Wednesday, February 6, 2013

BONGO MOVIES KUFANYA BONANZA
Wasanii wa sanaa za maigizo nchini ‘Bongo Movies’ wanatarajia kufanya bonanza litakalohusisha michezo mbalimbali kwa kushirikiana na wafanyakazi wa mahoteli ya kitalii jijini Dar es Salaam.
Akipiga stori na kona hii wikiendi iliyopita, Katibu Mkuu wa Chama cha Waigizaji Tanzania, Christian Kauzeni alisema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuleta ushirikiano endelevu kati ya wasanii na wafanyakazi wa mahoteli.
Alisema: “Litafanyika Jumamosi ya Februari 9, mwaka huu katika Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama. Kutakuwa na michezo mbalimbali kama pete, mpira wa miguu  na michezo mingine mingi.”

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...