Thursday, April 11, 2013

PART YA KAJALA MMMH

SIKU chache baada ya kuingia uraiani, staa wa filamu, Kajala Masanja amefanyiwa bonge la pati la kumkaribisha uraiani ambalo limezua miguno kwa waalikwa kutokana na kufuru ya fedha na matukio yaliyojiri.

Tukio hilo lililohudhuriwa na mastaa kibao lilijiri Aprili 9, mwaka huu katika Ukumbi wa Ambassadors uliopo Mikocheni, jijini Dar chini ya usimamizi wa Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’. Siku ya tukio, Wema akiwa ameambatana na wapambe wake waliuandaa ukumbi huo kwa mapambo, vinywaji, keki maalum iliyokuwa na maandishi yaliyosomeka; Welcome Back Kajala, ambapo muda ulipofika Kajala alianza kuwalisha baadhi ya mastaa ambao ‘walitimba’.

Chanzo chetu kilichoshuhudia tukio hilo kilidai kuwa, siku hiyo Wema aliteketeza mamilioni ya fedha kufanikisha tukio hilo lililokwenda hadi usiku mnene ambapo watu walijiachia ile mbaya. Kama hiyo haitoshi, kufuru nyingine ilifanywa na Kajala ambaye alibusiana kimahaba zaidi na mwigizaji Aunt Ezekiel kwa sekunde kadhaa huku wakionekana kama wamepitiliza kihisia za ‘kimalovee’ hali ambayo iliwafanya watu wahoji kulikoni!

“Jamani sasa kile nini tena wanafanya Kajala na Aunt? Utambusu vipi mwanamke mwenzako kwa staili ile ya njiwanjiwa? Hawa wasanii wetu jamani mhh!” alisikika mmoja wa waalikwa aliyekuwa eneo la tukio.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...