla ya
kutoweka.
Mtu mmoja alifariki dunia akifanyiwa matibabu katika hospitali ya mkoa mjini Dodoma.
uhamiaji haramu umeenea
Polisi nchini Tanzania wamesema wanamsaka dereva huyo ambaye alitoroka punde tu baada ya kushusha miili ya wahamiaji hao haramu.
Biashara ya kuwasafirisha wahamiaji haramu hasa
wanaotoka nchi za Somalia na Ethiopia kupitia Tanzania imeenea sana.
Wengi huelekea mataifa ya kusini mwa Africa kutafuta maisha bora.
No comments:
Post a Comment