Monday, April 22, 2013

MTOTO WA MWEZI MMOJA NA NUSU ABAKWA NA BABU YAKE

Mtoto wa kike mwenye umri wa mwezi moja na nusu amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa akiwa katika hali mbaya baada ya kudaiwa kunajisiwa na kuchanika vibaya sehemu zake za siri na kusababisha kupata haja kubwa na ndogo katika sehemu moja.

Habari za awali ambazo zilipatikana zilidai kuwa mtoto huyo alikuwa amenajisiwa na babu yake.

Akiongea katika wodi namba saba ya hospitali hiyo mama mzazi wa mtoto huyo Regina Msemakweli (24), mkazi wa Kijiji cha Isingu alisema kwa mtoto huyo alizaliwa Februari 25, mwaka huu wakati akiwa njiani kuelekea hospitali kujifungua.

Alisema kuwa, Aprili 17, mwaka huu aligundua kuwa mtoto wake amebakwa baadaya kurudi kutoka kisimani na kumkuta akilia bila kunyamaza na wakati wakwenda kisimani alimuacha mtoto huyo akiwa na mama mkwe na mtoto wake mwingine mdogo mwenye umri wa miaka miwili.

Regina alisema kuwa baada ya kuona mtoto akilia bila kunyamaza alimua kwenda kumuogesha ndipo aligundua sehemu za siri za mtoto huyo zikiwa zimevimba na kugundua alikuwa amechanika vibaya na alianza kutoa haja kubwana ndogo kwenye sehemu ya haja ndogo.

Alisema kuwa hali ya mtoto wake bado si nzuri kwani uvimbe sehemu za siri umepungua kidogo lakini madaktari baada ya kumchunguza mtoto walisema kuwa amebakwa.

“Nasikia tu na mimi kuwa watu wanasema amebakwa na baba mkwe wangu lakini wakati kitendo hicho kinatokea nilikuwa kisimani,” alisema.

Mganga mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa, DkLunemo Sakafu alisema kuwa, mtoto huyo alifikishwa hospitalini hapo na walipomchunguza waligundua kuwa alikuwa akitoka haja kubwa na ndogo kwenye sehemu moja. Alisema kuwa baada ya kufanyiwa uchunguzi alianzishiwa matibabu.

Muuguzi Mkunga wa hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa, Mary Mgonela alisema kuwa, mtoto huyo alipokelewa siku nne zilizopita akiwa na wifi yake kwani hata baba wa mtoto alipotakiwa kumpeleka mtoto huyo hospitali alisema kuwa alikuwa akienda kuchunga ng’ombe.

Alisema kuwa baada ya kuonekana suala hilo lazima litolewe taarifa Polisi Wifi yake alitakiwa kwenda polisi kuchukua PF 3 lakini hakurudi na alikwenda moja kwa moja mpaka sasa hajawahi kuonekana hata kuja kumjulia hali mtoto. Alisema kuwa baada ya wifi huyo kutoonekana ilibidi ripoti ilipotiwe kwa daktari na kisha polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Alisema kuwa katika maelezo ya mama wa mtoto kabla ya kufika hospitali walianza kwenda kwa mganga wa kienyeji ambapo alisema kuwa haliwezi suala hilo na ndipo walipoamua kuja hospitali.

Muuguzi huyo alisema kuwa, mtoto huyo ameumizwa vibaya na anaendelea kupatiwa matibabu huku madaktari wakijitahidi wanavyoweza kuokoa maisha yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, kamishna msaidizi wa Polisi, David Misime alisema kuwa, hana taarifa jua ya tukio hilo na atalifuatilia.

---

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...