Friday, September 14, 2012

STORI KAMILI KUHUSU KOCHA ALIETIMULIWA AZAM KUPATA KAZI KENYA.


President wa Sofapaka Elly Kalekwa akimpokea kocha Stewart Hall kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata Nairobi Kenya. (Picha ya michezo Afrika)
Aliekua kocha wa Azam Fc ya Tanzania kabla ya kutimuliwa siku kadhaa zilizopita Stewart Hall ametangazwa kuwa kocha Mkuu wa club ya Sofapaka ya Kenya.
Ndio anachukua nafasi ya kocha Salim Ali ambae alipigwa chini kwenye club hiyo baada ya kuwa na matokeo mabaya.
President wa Sofapaka Elly Kalekwa amesema Stewart anarekodi nzuri ya ukocha ndio maana wamevutiwa kumchukua ambapo akiwa na Azam aliiwezesha kushinda kombe la Mapinduzi, wakamaliza kwenye nafasi ya pili  Urafiki Cup, Vodacom Premier League and Kagame Cup.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...