Thursday, April 11, 2013

KUMBUKUMBU YA KANUMBA SHIJA ALEWA NJWIII....

MSANII kutoka Kiwanda cha Filamu Bongo, Deogratius Shija hivi karibuni amenaswa akiwa amelewa pombe tilalila kwenye kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kufariki kwa marehemu Steven Kanumba.

Deogratius Shija akiwa 'bwii'.

Tukio hilo lilitokea kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni, jijini Dar ambapo mwigizaji huyo alionekana akiwa ameshikilia chupa kadhaa za ulabu akijidunga kwa raha zake bila kujali waalikwa wengi walikuwa katika sura ya majonzi. Akizungumza na paparazi wetu baada ya kuulizwa kulikoni kulewa kiasi hicho, Shija alijitetea na kujisemea anajiona yupo kawaida hajalewa huku akiwa anauficha uso wake ili asipigwe picha. “Yaani sitaki kabisa kuandikwa magazetini jamani hapa najiona niko kawaida sijalewa sana ila nakunywa tu kama kupoteza mawazo hapa,” alisema Shija.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...