Wednesday, February 6, 2013

MANUMBA ALAZWA HOSPITALI ALIYOLAZWA MANDELAKwa mujibu wa chanzo chetu makini, DCI Manumba alisafirishwa kutoka Hospitali ya Aga Khan jijini Dar siku kadhaa zilizopita kwa kutumia gari maalum la kubebea wagonjwa hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere alikopakizwa kwenye ndege maalum ya Kampuni ya AAR kuelekea Bondeni baada ya afya yake kutengemaa kidogo.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Jaffer Dharsee, Manumba alisafirishwa baada ya kupata ahueni kidogo huku akiwa na uwezo wa kuchezesha viungo mbalimbali vya mwili wake, tofauti na hali aliyokuwa nayo awali.
Manumba alifikishwa hospitalini hapo Januari 13, mwaka huu baada ya kuhamishwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, akiwa anasumbuliwa na malaria kali (vijidudu 500) vilivyosababisha figo zake mbili zipoteze uwezo wa kufanya kazi na kupoteza fahamu.

Hospitali ya Milpark jijini Johannesburg, Afrika Kusini alipolazwa DCI Manumba.
Uchunguzi uliofanywa na Risasi Mchanganyiko, umebaini kuwa hospitali aliyopelekwa kiongozi huyo wa jeshi, Milpark ina uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa ya dharura kama mshtuko wa moyo, mtikisiko wa ubongo, kiharusi, kupooza, kupandikiza figo na mapafu na matatizo mengine yanayohusu mfumo wa fahamu.
Hospitali hiyo yenye wodi 90 za wagonjwa mahututi, madaktari wazoefu na vifaa vya kisasa vya tiba, ikiwa na historia ya kuwatibu watu wengi mashuhuri barani Afrika, inatajwa kutoa huduma bora zaidi.
Miongoni mwa watu mashuhuri waliowahi kutibiwa hospitalini hapo, ni Rais wa Kwanza Mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ambaye alilazwa Januari 25, mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...