Thursday, April 11, 2013

BABA ADAI HAITAMBUI NDOA YA BINTIYE!...

SALIEL Athanas Tillya, mkazi wa Temeke, Dar es Salaam ameibuka na kudai haitambui ndoa ya binti yake Helen Tillya (25) na Paul Komando iliyofungwa hivi karibuni akidai kwamba, binti yake huyo alimtenga yeye na kumtafuta mwanaume asiyejulikana na ukoo wao.

Bibi Harusi akimiminiwa kinywaji.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa ndani ya ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge, Dar mapema wiki hii baada ya ndoa hiyo kufungwa, mzee Tillya alisema: “Mimi ndiye baba mzazi wa Helena, naitwa Saliel Athanas Tillya. Nasema siitambui ndoa ya binti yangu kwa sababu sina baraka nayo, amechumbiwa kwa siri, amefunga ndoa kwa siri. “Mimi baba niko Dar es Salaam lakini simfahamu huyo bwana harusi na sijui anaitwa nani. Mbaya zaidi siku ya ndoa akapelekwa mwanaume gani sijui, akatambulishwa kama baba mdogo na ndiye msimamizi mkuu wa familia ya Tillya wakati akina Tillya wenyewe tupo.

Dk. Asha Rose Migiro naye alikuwepo katika harusi hiyo.

“Wanaposema ni baba mdogo, ina maana ni mdogo wangu mimi. Katika uzao wa baba na mama tupo saba tu, kuna Hery, yupo Arusha, Hezron yupo Temeke, Nicholas yupo Temeke. “Wengine ni Nivuaeli, Jenorois na Vailet, sasa huyo amesimamia wapi katika hawa?” alihoji mzee huyo. Aidha, mwandishi alimuuliza mzee kama anaishi na mama mzazi wa Helen ambapo alijibu kwa kusema: “Tulitengana kwa ugomvi mkubwa Julai 12, 2012. Wakati Helen akiwa masomoni nchini Uingereza nilikompeleka kwa fedha zangu. Aliporudi na kukuta nimetengena na mama yake na yeye akanikana, akasahau wema wangu wa kumsomesha. Mungu yupo.” Mwandishi: Unadhani kwa nini binti yako hakutaka kukujulisha lolote kuhusu kuchumbiwa kwake hadi ndoa? Baba: Alishajazwa maneno mabaya, nikawa kama adui yake. We fikiria toka amerudi Uingereza tumeonana mara moja tu, ndiyo maana nimesema Mungu yupo.

Baba anayedaiwa kuwa feki akiwa harusini hapo.

ILIVYOKUWA SIKU YA SEND OFF Send Off ya Helen ilifanyika Aprili 4 kwenye Ukumbi wa Sunset (Twiga Hall) uliopo Mbezi, jijini Dar. Matukio yaliyojitokeza siku hiyo ni pamoja na waalikwa kuhoji aliko baba mzazi wa bibi harusi kwani walijua anaishi Dar. Licha ya baba mzazi na ndugu wengine kuisusa sherehe hiyo, mama mzazi kwa upande wake alijitokeza na kupozi na baba mdogo huyo ambaye hakuwa akijitaja jina kila walipohitajika wazazi wa Helen.

BABA MZAZI ASAKWA UKUMBI MZIMA Muda mfupi baada ya shamrashamra ulifika wakati wa utambulisho ambapo bibi harusi ndiye aliyekuwa akiwatambulisha ndugu zake na kuanza kumtambulisha mama. Waalikwa walitaka kusikia kuhusu baba lakini Helen aliliminya suala hilo na kusababisha minong’ono ukumbini.

Mama mzazi wa Bibi Harusi akipokea keki.

SIKU YA NDOA Ndoa ya Helen na Paul ambayo pia ilihudhuriwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Asharose Migiro, ilifungwa Aprili 6 ndani ya Kanisa la Mtakatifu Joseph, Dar na kufuatiwa na sherehe zilizofanyika katika Ukumbi wa Sunset (Flamingo Hall). Alipogiwa simu Helen na kusomewa madai ya baba yake alijibu kwa kifupi: “Mimi sijui chochote kuhusu hilo

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...