Thursday, April 11, 2013

JOKATE AZIDIWA KANISANI

MWANAMITINDO ‘expensive’ Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ alizidiwa ghafla kwenye ibada ya kumkumbuka marehemu Steven Kanumba iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Kimara – Temboni, jijini Dar.

Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.

Jokate ambaye awali alikuwa mzima wa afya, alifika kwa ajili ya kujumuika na familia ya marehemu akiwa na lengo la kukamilisha siku yake kwa kwenda makaburini na baadaye katika Viwanja vya Leaders kulipokuwa na shughuli maalum ya kumkumbuka Kanumba lakini alishindwa baada kuzidiwa ghafla. “Nafikiri alikuwa na uchovu maana anaonekana alikuwa amefanya kazi nyingi mfululizo kwani alipopelekwa kupumzika ndani ya muda mfupi alijisikia vizuri,” alisema mmoja wa rafiki wa staa huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...