Wednesday, February 6, 2013

MATUMAINI AKWAMA KUTUA BONGO

INGAWA taratibu za kumrejesha nchini msanii wa vichekesho, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ aliyeko Msumbuji kukamilika, amekwama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo kutokana na kutokuwa na hati ya kusafiria.
Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’.
Matumaini yupo nchini humo ambapo inaelezwa kuwa ni mgonjwa na hali yake ni mbaya, hivyo ndugu zake kwa kushirikiana na wasanii kufanya taratibu za kumrejesha nchini.
Habari zinasema kwamba, taratibu za kumrudisha nchini zilikamilishwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla ambaye alitoa tiketi lakini Matumaini alikwama kwa kukosa hati ya kusafiria.

Wakati ndugu na wasanii wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar juzi Jumapili wakimsubiri ndipo taarifa zilipofika na kueleza kwamba amekwamishwa na hati ya kusafiria.
Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania, Michael Sangu ‘Mike’ ndiye aliyetoa taarifa hiyo akieleza amejulishwa na mtu aliyekuwa akishughulikia safari yake aliyeko jijini Maputo, Msumbiji.

Mike alisema: “Kila kitu kilikuwa tayari, tatizo ni mtu aliyepewa jukumu la kufuatilia pasipoti, hakuonekana airport, hivyo mtu anayehusika na vibali alikataa katakata kumruhusu kusafiri pamoja na kupewa maelezo mengi.”
Taarifa hiyo ilisababisha machozi kugubika miongoni mwa wasanii na ndugu wa msanii huyo, lakini juhudi zaidi za kufanikisha kurejeshwa nchini zinaendelea kufanyika.No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...