Monday, April 22, 2013

LULU AINGIA LOCATION.....

Lulu aingia location, Lulu ‘fake’ abembeleza mastaa wamfollow kwenye Twitter

Inaonekana muigizaji wa filamu Elizabeth ‘Lulu’ Michael ameingia location kufanya filamu yake inayoaminika kuwa ya kwanza tangu atoke mahabusu mwezi January mwaka huu.

Kupitia Instagram, juzi Lulu ameshare picha inayomuonesha akiwa location na muigizaji Hashimu Kambi na kuandika, take 1 action, Mic location, me doing my thng.”

Katika hatua nyingine, Lulu amelalamika kuwepo kwa akaunti fake ya Twitter yenye jina lake iitwayo @Lulu_actress. “Haya lulu mwingne huyo on twitter…..!am tired jaman…nyie ma lulu nioneeni huruma basi…..!!!nimechoka kusikia case’z zenu!!!!NIMECHOKA JAMANI ,” ameandika Lulu kupitia Instagram.

Katika akaunti hiyo Fake, mtu huyo ameandika profile yake isemayo: Am a bongo movie actress|caring,loving and loved lady| latest movie coming soon by the name The end of tourture| starring wil be me and jb (imechukuliwa kama ilivyoandikwa).

Akaunti halisi ya Lulu kwenye mtandao wa Twitter ni ile yenye jina @hotlulumichael..

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...