Syria ilidungua ndege bila ya onyo
Uturuki inasema kuwa ndege yake
ya kijeshi iliyotoweka Ijumaa, ilikuwa juu ya bahari ya kimataifa,
wakati Syria ilipoidungua bila ya onyo.
Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa
Uturuki, Ahmet Davutoglu, alisema ndege hiyo iliiingia kwenye anga ya
Syria, lakini haraka iliondoka.
Bwana Davutoglu alishikilia kuwa ndege hiyo haikuwa ikifanya baya.
Syria inasema ndege hiyo ilikuwa karibu na mwambao wake.
Waziri Mkuu wa Uturuki anakutana na viongozi wa
vyama vyengine bungeni baadae hii leo, kuamua hatua gani ya kuchukua
dhidi ya Syria.
Uturuki imewasiliana na Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa na mataifa matano yenye uanachama wa kudumu katika baraza la
usalama la Umoja wa Mataifa.