Raia wa Nigeria wahimizwa kupanga uzazi
Rais wa Nigeria Goodluck
Jonathan anasema wakati umefika raia wake kupanga uzazi. Kiongozi huyo
amesema kuna watoto wengi sana wanaozaliwa na ipo haja kuwepo na sheria
ya kuwa na mpango wa uzazi.
Ameongeza watu wasio jua kusoma wala kuandika
wameendelea kuwapata watoto wengi ambao wanashindwa kuwapa mahitaji
muhimu ya maisha.Umoja wa Mataifa unakadiria idadi ya Nigeria kuongezeka
kutoka milioni 160 hadi milioni 400 ifikapo mwaka 2050.
Nigeria inaongoza kwa idadi kubwa
zaidi ya watu Afrika na juhudi za awali kuwashawishi wazazi kuwapata
watoto wachache ziligonga mwamba.
Mwandishi wa BBC Will Ross amesema ongezeko la
watu linapunguza raslimali hali inayotishia kuwepo na machafuko ya
kushindania raslimali hususan arthi.
Rais Jonathan amesema ipo haja kuwepo na sheria ya kudhibiti idadi ya watoto wazazi wanaopata katika siku za usoni.
Amelitaka Baraza la Idadi ya watu kuanza kampeini ya kushawishi jamii umuhimu wa mpango wa uzazi.
Amesema japo suala hili ni nzito kutokana na
misimamo ya kidini na kimila, ipo haja jamii kubadilisha mawazo kwamba
watoto ni baraka kutoka kwa Mungu.
No comments:
Post a Comment