Fernando Alonzo ashinda Langalanga Ulaya
Dereva wa magari ya Timu ya
Ferrari Fernando Alonso amekua dereva wa kwanza kushinda mara mbili
mwaka huu kwa ushindi wa kishindo kwenye mashindano ya Ulaya.
Yeye Alonzo alianza katika nafasi ya 11 kabla ya
gari la usalama kuingilia mashindano kufuatia ajali lakini juhudi zake
zilimuezesha kupambana hadi nafasi ya nne.
Aliweza
kuongoza kufuatia mizengwe iliyotokea ndani ya kituo cha magari ya
McLaren ambako wakati wa kubadili tairi na kuongezea mafuta Hamilton
alipoteza zaidi ya sekundi 14 na kwa bahati nzuri dereva aliyekua
akiongoza Sebastien Vettel akashindwa kumaliza mbio hizo.
Kimi Raikkonen alimaliza wa pili, il hali
Hamilton akikwama ikisalia mizunguko miwili baada ya kukwaruzana na
Pastor Maldonaldo wa timu ya magari ya Williams.
Hadi hapo Hamilton alikua akishikiliaa nafasi ya
pili akijitahidi kumaliza katika nafasi hio licha ya tairi kuishilia
kwa kasi na Maldonaldo alimuingilia na kulichana gari kiasi kwamba
halingeweza kuendelea na mbio.
Ushindi wa Alonzo ni wa 29 ukimweka tangu aane
kushiriki mbio za magari na unamuweka kileleni mwa Madereva bora akiwa
na pointi 20, Mark Webber ni wa pili na Hamilton wa tatu, Vettel
anashikilia nafasi ya nne akiwa nyuma ya Alonzo kwa tofauti ya pointi
26.